settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini juu ya urefu wa nywele? Je wanaume wanapaswa kuwa na nywele fupi, na wanawake wanapaswa kuwa na nywele ndefu?

Jibu


Kifungu kinachozungumzia urefu wa nywele katika Agano Jipya ni 1 Wakorintho 11: 3-15. Kanisa la Korintho lilikuwa katikati ya mjadala juu ya majukumu ya wanaume na wanawake na utaratibu sahihi wa mamlaka ndani ya kanisa. Katika jamii ya Wakorintho, wanawake walionyesha kuwaheshimu waume zao kwa kuvaa pazia. Inaonekana kwamba baadhi ya wanawake katika kanisa walikuwa wakiondoa vazia zao, kitu ambacho maasherati wa hekalu pekee au wanawake wengine waasi waliyofanya. Kwa mwanamke kuja kanisani bila ya pazia yake ingekuwa kudharau mumewe, na pia ilionekana kuwa kuchanganyikiwa kwa kiutamaduni. Kwa ishara hiyo, kwa mwanaume kuvaa pazia au kwa namna fulani kufunika kichwa chake wakati wa ibada haikubalika kiutamaduni huko Korintho.

Paulo anaisihi biolojia kuelezea yafaayo katika kufuata viwango vya kitamaduni: wanawake kwa kawaida wana nywele ndefu zaidi kuliko wanaume, na wanaume hukabiliwa na hali ya upara. Hiyo ni kwamba, Mungu aliwaumba wanawake wenye "pazia la asili" na wanaume wenye kichwa "wazi."Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe. (mstari wa 6). Anachosema ni kwamba kama utamaduni unasema mwanamke hapaswi kuwa kipara(bila pazia ya asili), basi kwa nini angekataa kiwango hicho cha utamaduni cha kuvaa pazia (bila pazia yake ya asili)?

Kwa upande mwingine, sio kawaida kwa mwanamume kuwa na "nywele ndefu" (mstari wa 14). Nywele zake ni za kawaida (na nyembamba) kuliko ya mwanamke. Hii inaambatana na mila ya Wakorintho ya wanaume kutovaa pazia wakati wa ibada. Paulo anahimiza kanisa kufuata maoni ya kawaida ya maumbile ya wanaume na wanawake.

Basi urefu wa nywele sio msingi kuu wa kifungu hiki cha Maandiko. Tunapata maagizo yafuatayo kutoka kwake: 1) Tunapaswa kuzingatia viashiria vya utamaduni vinavyokubalika vya jinsia. Wanaume wanapaswa kukaa kama wanaume, na wanawake wanapaswa kukaa kama wanawake. Mungu hakubali mchanganyiko wajinsia mbili 2) Hatupaswi kuasi dhidi ya utamaduni tu kwa sababu ya kuasi, kwa kusingizia "uhuru" wa Kikristo. Inafaa tujali jinsi tunavyojionyesha wenyewe . 3) Wanawake wanapaswa kujitolea wenyewe chini ya mamlaka ya uongozi wa kiume wa kanisa. 4) Hatupaswi kugeuza majukumu ya Mungu ya wanaume na wanawake.

Utamaduni wetu leo haitumii pazia au kufunika kichwa ili kuonyesha heshima kwa mamlaka. Majukumu ya wanaume na wanawake hayajabadilika, lakini jinsi tunavyotekeleza majukumu hayo hutegemea na utamaduni. Badala ya kuweka viwango vya kisheria vya urefu wa nywele, tunapaswa kukumbuka kuwa suala la kweli ni hali ya moyo wetu, mwitikio wetu binafsi kwa mamlaka ya Mungu, amri yake iliyowekwa, na uchaguzi wetu wa kunyenyekea mbele ya mamlaka hayo. Wanaume na wanawake wana majukumu tofauti, na sehemu ya tofauti hiyo inaonyeshwa kwa nywele zao. Nywele za mwanamume zinapaswa kuonekana kuwa kiume. Nywele za mwanamke zinapaswa kuonekana kama kike.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya urefu wa nywele? Je wanaume wanapaswa kuwa na nywele fupi, na wanawake wanapaswa kuwa na nywele ndefu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries