settings icon
share icon
Swali

Utetezi wa Plantinga wa hiari huru ni gani, na ni namna gani unashughulikia tatizo la uovu?

Jibu


Alvin Plantinga aliyezaliwa mwak wa 1932, ni mwanafalsafa na amekuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Calvin na Chuo Kikuu cha Notre Dame. Anasifiwa kwa kuunda jibu pana na linaloheshimiwa sana kwa “tatizo la kimantiki la uovu.” Jibu hili linajulikana kama utetezi wa hiari huru. Tatizo la kimantiki la uovu linadai kuwa kuwepo kwa uovu hakupatani kabisa na kuwepo kwa Mungu. Ili kushinda shambulio kama hilo, ni muhimu kuonyesha kwamba kimantiki inawezekana uovu kuwepo, hata kama wema upo. Kama vile ilivyokubaliwa na idadi kubwa ya wasomi- wakanamungu au labda-utetezi wa Plantinga wa hiari huru hutimiza lengo hili. Ingawa hii haiondoi aina zote za tatizo la uovu, utetezi wa Plantinga hubadalisha uwezo wake.

Tatizo la kimantiki la uovu linadai kwamba, kutokana na kuwepo kwa Mungu mwenye uwezo wote, mwenye upendo wote, kuna uwezekano wa kuwepo kwa ouvu. Ikidhihirishwa kwa njia mbalimbali, hii labda ndiyo mbinu inayotumiwa sana katika majaribio ya “kuthibitisha” kwamba Mungu hayupo.

Utetezi wa Plantinga kwa hiari huru unabishi kwamba shambulio hili halijakamilika kimantiki na kwa hivyo halifai. Kimantiki hakuna wazo-hakuna ufafanuzi kamili, wa asili-ambao unadai kwamba Mungu hawezi “kuruhusu” uovu. Ili afanye ukosoaji wake usikike, mwenye anadai kwamba Mungu hawezi kuwa mwenye mamlaka yote na mema na mabaya yote yawepo, hana budi kudhania jambo fulani kumhusu Mungu zaidi ya kauli hiyo. Kuna dhana iliyofichwa-dhana iliyoachwa bila kutajwa: dhana kwamba hakuna kabisa sababu ya Mungu mwenye uwezo wote na mwema, anaweza kuruhusu uovu. Hata hivyo, dhana hiyo inaweza kuwa au isiwe ya busara. Zaidi ya hayo, huenda isilingane na asili ya Mungu kama inavyoelezwa na wale wanaomwamini.

Plantinga anabishi kwamba hiari huru ya kuchagua hutoa sababu inayowezekana ya kimantiki kwa Mungu mwenye uwezo wote, mwenye ujuzi wote, na wema wote na kuruhusu kuwepo kwa uovu wa kiadili. Uweza wa Mungu haumaanishi ukinzano wa kimantiki, kama vile kufanya mduara wa mraba. Kwa maoni ya Plantinga, mtu anayeweza kutenda dhambi kiadili ni kiumbe asiye na hiari huru. Kwa hiyo, ni jambo la busara kusema kwamba Mungu anaweza kufanya dhambi isifanyike, au Anaweza kuniweka huru, bali hawezi kufanya zote kwa pamoja. Utetezi wa hiari huru unapendekeza uwezekano kwamba, kwa Mungu, uwezo wa mwanadamu wakufanya maamuzi ya kimaadili ni kitu kilicho cha kipaumbele-na sharti la muhimu zaidi la kimaadili-kuliko ulimwengu usio na uovu kabisa.

Kwa maneno mengine nia ya Muumba ya kutaka kuwapa wanadamu uhuru wa kuchagua hudokeza uwezekano wa kuwepo kwa uovu katika ulimwengu ulioumbwa na Mungu mwema na mwenye nguvu zote.

Iwe kweli au isiwe kuhusu uwezekano uliotamkwa na Plantinga, hauhusiani na thamani yake kama tetezi. Tatizo la kimantiki la uovu hufanya madai kulingana na mantiki; utetezi wa hiari unaonyesha kuwa unashindwa, kwa misingi ya kimantiki. Mtu halazimiki kukubali maoni yote ya Plantinga ili kutambua kwamba-kimantiki utetezi wake unafaulu kushinda toleo hilo hususani tatizo la uovu.

Ni muhimu kutambua kwamba utetezi wa Plantinga wa hiari huru ni kwamba: “utetezi.” Kwa hivyo hautumiki kuhalalisha matendo yoyote mahususi ya Mungu. Utetezi hasa hutawanya tu shambulio, na kulifanya kuwa dhaifu. Utetezi wa hiari huru hauthibitishi kwamba Mungu yupo, lakini unathibitisha-kwa maneno ya wazi kabisa kwamba hakuna ukinzano wa kimantiki kati ya Mungu mwema, mwenye mamlaka yote na kuwepo kwa uovu wa maadili. Wanafalsafa, hata wasioamini kuwa kuna Mungu, wamekiri hivyo hadharani.

Utetezi wa hiari huru wa Plantinga umejulikana tangu alipochapisha toleo lake mara ya kwanza mnao mwaka wa 1977. Hilo halijazuia watu wengi kutumia tatizo la kiakili la uovu kuwa shambulio dhidi ya Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba tatizo la kimatiki la uovu bado lipo kwa maana ile ile- na kwa sababu zile zile-kwamba bado kuna mjadala kuhusu iwapo dunia ni tambarare au la. Ni wale tu wanaokosa mtazamo na habari wanaojaribu kudai kwamba Mungu na uovu hawapatani kimantiki.

Kwa kusema hayo, tatizo la uovu linahusisha mengi zaidi ya uwezekano kamili. Baadhi ya wakosoaji wa Mungu walitoa madai yenye utata zaidi kwamba kuwepo kwa Mungu ni jambo lisilo sawa (badala ya kuwa haliwezekani), kutokana na kuwepo kwa uovu. Hili, bila shaka, ni pingamizi lisilo na nguvu sana. Pia ni mojawapo la utetezi wa hiari huru wa Plantinga haukusudiwi kukabiliana. Ndio uelewe Maandiko zaidi vile yanavyojibu tatizo la uovu lazima uangalie suala hili kutoka kwa mtazamo huu; vivyo hivyo, madai kwamba uovu na Mungu havipatani huitaji zaidi ya utetezi tupu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Utetezi wa Plantinga wa hiari huru ni gani, na ni namna gani unashughulikia tatizo la uovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries