settings icon
share icon
Swali

Je, upatanisho wa Kristo ni usio na mpaka?

Jibu


Biblia ina mengi ya kusema juu ya upatanisho wa Kristo. Swali tunalouliza ni ikiwa thabihu Yake ilitoa upatanisho ulio na mpaka au usio na mpaka. Neno upatanisho linamaanisha "kuridhika au malipo ya kosa au jeraha; kurekebisha." Fundisho la upatanisho usio na mpaka linasema kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya watu wote, ikiwa wangemwamini au la. Tunaporejelea kwa kazi ya Yesu iliyokamilika msalabani, upatanisho unahusu uridhiano wa Mungu na mwanadamu kama ilivyotimizwa kupitia mateso na kifo cha Kristo. Paulo anaangazia kazi ya yesu upatanisho anaposema, "Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake!" (Warumi 5:8-10).

Jinsi fidia hii ya makosa au upatanisho ulivyotekelezwa na kile kilichohusika, imekuwa ikijadiliwa na wanatheolojia kwa karne nyingi. Kuna angalau hali tisa tofauti za upatanisho wa Kristo; kwamba upatanisho ni mfano mzuri kwetu (nadharia ya mfano wa Maadili), kwamba ni uamuzi badala wa kisheria (dadharia ya adhabu badala ).

Lakini labda mjadala wenye utata zaidi kuhusu upatanisho wa Yesu unazingatia unaofahamika kuwa upatanisho "ulio na mpaka" au "dhahiri". Kambi moja ya kitheolojia (inayojumuisha wale wanaoshikilia mafundisho yake Jacobus Arminius na John Wesley) wanaamini kwamba Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya wale wote watawahi kuishi. Kambi nyigine ya kitheolojia -inayojumiusha wanatheolojia wenye mageuzi, ambao mara nyingi wanaitwa "Wakalvini" waliokuwepo baada ya John Calvin aliyebadilika- wanasema kwamba Yesu alikufa tu kwa ajili ya wale waliochaguliwa na Baba tangu kuumbwa kwa ulimwengu ili kuokolewa. Kikundi hiki cha watu waliokombolewa mara nyingi hufahamika kama "wateule" au "waliochagukiwa" na Mungu. Je, ni msimamo mgani ulio sawa? Je, Yesu alikufa kwa ajili ya kila mtu ulimwenguni au tu kwa ajili ya kikundi fulani cha watu?

Je, kila mtu ataokolewa?
Tunapochunguza suala hili, swali la kwanza tunalouliza ni hili:Je, kila mtu ataokolewa kupitia kazi ya upatanisho ya Yesu? Wale ambao wanaoshikilia mtazamo huo wa watu wote wanasema "ndio."

Watu wa ulimwengu wanasema kwamba, kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili ya kila mtu na dhambi zote za wanadamu alizibeba Kristo, kila mtu ataishi milele na Mungu.

Hata hivyo, Maandiko yanapinga mafundisho hayo (ambayo yalianzishwa na mwalimu aliyeitwa Laelius Socinus katika karne ya kumi na sita). Biblia inaweka wazi kwamba watu wengi watapotea, na mistari ya Biblia inayoangazia ukweli huu inafuata:

• "Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele" (Danieli 12:2)

• "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache"(Mathayo 7:13-14)

• "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mathayo 7:22-23)

• "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele" (Mathayo 25:46)

• "Watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake" (2 Wathesolanike 1:9)

• "Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto"(Ufunuo 20:15)

Kwa kuwa sio kila mtu ataokolewa, tunapaswa kuelewa ukweli kwamba: upatanisho wa Kristo una mpaka. Basi kama sivyo, fundisho la ulimwenguni kote ni la kweli, na bado Maandiko yanafundisha wazi kuwa sio kila mtu atakayeokolewa. Kwa hivyo isipokuwa mtu anashikilia fundisho la ulimwengu na anaweza kushinda uthibitisho wa Biblia kama ilivyoelezwa hapo juu, basi mtu lazima aamini katika upatanisho ulio na mpaka.

Jinsi gani upatansho ukawa wenye mpaka?
Swali muhimu la kuchunguza ni hili: Ikiwa upatanisho una mpaka (na una mpaka), una mpaka vipi? Maneno maarufu ya Yesu katika Yohana 3:16 yanatoa jibu la swali hilo: " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Katika kifungu hiki, hali ya lazima inayoweka mpaka wa upatanisho inapatikana: "yeyote atakayeamini" (kwa Kiyuani: " wote waaminiye"). Katika maneno mengine, upatanisho una mpaka kwa wote wanaoamini na wote wanaoamini tu.

Je, nani huweka mipaka ya uptanisho?
Waarmenia na Wakalvini hawakubaliani na hoja hii-upatanisho wa Kristo una mipaka katika wale wanaoamini. Kutokubaliana kunatokea juu ya swali linalofuata: je, ni nani huweka mipaka ya upatansho-Mungu au mwanadamu? Wakalvini wanashikilia kwamba Mungu huweka mpaka wa upatanisho kwa kuchagua wale atakaowaokoa, na kwa hivyo Mungu alimfanya Kristo kutwaa dhambi za wale aliowachagua wapate kuokoka. Msimamo wa Waarmenia na Wesley unasema kwamba Mungu haweki mipaka katika malipo ya Kristo ya dhambi lakini ni mwanadamu ambaye huweka mpaka wa upatanisho kwa kuchagua kwa hiari kukubali au kukataa toleo ambalo Mungu hutoa la wokovu.

Wanatheolojia wa Waarmenia na Wesley kwa kawaida hutoa msimamo wa kwamba upatanisho hauna mpaka katika mwaliko wake lakini una mipaka katika matumizi yake. Mungu hutoa mwaliko kwa wote; hata hivyo, ni wale tu huitikia injili kwa imani ambao kazi ya upatanisho hufanyika kwa hali yao ya kiroho.

Ili kuunga mkono msimamo kwamba ni mwanadamu na sio Mungu anayeweka mpaka wa upatanisho, Waarmenia na Wesley wanaorodhesha vifungu kadhaa vya maandiko, pamoja na yafuatayo:

• "Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote (I Yohana 2:2, kusisitizwa kumeongezwa).

• "Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29, kusisitizwa kumeongezwa)

• "Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu" (Yohana 6:51, kusisitizwa kumeongezwa)

• "Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu" (Yohana 12:32, kusisitizwa kumeongezwa)

• "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake" (1 Timotheo 2:5–6, kusisitizwa kumeongezwa)

• "Ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu" (Waebrania 2:9, kusisitizwa kumeongezwa)

• "Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia " (2 Petero 2:1, kusisitizwa kumeongezwa)

Kwa kuongezea marejeleo ya Biblia hapo juu, wanatheolojia Waarmenia na Wesley hutoa hoja kadhaa zenye mantiki za kuunga mkono kesi yao. Inayojulikana sana ni kwamba, ikiwa Mungu ni mwenye upendo wote, mbona Kristo hakufa kwa ajili ya kila mtu? Je, Mungu anapenda kila mtu (tazama Yohana 3:16)? Wanachukulia upatanisho ambao umewekwa mipaka na Mungu kama kukana Mungu ni asiye na mwisho.

Zaidi ya hayo, Waarmenia/Wesley huamini kwamba upatanisho uliowekwa mipaka na Mungu ni mbaya kwa ujumbe wa injili. Je, mwinjilisti anawezaje kuubiri kwamba "Kristo alikufa kwa ajili yako" ikiwa Kristo hakufa kwa ajili ya watu wote? Wanasema mwinjilisti hana uhakika anapoambia mtu kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya mtu huyo kwa sababu mwinjilisti huyo hana wazo halisi kama ndivyo ilivyo (ikiwa upatanisho umewekwa mpaka na Mungu).

Upatanisho usio na mpaka-hitimisho
Isipokuwa mtu ni wa ulimwengu na anaamini kwamba kila mtu ataokolewa mwishowe, Mkristo lazima awe na imani katika upatanisho wenye mwisho. Sehemu muhimu ya ugomvi ni kuhusu ambaye anaweka mpaka katika upatanisho-Mungu au mwanadamu. Wale ambao wanaamini kwamba Mungu huweka mpaka katika upatanisho wanapaswa kujibu hoja za Biblia zilizotolewa na wale wanaoamini katika upatanisho uliowekwa mpaka na binadamu, na pia waeleze jinsi Mungu anavyoweza kuelezwa katika Maandiko kwamba anapenda watu wote lakini bado Mwanaye asife kwa ajili ya wote.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, upatanisho wa Kristo ni usio na mpaka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries