settings icon
share icon
Swali

Wanandoa Wakristo wanapaswa kutafuta ushauri wa ndoa wakati gani?

Jibu


Wanandoa wowote walio na shida katika ndoa yao wanapaswa kutafuta ushauri haraka zaidi kuliko baadaye. Kila ndoa ina matuta na mizunguko kwamba ikiwa haitashughulikiwa kwa usahihi inaweza kuunda pengo pana sana la kuziba. Mara nyingi, aidha kwa kiburi au aibu, wanandoa hawatafuti msaada haraka kwa maswala wanayokabiliana nayo ili kuokoa ndoa yao. Wanasubiri mpaka uharibifu mkubwa umesababishwa kuwa ndoa tayari imekufa na mshauri ana kido sana la kufanya. Mithali 11:14 inasema, " Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu." Tunapopambana na vita kubwa sana kwetu peke yetu kivimudu, watu wa hekima wanatafuta ushauri wenye hekima.

Masuala ya mara kwa mara katika ndoa ni kama ishara za barabara za onyo ya hatari inayokuja. Baadhi ya ishara hizi za barabarani ni:
1. Kutokuwa na uwezo wa kutatua migogoro kwa njia njema.
2. Mwenzi mmoja anataka kutawala uhusiano ili mahitaji ya wengine hayafikiwi.
3. Kukosekana kwa maelewano.
4. Mshiriki mmoja anatoka nje ya ndoa ili "kurekebisha" matatizo.
5. Kuvunjika kwa mawasiliano.
6. Kuchanganyikiwa kuhusu majukumu ya kila mmoja katika ndoa.
7. Ponogirafia.
8. Udanganyifu.
9. Kutokubaliana kuhusu mitindo wa ulezi.
10. Uraibu.

Wakati wanandoa wanapotambua ishara hizi za onyo, ni busara kutafuta ushauri wa kiungu. Hata hivyo, sio ushauri wote unaojionyesha kuwa wa "Ukristo" unategemea ukweli wa Neno la Mungu. Marafiki na familia wanaweza kuwa na nia njema, lakini wanaweza kutoa suluhisho lisilo la maandiko ambalo litaleta mhchanganyiko na kusababisha tatizo kuwa na mbaya zaidi. Mshauri anapaswa kuchaguliwa kulingana na falsafa yake na kuzingatia Maandiko kama msingi wa afya ya kihisia. Hadithi nyingi za kutisha zimekuja kutoka kwa watu ambao walitafuta ushauri kutoka kwa wale waliowaamini, na kupata kwamba ni "mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo" (Mathayo 7:15) ambao wamekubalia dhambi na kumwambia yule aliykosewa "kuiyeweka katika kaburi la sahaulifu."

Maswali machache katika mahojiano ya mwanzo mwanzo yanaweza kuondoa baadhi ya hawa"mbwa mwitu" kabla ya wakati na fedha ziharibiwe. Wanandoa wanaowachunguza washauri wanapaswa kuzingatia yafuatayo:

1. Mshauri alipata wapi mafunzo au cheti? Kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba utapokea tiba ya kibiblia ikiwa mshauri amefundishwa kupitia mpango wa ushauri wa Kikristo badala ya shirika la kidunia au chuo kikuu. Cheti cha taifa hakina uhakika utapata shauri bora. Ushauri bora wa maandiko unaweza kupatikana kupitia wachungaji wa ndani, washauri wa kujitolea, na makundi ya msaada.

2. Je, mshauri huyu ana uzoefu katika kushughulika na masuala fulani yanayohusika? Maswali machache muhimu kama vile, "Mtazamo wako kwa uraibu wa ponogirafia?" itakusaidia kuamua kama unakubaliana na mtazamo wa mshauri huu.

3. Je! Unakubaliana na falsafa hii ya mshauri na / au ushirikiano wa kidini? Kuna madhehebu na dini ambazo hubeba bendera ya "Kikristo" lakini inaweza kuwa mbali sana na mfumo wa imani ya wanandoa ili waweze kufaidika na ushauri. Kuchagua mshauri kutoka ndani ya mfumo wa dini ya wanandoa unaweza kufanya ushauri huo kuwa wa ufanisi zaidi.

Hakuna kitu ambacho kinaweza kutoa ahadi kamili, lakini kuzingatia maswali hayo kunaweza kusaidia kujucha nyanja. Mungu anaunga mkono ndoa; Yeye huchukia talaka (Malaki 2:16). Hatua ya kwanza wanandoa wanapaswa kuchukua ni kumwomba Mungu awaongoze kwa mshauri mzuri. Inaweza kuchukua uchunguzi kidogo, lakini kutafuta mshauri ambaye anaweza kuleta hekima ya Mungu kwa ndoa yenye mgogoro ni jitihada zinazofaa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wanandoa Wakristo wanapaswa kutafuta ushauri wa ndoa wakati gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries