settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya utaratibu wa teolojia?

Jibu


“Mfumo” wamaanisha kitu ambacho kimewekwa kwa utaratibu. Utaratibu/mfumo wa teolojia kwa hivyo ni mgao wa teolojia katika utaratibu unaoelezea sehemu zake mbalimbali. Kwa mfano, vitabu vingi vya bibilia vinatoa habari kuhusu malaika. Hakuna kitabu hata kimoja kinachotoa habari yote kuhusu malaika. Utaratibu/mfumo wa teolojia wachukua habari zote kuhusu malaika kutoka vitabu vyote vya Bibilia na kuipanga kwa mfumo huitwao mfumo wa malaika. Huu ndio wajibu wa taratibu ya teolojia yahusika-kupanga mafunzo ya Bibilia kwa vitengo.

Teolojia halisi ni udadisi wa Mungu Baba. Kristolojia ni udadisi wa Mungu Mwana, Bwana Yesu Kristo. Niumatolojia (Pneumatology) ni somo la Mungu Roho Mtakatifu. Bibiliojia (Bibliology) ni somo la Bibilia. Soteliolojia (Soteriology) ni somo la wokovu. Ekilesia (Ecclesiology) ni somo la kanisa. Esikatolojia (Eschatology) ni somo la nyakati za mwisho. Anchelolojia (Angelogy) ni somo la malaika. Ukristo-mapepo (Christian demonology) ni somo la mapepo kutoka mtazamo wa Kikristo. Anthropolojia (Anthropology) ni somo la wanadamu kutoka kwa mtazamo wa Kikristo. Hamatiolojia (Hamartiology) ni somo la dhambi. Utaratibu wa Bibilia ni silaha muhimu ya kutusaidia kuelewa na kufunza bibilia kwa njia ya mpangilio.

Kwa kuongezea juu ya utaratibu wa teolojia, kuna njia nyingine ambazo teolojia inaweza kugaganywa. Teolojia ya kibibilia ni somo fulani la Bibilia na kutia mkazo sehemu mbalimbali za teolojia inayoangazia. Kwa mfano, Injili ya Yohana inaelezea sana kuhusu Yesu kwa vile inaangazia uungu wa Kristo (Yohana 1:1, 14; 8:58; 10:30; 20:28). Historia ya teolojia ni somo la kanuni na namna zimejipuka katika karne nyingi ya kanisa. utaratibu wa teolojia ni somo la kanuni za mfumo wa teolojia. Teolojia ya kisasa ni somo la kanuni ambazo zimejipusa au zimekuwa zikiangaziwa hivi karibuni. Haijalishi ni mtindo gani wa teolojia unasomwa, kilicho cha muimu ni teolojia imedadisiwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya utaratibu wa teolojia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries