Swali
Wakristo wanastahili kuwa wastahimilifu kwa imani za dini za watu wengine?
Jibu
Katika kisasi chetu “ustahimilifu,” tabia ya imani kwamba maarifa na maadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati kuwa maadili ya juu sana. Kila falsafa, hoja, na mifumo ya imani iko na alama sawa, anasema anaye shikilia kuwa maarifa na madili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati, ni yanastahili kuwa na heshima sawa. Wale wanaopendelea mfumo mmoja wa imani kuliko mwingine au kusema kuwa ufahamu wa ukweli wote umechukuliwa kuwa wa mafikira finyu, bila ufahamu wo wote, au hata kuwa ya ukole.”
Hata hivyo, madini mbalimbali kwa umoja wanafanya tangazo kuwa na maarifa na maadili ni mambo ya mpito hayawezi kuunganisha tatanisho lo lote. Kwa mfano, Bibilia yasema kuwa “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa maramoja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:29), huku madini ya Mashariki yakifunza kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine. Kwa hivyo tunakufa mara moja au mara nyingi? Mafunzo yote hayawezi kuwa kweli. Anayeshikilia kuwa maarifa na maadili ni mambo ya mpito kimsingi wanaelezea ukweli ili waanzishe ulimwengu wa kisadifa mahali ambapo mambo mengi, “kweli” inayochichanganya inaweza kuwepo.
Yesu alisema, “Mimi ndimi njia na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6). Mkristo amekubali ukweli si eti ni dhana, lakini kama mtu. Ufahamu huu wa ukweli unamtenga Mkristo kutoka kile kinaitwa “mawazo wazi” ya siku. Mkristo hadharani amekubali kuwa Yesu alifufuka kutoka kwa wafu (Warumi 10:9-10). Kama kwa kweli anaamini katika ufufuo, anawezaje tena kuwa “wa mawazo wazi” kuhusu mtu ambaye hajaokoka kuwa Yesu hakufufuka? Kwa Mkristo kukana mafunzo ya kweli ya neno la Mungu kwa kweli atakuwa akimsaliti Mungu.
Kumbuka kwamba tumetaja msingi wa imani yetu katika usoefu wetu kufikia hapa. Vitu vingine (kama ufufuo wa mwili wa Kristo) ni vitu havijadiliwi. Vitu vingine vinaweza kuwa wazi kwa mjadala, ni kama ni nani alikiandika kitabu cha Weabrania au hali ya “mwiba katika mwili wa” Paulo. Lazima tuepuke kufinyiliwa chini katika mapishano juu ya mambo ya pili (2 Timotheo 2:23; Tito 3:9).
Hata mnapo bishana juu ya kanuni mahususi, Mkristo lazima ajizuie na aonyeshe heshima. Ni kitu kimoja kutokubaliana na msimamo; vilevile ni kitu kingine kumshushia mtu. Lazima tushikilie kwanza ile kweli huku tukionyesha upendo kwa wale wanaoushuku. Kama Yesu, lazima tuwe na wingi wa neema na kweli (Yohana 1:14). Petero anafikia usawa kati ya kuwa na jibu na kuwa na ukarimu: “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu” (1 Petero 3:15).
English
Wakristo wanastahili kuwa wastahimilifu kwa imani za dini za watu wengine?