settings icon
share icon
Swali

Je! Ubatizo unahitajika kabla ya mtu kupokea ushirika?

Jibu


Haielezwi katika Maandiko kwamba mtu lazima abatizwe kabla ya kuweza kupokea Meza ya Bwana. Hata hivyo, mahitaji sawa kwa ubatizo pamoja na kushiriki katika Meza ya Bwana ni wokovu kupitia imani katika kifo, kuzika na kufufuliwa kwa Yesu Kristo.

Meza ya Bwana ilianzishwa na Yesu vile alikuwa akila chakula cha Pasaka pamoja na wanafunzi Wake jioni kabla ya kusulubiwa kwake (Mathayo 26: 20-28). Katika Mathayo 28:19, baada ya kifo na ufufuo wa Bwana wetu, alitoa Tume Kubwa kwa wanafunzi Wake kwenda ulimwenguni kote na kufundisha injili yake. Yesu alifuatilia tume kwa amri ya kubatiza waumini wapya. Ubatizo wa maji kwa jina la Utatu umefanywa na kanisa tangu mwanzo. Mahitaji pekee, kama ilivyoelezwa hapo juu, ni kwamba mtu amemwamini Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi. Ubatizo ni picha ya uzoefu wa wokovu na ni tendo la utii kwa Bwana wetu. Inachukuliwa na wasomi wengi wa Biblia kuwa hatua ya kwanza ya ufuasi wa Kikristo.

Meza ya Bwana ni njia ya waumini katika Kristo wanashiriki na Bwana wao na kukumbuka kifo Chake. Ubatizo ni alama muhimu ya kutambua waumini katika Kristo. Mtu ambaye hajawai kubatizwa anaeza kuwa muumini lakini hajajitambua wazi wazi kama mmoja au amechukua hatua ya kwanza ya utii kwa Kristo. Labda hii ndio sababu baadhi ya makanisa yanahitaji ubatizo kabla ya kushiriki Meza ya Bwana. Hata hivyo, tena, hakuna mahali Maandiko inatoa maagizo haya.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ubatizo unahitajika kabla ya mtu kupokea ushirika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries