settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Wakristo wanapinga usawa katika ndoa?

Jibu


"Usawa wa ndoa" ni maneno yanayotumika katika ndoa ya mashoga / mjadala wa ndoa za jinsia moja katika baadhi ya nchi. Neno "usawa wa ndoa" ni jaribio la kutafakari tena mazungumzo na kusingizia ukosefu wa hekima kwa wale wanaopinga ndoa za jinsia moja. Kupinga kutambuliwa kwa fungamano ya ushoga kama ndoa ni jambo moja. Lakini ni ngumu zaidi kupinga "usawa" katika haki za ndoa. Hata hivyo, kuzindua lebo mpya kwa mjadala haibadilishii masuala ya msingi katika mjadiliano huu. Ikiwa "usawa wa ndoa" inamaanisha "ndoa ya mashoga," Wakristo wanapaswa kupinga.

Kwa nini Wakristo wanapinga usawa wa ndoa? Swali yenyewe ni ya kupotosha. Sio Wakristo wote wanaopinga usawa wa ndoa, ndoa ya mashoga. Wakristo wengi wanaunga mkono kutambuliwa kisheria kama ndoa hizo fungamano za mashoga. Wakristo hao kwa ujumla wanasisitiza kwamba maadili ya ngono haipaswi kuwa sheria na kwamba, katika jamii huru, watu wanapaswa kuolewa na yeyote wanaotaka.Katika Biblia, hii ni kosa kubwa.

Biblia imeweka wazi kwamba ushoga ni dhambi isiyo ya kawaida (Mambo ya Walawi 18:22, Warumi 1: 26-27; 1 Wakorintho 6: 9). Biblia inaonyesha ndoa kama uvumbuzi wa Mungu, na Mungu ameielezea kuwa ni agano kati ya mwanaume na mwanamke kwa maisha yao yote (Mwanzo 2:24, 1 Wakorintho 7: 2-16; Waefeso 5: 23-33). Katika Biblia, ushirika wa ushoga sio ndoa. Haijalishi ikiwa serikali inaruhusu ufafanuzi mpya wa ndoa. Haijalishi ikiwa jamii inaunga mkono ndoa ya jinsia moja. Uhusiano wa ushoga daima umekuwa, na daima utakuwa, upotovu wa uumbaji wa Mungu.

Katika jamii za kisasa ambazo zinazidi kuwa za kidunia na zisizo za Kikristo, mjadala wa usawa wa ndoa hatimaye utafanikishwa na harakati za haki za mashoga. Ikiwa hakutakua na toba ya kitaifa na uamsho wa imani ya Kikristo, vyama vya mashoga vitatambuliwa rasmi kama ndoa halali, na haki zote na marupurupu yanayohusiana na hayo. Lakini, haijalishi kila jamii inachofanya , haiwezi kubadili ukweli kwamba wafuasi wa Kristo wanapaswa kujiunga na, na kunyenyekea kwa Neno Lake. Na Neno lake linasema bila shaka kwamba ndoa ni kati ya mmwanaume mmoja na mwanamke mmoja. Kama Wakristo, tunakubali ukweli kwamba tunaishi katika mataifa ya kidunia na ya wasiomcha Mungu, lakini tunathamini Neno la Mungu lisilobadilika kuliko mambo ya jamii. "... Mungu na awe wa kweli, na kila mwanadamu ni mwongo ..." (Warumi 3: 4).

Wakristo hawana haja ya kupigana mashoshoga wanaopewa fungamano za kiraia na faida za serikali ambazo fungamano hizo hutoa. Mapumziko ya kodi, haki za urithi, haki za kutembelea hospitali, nk, haziingiliwi katika Biblia. Lakini, katika ufafanuzi wa ndoa, Wakristo wanapaswa kusimama imara. Mungu aliumba ndoa. Hakuna mwanadamu aliye na haki au mamlaka ya kubadilisha maana ya ndoa. Haijalishi mambo yale serikali na jamii zinaiidhinisha, fungamano za ushoga hazitakuwa na usawa na ndoa kati ya mwanaume na mwanamke

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Wakristo wanapinga usawa katika ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries