settings icon
share icon
Swali

Kuadhimisha ulaji meza wa kwanza ni jambo la kibiblia?

Jibu


Hakika hakuna chochote ndani ya Maandiko ambacho kinazungumzia kuhusu "meza ya kwanza." Meza ya Kwanza ni sehemu ya mafundisho kwa watoto katika kanisa la Kirumi la Katoliki, na yametengezwa kama mojawapo ya sakramenti zao saba. Katika teolojia ya kanisa la Kirumi la Katoliki, sakramenti ni kitendo ambacho mtu hufanya ili kupata neema au kibali cha Mungu. Kabla mtoto aweze kuwa na ufahamu wowote juu ya dhambi, anabatizwa, sakramenti ya kwanza katika mfumo wa Katoliki ya Kirumi. Halafu atapitia katika taratibu ya masomo ya Katekisimu, baada ya hapo anafikia Kukiri kwake kwa kwanza. Hii inaitwa "upatanisho" au "toba" na hii ni Pamoja na kwenda kwa kuhani, kuungama dhambi kwake na kufanya toba yoyote au sala na matendo ambayo kuhani ataamuru. Ni baada ya hiyo ndipo Mkatoliki wa Kirumi anaweza kuanza kuchukua sakramenti.

Kinyume na haya, maandiko yanatuambia, "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu" (1 Timotheo 2:5). Hatuambiwi tukiri dhambi zetu kwa mtu yeyote ili azisamehe, bali kuomba na kukiri kwake Mungu. Ni katika Yesu Kristo tu ndio tunapata msamaha kamili na wa bure. Tito 3:5-6 ni mojawapo wa vifungu vingi ambavyo vinamtambulisha Yesu kama njia ya msamaha, wala sio ibada ya kidini.

Tunajifunza kuhusu Meza ya Bwana katika 1 Wakorintho 11:23-34. Ushirika Mtakatifu ni wa wale wanaomwamini Yesu Kristo na inapaswa kuzingatiwa kwa unyenyekevu. Kanisa la Korintho lilikua likitumia vibaya huduma hii, kwa hivyo Paulo, chini ya mamlaka ya Roho wa Mungu, aliandika kuhusu mtazamo tunapaswa kufuata katika ibada hii ya ukumbusho. Ni ibada ya ukumbusho ya Yesu Kristo, ambaye alikufa mara moja kwa ajili ya wote. Yeye haitaji kutolewa kafara tena, kama vile Misa ya Katoliki inavyojaribu kufanya. Yesu Kristo tayari alikufa, akazikwa, na akafufuka kutoka kwa wafu. Tunapotwaa mkate na kikombe "tunatangaza mauti ya Bwana hadi ajapo" (1 Wakorintho 11:26). Yeye yu hai leo, na tunaulizwa kukumbuka kila wakati tunaposhiriki Meza ya Bwana kwamba Yesu yu hai na yuaja tena.

Kwa hivyo, hakuna msingi wa kibiblia wa mila zilizotengenezwa na mwanadamu za "kukiri Kwanza" au "Ushirika mtakatifu wa Kwanza" kama vile Kanisa la Katoliki la Kiroma limeunda. Hata hivyo, kuna ukweli muhimu ambao Mungu anataka sisi sote tujue-Yesu Krsito alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na anataka tuje kwake tupate msamaha. Pia, anataka tushiriki katika Meza ya Bwana tukija kwake na kukumbuka tendo lake la mara moja la upendo wa msalabani Kalvari.

Ikiwa kuna uelewo mzuri wa ushirika mtakatifu, je! Kuna chochote kibaya au kisicho cha kibiblia juu ya kusherehekea ushirika mtakatifu wa kwanza wa mtoto? La, hakuna. Kwa kweli, kushiriki kwa kwanza kwa mtu katika ushirika mtakatifu ni jambo la kushangaza, inafaa kusherehekewa. Wakati mtu anaweka kibinafsi imani yake kwa Yesu Kristo, na kisha, kupitia ushirika mtakatifu, anamwabudu Mwokozi kwa kukumbuka kifo Chake na damu iliyomwagika, hakika hiyo itakuwa sahihi kutambua na kusherehekea.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuadhimisha ulaji meza wa kwanza ni jambo la kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries