settings icon
share icon
Swali

Je! Upendo wa eros ni nini?

Jibu


Lugha ya Kiyunani inatumia maneno tofauti kueleza maana mbalimbali ya "upendo." Neno moja ni eros, neno linalotumiwa kuonyesha upendo wa kijinsia au hisia za kutia ashiki ambazo zinashirikiwa kati ya watu ambao wanavutiwa kimwili wao wenyewe. Kwa nyakati za Agano Jipya, neno hili lilikuja kushushwa hadhi sana na utamaduni kwamba halitumiwi hata mara moja katika Agano Jipya nzima.

Neno lingine la Kiyunani kwa upendo ni phileo. Neno hili linazungumzia zaidi upendo wa kusisimua kati ya familia au marafiki. Kwa kuwa eros unahusishwa kwa karibu sana na ashiki, phileo unaweza uhusishwa zaidi na hisia au moyo (kuzungumza kisitiari). Tunahisi upendo kwa marafiki na familia zetu, kwa kawaida sio katika dhana ya eros, bali upendo ambao unatutia sisi motisha kutaka kuwatendea kwa unyenyekefu na kuwasaidia ili wafanikiwe. Hata hivyo, phileo haisiwi kati ya watu ambao wana chuki kati yao. Tunaweza hisi upendo wa phileo kuelekea marafiki na familia lakini si kwa watu ambao hatupendi au kuwachukia.

Tofauti na haya yote mawili ni neno la tatu la Kigiriki kwa upendo, agapao, linalofafanuliwa kwa kufanana hasa kama "upendo wa kujitolea." Ni upendo ambao unawasogeza watu kwa hatua na unaangalia ustawi wa wengine, bila kujali gharama ya kibinafsi. Kuzungumza Kibiblia, agapao ni upendo ambao Mungu aliwaonyesha watu wake kwa kumtuma Mwanawe, Yesu, kufa kwa ajili ya dhambi zao. Ni upendo ambao unaozingatia mapenzi, sio hisia au ashiki. Huu ndio upendo ambao Yesu anawaagiza wanafunzi wake waonyeshe kwa maadui zao (Luka 6:35). Eros na phileo hazionyeshwi kwa watu ambao wanatuchukia na kututakia mabaya; lakini agapao huonyeshwa. Katika Warumi 5:8, Paulo anatuambia kwamba upendo wa Mungu kwa watu Wake yalifanywa dhahiri kwa kuwa "tulipokuwa bado wenye dhambi [yaani, maadui], Kristo alikufa kwa ajili yetu."

Kwa hivyo kuhamia kutoka msingi hadi safi, tuna eros, phileo, na agapao. Hii sio kupaka matope eros kama dhambi au unajisi. Upendo wa kijinsia sio asili unajisi au uovu. Badala yake, ni zawadi ya Mungu kwa wanandoa kuonyesha upendo wao kati yao, kuimarisha kuunganishwa kati yao, na kuhakikisha kuishi kwa mbio za binadamu. Biblia hutoa kitabu kimoja chote kwa baraka za upendo wa ashiki, au kijinsia, na upendo-Wimbo Ulio Bora. Upendo kati ya mume na mke lazima uwe, kati ya vitu vingine, upendo wa ashiki. Hata hivyo, uhusiano wa muda mrefu ulio msingi tu juu ya upendo wa ashiki umehukumiwa kushindwa. 'Msisimko' wa upendo wa kijinsia unaisha haraka ijapokuwa kuna phileo au agapao kwenda pamoja nayo.

Kinyume chake, wakati hakuna kitu chochote kiasili ni dhambi na upendo wa ashiki, iko katika nyanja hii ya upendo kwamba asili yetu ya dhambi inafanywa wazi zaidi kwa sababu ya kimsingi ya kuzingatia nafsi, hili hali phileo na agapao huzingatia wengine. Fikiria kile Mtume Paulo anaambia kanisa la Kolosai: "Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu" (Wakolosai 3:5). Neno la Kiyunani kwa "uasherati wa kijinsia" (porneia) kimsingi linahusu upeo wa dhambi ya kijinsia (uzinzi, uasherati, ushoga, ukatili, nk).

Wakati inashirikishwa kati ya mume na mke, upendo wa ashiki unaweza kuwa jambo la ajabu, lakini kwa sababu ya asili yetu ya dhambi iliyoanguka, mara nyingi eros inakuwa porneia. Wakati hili linatokea, wanadamu wanaelekea kupita kiasi, na kuwa labda wa kujinyima anasa za mwili au muumini wa Imani kuwa anasa ni kitu muhimu. Wa kujinyima anasa ni mtu anayejaribu kukwepa kabisa upendo wa kijinsia kwa sababu ya ushirika wake na uasherati huifanya kuonekana uovu na kwa hivyo lazima uepukwe. Muumini wa Imani kuwa anasa ni kitu muhimu ni mtu ambaye anaona upendo wa kijinsia bila kuzuia kama asili kamilifu. Kama ilivyo kawaida, mtazamo wa kibiblia unaonekana katika usawa kati ya mambo haya mawili makubwa ya dhambi. Ndani ya unganishwi wa ndoa ya kuvutiwa na mtu wa jinsi tafauti, Mungu anasherehekea uzuri wa upendo wa kijinsia: "Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, akayale matunda yake mazuri. Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi, nachuma manemane yangu na rihani, nala sega la asali na asali yangu, naywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, naam, nyweni sana, wapendwa wangu"(Wimbo Ulio Bora 4:16, 5:1). Lakini nje ya ndoa ya kibiblia, eros inakuwa potofu na dhambi.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Upendo wa eros ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries