settings icon
share icon
Swali

Je, ushirika unapaswa kuwa wazi au kufungwa?

Jibu


Tofauti kati ya ushirika "wazi" na "umefungwa" unategemea mtazamo wa kanisa kuhusu madhumuni ya ushirika na mamlaka ya kanisa. Makanisa ambayo hufanya ushirika "wazi" wanaalika waumini wote wanaokiri katika Kristo kujiunga nao katika kufuata sheria. Makanisa ambayo hufanya ushirika "umefungwa" wanaweka vipimo vha kujihusisha katika Meza ya Bwana/Pasaka kwa mwili wa mtaa wao wenyewe- wanachama rasmi tu walio katika msimamo mzuri wanaruhusiwa kushiriki. Makanisa mengine hufanya aina ya tatu, ambayo wanaita ushirika wa "karibu"; katika ushirika wa "karibu" wanachama wa makanisa mengine katika dhehebu moja wanaruhusiwa kuvunja mkate pamoja na wanachama wa kanisa la mtaa.

Mafundisho ya Biblia juu ya Meza ya Bwana/Pasaka hupatikana katika 1 Wakorintho 11:17-34 na inakuza ushiriki wazi kwa waumini. Wale wote ambao ni waumini wa kweli katika Mungu kwa njia ya imani binafsi katika Yesu Kristo, Mwana Wake, wanastahili kushiriki Meza ya Bwana kwa sababu ya ukweli kwamba wamekubali kifo cha Kristo kama malipo ya dhambi zao (tazama pia Waefeso 1:6-7).

Sababu nyuma ya makanisa mengine kufanya ushirika umefungwa au wa karibu ni kwamba wanataka kuhakikisha kila mtu anashiriki ni mwamini. Hili linaeleweka; hata hivyo, linaweka uongozi wa kanisa na/au mabawabu wa kanisa katika nafasi ya kuamua ni nani anayestahili kushiriki, ambayo ni tatanishi kwa ubora. Kanisa fulani linaweza kuchukulia kwamba wajumbe wao wote rasmi ni waumini wa kweli, lakini dhana hiyo inaweza au haiwezi kuwa kweli.

Mazoezi ya ushirika umefungwa- kuzuia ushirika kwa wajumbe wa kanisa-pia ni jaribio la kuhakikisha mtu asishiriki "kwa njia isiostahili" (1 Wakorintho 11:27). Makanisa ya ushirika-umefungwa huzingatia kwamba mwili wa mtaa pekee una uwezo wa kuamua ustahili wa kiroho wa wanachama wake; hakuna njia ya kuamua hali ya kiroho ya wa nje au wageni. Hata hivyo, 1 Wakorintho 11:27 inaelezea namna ambavyo mtu anakula mkate na kikombe, si kwa kustahili kwake binafsi. Hakuna mtu "anastahili" kushiriki na Mungu; ni kwa sababu ya damu iliyomwagika ya Kristo kwamba tumefanywa kustahili. Njia ya kushiriki inakuwa haistahili wakati waumini fulani wanatengwa (mstari wa 21), wakati washiriki wanakataa kugawana (mstari 21), wakati ulevi unahusika (mstari wa 21), wakati masikini wanadhalilishwa (mstari wa 22), wakati ubinafsi unakuzwa (aya ya 33), au wakati mkusanyiko utaonekana kama chakula tu ili kukidhi njaa (mstari wa 34).

Kibiblia, ushirika unapaswa uwe wazi kwa waumini wote, si kufungwa kwa kanisa fulani au dhehebu. Kilicho muhimu ni kwamba washiriki ni waumini waliookoka kutembea katika ushirika na Bwana wao na kwa kila mmoja. Kabla ya kushiriki kwenye ushirika, kila muumini anapaswa kujichunguza mwenyewe nia zake (1 Wakorintho 11:28). Haijalishi kanisa la mtu ni gani, kutohusu, chuki, ubinafsi, na tamaa hazina nafasi katika meza ya Bwana.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ushirika unapaswa kuwa wazi au kufungwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries