settings icon
share icon
Swali

Utengano kibiblia ni nini?

Jibu


Kutengana kibiblia ni kutambua kwamba Mungu amewaita waumini kutoka hali ya dunia na katika usafi wa kibinafsi na ushirika katikati ya tamaduni za dhambi. Kutenganaa kibiblia kawaida huchukuliwa katika maeneo mawili: wa kibinafsi na wa Kikanisa.

Kujitenga kwa kibinafsi unahusisha juhudi za mtu binafsi kwa kiwango cha kanuni cha maadili ya kiungu. Danieli aliweka katika mazoezi utengano wa binafsi wakati yeye "Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa" (Danieli 1:8). Yake ilikuwa kujitenga kwa kibiblia kwa sababu maadili yake ni kwa niaba ya ufunuo wa Mungu katika sheria ya Musa.

Mfano wa kisasa wa kujitenga kibinafsi unaweza kuwa uamuzi wa kukataa mialiko ya sherehe ambapo mvinyo unatumikia. Uamuzi wa aina hiyo unaweza fanywa ili kukwepa majaribu (Warumi 13:14), ili kuepuka "kila aina ya uovu" (1 Wathesalonike 5:22), au tu kuwa thabiti katika ule ushawishi wa kibinafsi (Warumi 14:5).

Biblia inafundisha wazi kwamba mtoto wa Mungu anastahili kujitenga na dunia. "Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maan pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tean pan ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja nay eye asiyeamini? Teena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maan sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea name nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, msiguze kitu kilicho kichafu, name nitawakaribbisha, asema Bwana "(2 Wakorintho 6:14-17; angalia pia 1 Petro 1:14-16).

Kujitenga Kikanisa kunahusisha maamuzi ya kanisa kuhusu uhusiano wake na mashirika mengine, kwa kuzingatia theologia yao au matendo. Utengano umeonyeshwa katika neon hilo hilo “kanisa," ambalo latoka kwa neon la Kigiriki ekklesia likimaanisha “Aitwaye –toka kwa mkusanyiko." Waraka wa Yesu kwa kanisa la Pergamo, aliwaonya kwa kuruhusu wale waliofunza mafundisho ya uongo (Ufunuo 2: 14-15). Kanisa lilikuwa lijitenge , kuvunja uhusiano na uzushi. Mfano wa kisasa wa Kanisa kujitenga unaweza kuwa msimamo wa dhehebu dhidi ya ushirikiano wa kiekumeni ambao utaunganisha kanisa na waasi.

Kujitenga kibiblia hauhitaji Wakristo wasiwe na mawasiliano na wasio amini. Kama Yesu, tunapaswa kuwa na urafiki na wenye dhambi bila kushiriki dhambi (Luka 7:34). Paulo anaelezea mtazamo wa uwiano wa kujitenga: " Niliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maan hapo ingewalazimu kutoka katika" (1 Wakorintho 5:9-10). Kwa maneno mengine, sisi tuko duniani, lakini si wa dunia.

Sisi ni kuwa mwanga wa ulimwengu bila kuruhusu dunia kupunguza mwanga wetu. "Nyinyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yanu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni" (Mathayo 5:14-16).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Utengano kibiblia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries