settings icon
share icon
Swali

Upendo wa Kristo ni nini?

Jibu


Maneno "upendo wa Kristo," kinyume na "upendo kwa Kristo," ina maana ya upendo aliyo nao kwa wanadamu. Upendo wake unaweza kuelezewa kwa ufupi kama nia yake ya kutenda kwa maslahi yetu bora, hasa katika kukidhi mahitaji yetu makubwa, hata ingawa ilimupa kila kitu na hata ingawa hatukustahili kabisa upendo huo.

Ijapokuwa Kristo Yesu, akiwa Mungu katika asili, alikuwepo mwanzo wa wakati na Mungu Baba (Yohana 1: 1) na Roho Mtakatifu, kwa hiari aliacha kiti chake cha enzi (Yohana 1: 1-14) kuwa mtu, kwamba Yeye aweza kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu ili tusiweze kulipa milele katika ziwa la moto (Ufunuo 20: 11-15). Kwa sababu dhambi ya wanadamu imelipwa na Mwokozi wetu asiye na dhambi Yesu Kristo, Mungu ambaye ni mwenye haki na mtakatifu anaweza sasa kusamehe dhambi zetu tunapokubali malipo ya Kristo Yesu kama yetu (Warumi 3: 21-26). Hivyo, upendo wa Kristo unaonyeshwa katika kuondoka kwake nyumbani mbinguni, ambako aliabudiwa na kuheshimiwa kama alivyostahili, kuja duniani kama mtu ambako angekejeliwa, kusalitiwa, kupigwa, na kusulubiwa msalabani kulipa adhabu kwa dhambi zetu, kufufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu. Aliona haja yetu ya Mwokozi kutoka kwa dhambi zetu na adhabu yake kama muhimu zaidi kuliko faraja na maisha yake mwenyewe (Wafilipi 2: 3-8).

Wakati mwingine watu wanaweza kutoa maisha yao kwa hiari kwa wale wanaoona kuwa wanastahili rafiki, jamaa, watu wengine "wema" — lakini upendo wa Kristo unaendelea zaidi ya hayo. Upendo wa Kristo huzidisha hadi kwa wale ambao hawastahili. Kwa hiari alichukua adhabu ya wale waliomtesa Yeye, waliomchukia, waliomwasi, na hawakujali chochote juu yake, wale ambao hawakusistahili zaidi ya upendo Wake (Warumi 5: 6-8). Aliwapa zaidi aliyoweza kuwapatia wale ambao walistahili kwa uchache! Basi dhabihu ni msingi wa upendo wa kimungu, unaitwa upendo wa agape. Huu ni upendo wa Mungu, sio upendo wa kibinadamu (Mathayo 5: 43-48).

Upendo huu aliouonyesha kwetu msalabani ni mwanzo tu. Tunapoweka imani yetu kwake kama Mwokozi wetu, Yeye hutufanya watoto wa Mungu, warithi pamoja naye! Anakuja kukaa ndani yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu wake, akiahidi kwamba hatatuacha au kutusahu (Waebrania 13: 5-6). Hivyo, tuna rafiki mzuri wa maisha. Na bila kujali tunayopitia, Yeye yuko pale, na upendo wake unapatikana kwa sisi (Warumi 8:35). Lakini Yeye anatawala kwa haki kama Mfalme mwenye huruma mbinguni, tunahitaji kumpa nafasi anayostahili katika maisha yetu pia, ya Mwalimu na sio tu rafiki. Ni wakati tu kwamba tutapata maisha kama alivyotaka na kuishi katika ukamilifu wa upendo wake (Yohana 10: 10b).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Upendo wa Kristo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries