settings icon
share icon
Swali

Mbona usinzi katika ndoa in uharibifu?

Jibu


Usinzi katika ndoa, au kutokuwa na uaminifu, hutokea pale wakati mpenzi mmoja katika ndoa anatoka nje ya ndoa na kushiriki katika uhusiano wa kingono na mtu mwingine. Angalau kila mtu anaelewa kuwa kutokuwa na uaminifu katika ndoa sio mzuri; tafiti nyingi zinaonyesha kuwa takribani asilimia 90 ya Wamarekani, Mkristo au wasio Wakristo Wanaamini kuwa usinzi katika ndoa si sahihi. Hata hivyo, kusema kihesabu, kati ya asilimia 30 na 50 ya Wamarekani watawadanganya wapenzi wao. Kuna sababu kadhaa za watu wanaohusika katika uzinzi, lakini wingi wa matukio hayo hutokea kwa sababu ya haja ya kushikamana kihisia. Wanadamu wana haja ya kina ya kutakwa, hitajika, na kueleweka. Kwa kweli, haja hii inatimizika katika uhusiano wa ndoa. Ikiwa haja haitimizwi katika ndoa, mke anaweza kuangalia kwingine ili kuhusiana kihisia (na kimwili), ambako hii husababisha kutokuwa na uaminifu katika ndoa.

Usinzi katika ndoa hauelekezi katika furaha. Mungu alifanya ngono ili ifurahikiwe ndani ya uhusiano wa ndoa wa kujitolea; kuondoa ngono kutoka kwa hali hiyo ni kupotosha matumizi yake na kupunguza kikamilifu furaha yake. Kujamiana kwa ngono kunahusisha kiwango cha urafiki usiowezekana katika uhusiano wowote wa kibinadamu. Wakati Mungu aliwaletwa Adamu na Hawa pamoja katika ndoa, alianzisha uhusiano wa "mwili mmoja". Mwanzo 2:24 inatuambia kwamba mtu anapaswa kuacha familia yake, na kujiunga na mkewe, na kuwa "mwili mmoja" pamoja naye. Wazo hili linafanyika kupitia Agano Jipya pia; tunaona katika maneno ya Yesu katika Mathayo 19: 5 na Marko 10: 7. Paulo anaelezea wazo la "mwili mmoja" katika 1 Wakorintho 6: 12-20. Anasema kwamba wakati mtu anakuwa na ngono na kahaba, wamekuwa "mwili mmoja" (mstari wa 16). Ni wazi kwamba kuna kitu maalum katika uhusiano wa ngono; si utenda kazi tu wa kibiolojia.

Usinzi katika ndoa ni uharibifu sana kwa ndoa kwa sababu watu wawili huwa "mwili mmoja" huhusisha zaidi ya urafiki wa kimwili tu. Wakati wa ngono, kuna ushirikiano wa hisia na miili. Uthabiti wa Agano la Kale kwa ngono unahusisha neno "kuonana" kimwili-neno muhimu. Wakati wa ngono, kutaniko la karibu zaidi la binadamu, mtu anaweza kusema "kweli" ninamjua mtu mwingine vizuri. Kiwango cha uaminifu kinachohitajika kwa tendo hili kunamfanya mtu awe mshtuko mkubwa, na hii ndio mojawapo ya sababu ni kwa nini ngono lazima iwe kwenye uhusiano wa ndoa. Ndoa inaruhusu uwezekano wa kuwa hatarini bila hofu; kila mwanandoa anahifadhiwa na ahadi ya mwingine na utulivu wa asili katika uhusiano wa agano. Kuvunja imani hiyo kwa njia ya usinzi ni mbaya kwa mtu binafsi na kwa ndoa. Ni usaliti wa ujasiri, kuvunja ahadi, kupoteza usalama, na kuyumbisha muungano.

Usinzi katika ndoa sio moja kwa moja kifo cha ndoa. Ripoti zinasema kuwa asilimia mia 60 hadi 75 ya wanandoa ambao wamepata kusalitiwa hukaa pamoja. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa mahusiano haya yameponywa au kwamba uaminifu na kujitolea vimepatikana tena. Mara nyingi, wanandoa hukaa pamoja baada ya kuadiliana kwa ndoa si kwa sababu wanafurahi pamoja lakini kwa sababu wanaogopa njia mbadala. Hata hivyo, kuna wanandoa wengine ambao hufanya juhudi zaidi za kukabiliana na shida hiyo, wakitambua udhaifu, na kurekebisha makosa. Wanandoa hao wana nafasi nzuri sana ya kukaa pamoja lakini hupitia mchakato na kuja kwenye ndoa yenye nguvu, yenye furaha, yenye utimilifu.

Ni muhimu kumbuka kwamba usinzi katika ndoa, kama dhambi zingine zote, unaweza kusamehewa. Mzinzi awe mke au bwana hayuko mbali na neema ya Mungu haiwezi mfikia (Isaya 59: 1). Vile mwenye dhambi anapotububu na Mungu kumsamehe, mpenzi aliyesalitiwa pia anastahili kusamehe. Yesu alisema kwamba, ikiwa hatutasamehe dhambi za wengine, dhambi zetu wenyewe hazitasamehewa (Mathayo 6:15). Ili "kusamehe na kusahau" sio ya kawaida, na sio rahisi. Njia ya urejesho itakuwa ndefu na yenye uchungu. Lakini neema ya Mungu daima inatosha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mbona usinzi katika ndoa in uharibifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries