settings icon
share icon
Swali

Ni urafik upi wa kweli kulingana na Biblia?

Jibu


Bwana Yesu Kristo alitupa ufafanuzi wa rafiki wa kweli: " Hakuna upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya marafiki zake .Ninyi mmekuwa marafiki zangu, mkitenda niwaamuriyo. Siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake, bali nimewaita marafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu "(Yohana 15: 13-15). Yesu ni mfano mkuu wa rafiki wa kweli, kwa kuwa alitoa uhai wake kwa ajili ya "marafiki" Wake. Pia, mtu yeyote anaweza kuwa rafiki Yake kwa kumtegemea kama mwokozi wake binafsi, akizaliwa tena na kupokea maisha mapya ndani Yake.

Kuna mfano wa urafiki wa kweli kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli, ambaye, licha ya kumfuatia Daudi baba yake na kujaribu kumwua, alisimama na rafiki yake. Utapata hadithi hiyo katika 1 Samweli sura ya 18 hadi sura ya 20. Baadhi ya vifungu muhimu ni 1 Samweli 18: 1-4; 19: 4-7; 20: 11-17, 41-42.

Kitabu cha Mithali pia kinaelezea hekima kuhusu marafiki. "Rafiki hupendasiku zote; na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu" (Mithali 17:17). " Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe;, lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu" (Methali 18:24). Suala hapa ni kwamba ili uwe na rafiki, lazima awe rafiki. "Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana (Mithali 27: 6). "Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake" (Mithali 27:17).

Kanuni ya urafiki pia inapatikana katika Amosi. "Je! Wawili wanaweza kutembea pamoja, isipokuwa walikubaliana?" (Amosi 3: 3). Marafiki huwa na fikra sawa. Rafiki ni mtu ambaye unamwaini na unaweza kumwambia jambo kwa uaminifu kamili. Rafiki ni mtu unayemheshimu na anayekuheshimu, sio kwa msingi wa kustahili lakini kulingana na usawa wa fikra.

Hatimaye, ufafanuzi halisi wa rafiki wa kweli unatoka kwa mtume Paulo: "Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu alionyesha upendo wake mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi "(Warumi 5: 7-8). "Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake" (Yohana 15:13). Sasa, huo ni urafiki wa kweli!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni urafik upi wa kweli kulingana na Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries