settings icon
share icon
Swali

Je! ina maana gani kuwa upendo wa wengi utapoa (Mathayo 24:12)

Jibu


Yesu alitabiri kuwa upendo wa wengi utapoa kama sehemu ya jibu lake kwa wanafunzi wake, “Ni nini itakua ishara kukuja kwake, na mwisho wa dunia?” katika Mathayo 24 katika hotuba yake katika mlima wa mizeituni, Yesu anaelezea mwisho wa duni ambao utatangulia ujio wake mara ya pili. Anasema kwamba kutakuweko na kristo wa uwongo (Mathayo 24:5), vita (Mathayo 24:6), ugomvi na majanga ya asili (Mathayo 24:7).

Yesu pia alionya dhidi ya kuteswa kwa waumini, ambapo baadhi watathibitisha kuwa wanafunzi wa uwongo ambao watawageukia wenzao (Mathayo 24:9-10). “Na,” Yesu akasema, “Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa” (Mathayo 24:12). Iwe ni kwa sababu ya udanganyifu shawishi wa walimu wa uwongo au mateso, au hofu ya kufa, bidii ya wasomi wengi wa uwongo itadidimia. Upendo wao kwa Mungu na kwa kanisa “utapoa.” Wakristo wa kweli, hata wale ambao imani yao ni hafifu, watavumilia hadi mwisho (Mathayo 24:13). Kunao upendo wa kweli ambao ni tunda la Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22), na hauwezi didimia (1 Wakorintho 13:7). Upendo wa kweli hauwezi kupoa kwa sababu umedumishwa na Kristo ambaye anaweza kutukinga dhidi ya kuanguka (Yuda 1:24).

Kwa wale wasio na Roho Mtakatifu, hata hivyo ule upendo walio nao utapoa na kupoa sana katika siku za mwisho. Paulo anapanua hoja hii katika 2 Timotheo 3:1-4 wakati anapoelezea siku za mwisho. Upendo hao watu watakuwa nao hautokuwa moto, upendo ulio hai kwa Mungu na kweli Yake na kwa watu Wake. Badala yake, ni upendo wa kibinafsi na upendo wa pesa (aya ya 2). Paulo anawaelezea wale ambao upendo wao kwa Mungu, Kristo na watakatifu kuwa ni wa unafiki, na sio upendo halisi. Wanafanya yote wayafanyo kwa misingi ya dini ili wao wenyewe wapate tunuku. Hawafanyi chochote kwa ajili ya utukufu wa Mungu, heshima ya Kristo, au mema kwa ajili ya wengine.

Je! tunawezaje kuwa na uhakika kwamba upendo tulio nao kwa Kristo hautapoa? Tunaanza kwa kujichunguza ili tuwe na uhakika kwamba tuko katika imani (2 Wakorintho 13:5). Ikiwa sisi ni wa Yesu, tunaweza kuwa na ujasiri kuwa tunamiliki upendo kutoka kwa Roho Mtakatifu ambao hautapoa kamwe. Kwa hivyo lazima tufanye juhudi za kuongeza upendo wetu: “Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu” (Wafilipi 1:9-11).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! ina maana gani kuwa upendo wa wengi utapoa (Mathayo 24:12)
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries