settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu aina za kudumu za kupanga uzazi kama vile kuweka mipira au kutoa nguvu za kiume?

Jibu


Kupanga uzazi linaweza kuwa suala la utata miongoni mwa Wakristo kwa sababu Biblia haikubali au kuhukumu matumizi yake. Pia Biblia haifafanui juu ya njia za kupanga uzazi za kudumu kama vile kuweka mipira au kutoa nguvu za kiume, taratibu hizi hazikujulikana wakati wa Biblia. Kupanga uzazi, ya kudumu au vinginevyo, ni suala la moyo na imani ya mume na mke.

Katika majadiliano yoyote juu ya kupanga uzazi wa kudumu , lazima tuelewe kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu (Zaburi 127: 3-5). Watoto si mizigo ya kubeba lakini baraka za kupokea kwa furaha. Kutoka kwa mtazamo furaha wa kibiblia, kila wanandoa wanapaswa "kutarajia" kuwa na watoto na angalau kuwa tayari kwa uwezekano huo. Kutokuwa na uwezo wa kuwa na watoto ilikuwa inachukuliwa kuwa laana katika nyakati za kale, na uwezo wa kupata furaha. Hakuna mtu yeyote katika Biblia aliyerekebishwa kuwa hajui kuhusu kuzaa watoto.

Upangaji uzazi wa kudumu (yaani, kutoa nguvu za kiume au kuweka mipira) inaweza kuwa sahihi kwa wanandoa wengine ambao huhisi wasiwe na watoto zaidi. Kunaweza kuwa na masuala ya afya, fedha, au uhusiano ya kuzingatia. Uamuzi wa kutumia upangaji wa uzazi wa kudumu haupaswi kuzingatia ubinafsi au ubatili (Wafilipi 2: 3-4) lakini kwa hamu ya kumpendeza Mungu na kufuata mapenzi Yake.

Watu wengi huhisi tunapaswa kuwa na watoto tu kama tunataka kupokea baraka zote za Mungu na kwamba hatupaswi kupunguza ukubwa wa familia kwa njia ya kupanga uzazi wa kudumu. Hata hivyo, kwa sababu Biblia haizuii upangaji wa uzazi, kwa muda mfupi au wa kudumu, hatuwezi kusema kuwa ni sawa katika hali zote. Kupitia mahusiano yetu binafsi na Mungu, tunaweza kutafuta mapenzi ya Mungu kuamua ukubwa wa familia zetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu aina za kudumu za kupanga uzazi kama vile kuweka mipira au kutoa nguvu za kiume?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries