settings icon
share icon
Swali

Je! Ni mfano upi wa kibiblia wa uongozi wa Kanisa?

Jibu


Kuna mfano tofauti wa uongozi wa Kanisa katika Agano Jipya, ijapokuwa mfano huo unaonekana kupuuswa badala kuelezewa kwa uhalisi. Agano Jipya linataja idara mbili za kanisa: mashemasi na wazee (ambao pia wanaitwa wachungaji au waangalizi).

Maneno mwangalizi (wakati mwingine hutafsiriwa "kasisi"), kasisi (ambalo linaweza kutafsiriwa "mchungaji"), na mwangalizi (wakati mwingine hutafsiriwa "askofu") hutumiwa kwa mkabala katika Agano Jipya. Ingawa maneno haya mara nyingi humaanisha mambo tofauti kati ya makanisa mbalimbali hii leo, Agano Jipya linaonekana kuashiria ofisi moja, ambayo ilichukuliwa na wanaume kadhaa ambao wanamcha Mungu ndani ya kila kanisa. Mistari ifuatayo inaonyesha jinsi maneno hayo yanaingiliana na yanatumiwa kwa kubadilikana:

Katika Matendo 20:17-35 Paulo anazungumza na viongozi wa kanisa la Efeso. Hapa wanaitwa "wazee" katika aya ya 17. Katika aya ya 28 anasema, "Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu." Hapa wazee wanaitwa "waangalizi" na kazi yao ya ukasisi/uchungaji zinarejelewa na kanisa linaitwa "kundi."

Katika Tito 1: 5–9, Paulo anatoa sifa za wazee (aya ya 5) na anasema sifa hizi ni muhimu kwa sababu "Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama" (aya ya 7). Katika 1 Timotheo 3: 1-7, Paulo pia anatoa sifa za waangalizi, ambazo ni sawia na sifa za wazee katika Tito. Katika 1 Petro 5: 1-4, Petro anawaambia wazee "lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa." Kutoka kwa vifungu hivi, tunaona kwamba ofisi ya mzee / kasisi-mchungaji / mwangalizi-askofu ni moja. Wale wanaochukua nafasi za ofisi hii wanapaswa kuongoza, kufundisha, na kulichunga kanisa kama vile mchungaji afavyo.

Zaidi ya hayo, tunaona kwamba kila kanisa lina wazee (walio wengi). Wazee wanapaswa kuongoza na kufundisha (1 Timotheo 5:17). Mtindo wa kibiblia ni kwamba kikundi cha wanaume (na wazee kila wakati huwa wanaume) kina jukumu la uongozi wa kiroho na huduma ya kanisa. Hakuna kanisa ambalo limetajwa likiwa na mzee/kasisi mmoja ambaye ndiye anasimamia kila kitu, au kunako tamko la uongozi wa kanisa lote jumla (ijapokuwa kanisa lina sehemu yake maalum).

Huku wazee wakiwa na jukumu la kufundisha na kuongoza kundi, bado kunayo mengi ambayo yanahitaji kufanywa kwa kiwango cha mwili. Ofisi ya shemasi inaangazia mahitaji ya kimwili ya kanisa. Katika Matendo 6, kanisa la Yerusalemu lilikuwa likikidhi mahitaji ya kimwili ya watu wengi kanisani kwa kuwapa chakula. Baadhi ya wajane walikuja kwa mitume kwa sababu hawakupata kile walichohitaji. Mitume walijibu, "Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya neno la Mungu ili kuhudumu mezani" (Matendo 6: 2). Ili kuwapunguzia mitume kazi, watu waliambiwa "chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, nasi tutatumia muda wetu kuomba na huduma ya neno" (mistari ya Matendo 6: 3-4). Ingawa wanaume waliochaguliwa hapa hawaitwi mashemasi, wasomi wengi wa Biblia wanawaona kama mashemasi wa kwanza, au angalau mfano wa msimamo huo. Neno shemasi linamaanisha "mtumishi." Mashemasi ni wahudumu wa kanisa walioteuliwa ambao huhudumia mahitaji ya kimwili ya kanisa, wakiwasaidia wazee kuhudhuria huduma zaidi ya kiroho. Mashemasi wanapaswa kuwa wakomavu kiroho, na sifa za mashemasi zimetolewa katika 1 Timotheo 3: 8-13.

Kwa kifupi, wazee wanaongoza huku mashemasi wakihudumia. Vitengo hivi haviko haviachani na kila mmoja akiwa peke yake. Wazee huwahudumia watu wao kwa kuwaongoza, kufundisha, kuomba, ushauri n.k.; na mashemasi wanaweza kuongoza wengine katika huduma. Kwa kweli, mashemasi wanaweza kuwa viongozi wa kikundi cha huduma ndani ya kanisa. Bado, kuna tofauti ya kimsingi kati ya wale wanaohusika na uongozi wa kiroho wa kanisa na wale wanaohusika na huduma zingine.

Kwa hivyo, kunisa lenyewe linafaa wapi katika muundo wa uongozi wa kanisa? Katika Matendo 6, ni kanisa lenyewe lililochagua mashemasi, kwa hiyo makanisa mengi hii leo yanaruhusu kanisa lenyewe bila kushawishiwa na linguine kuchagua na kuridhia mashemasi wa kanisa. Na, kwa kweli, washirika wa kanisa wanapaswa kuwa wahudumu wa kwanza kuwa wahubiri na wainjilisti wanaofikia ulimwengu uliopotea. Wazo kwamba kanisa huajiri mhubiri aliyesoma kufanya kazi ya kanisa sio jambo la kibiblia.

Kunaweza kuwa na tofauti za kikanisa za uongozi wa kanisa kwa sababu huu ni mfano tu wa kimsingi; undani haujaelezewa katika Maandiko. Mfumo wa kimsingi unaopatikana katika Agano Jipya ni kwamba kila kanisa linapaswa kuwa na wazee zaidi ya mmoja na wa kiume wanaomcha Mungu ambao wana jukumu la kuongoza na kufundisha kanisa na mashemasi ambao ni wacha Mungu ambao wana jukumu la kuwezesha huduma za kanisa. Wingi wa wazee hukinga kanisa kutokana na udhaifu na uwezekano wa kutumia mamlaka kupita kiasi mzee akiwa mmoja anaweza kuleta. Ili mradi mtindo huu wa kimsingi umefuatwa, kanisa linakuwepo kulingana na muundo wa kibiblia. Kuwa na mchungaji wa pekee anayedhibiti kanisa sio mfano wa kibiblia, wala sio utaratibu ambao kwamba mchungaji anafanya kazi kwa niapa ya mashemasi ambao husimamia huduma ya kanisa. Kanisa linapaswa kufuata mwongozo wa wachungaji wanaomfuata Kristo. Kwa hekima yao, wazee wanaweza kuomba kinisa kuidhinisha maamuzi makuu wanayofanya, lakini kanisa halipaswi kuwa mamlaka ya mwisho. Mambo yote hukoma na wazee / wachungaji / waangalizi, ambao wanawajibika kwa Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni mfano upi wa kibiblia wa uongozi wa Kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries