settings icon
share icon
Swali

Unyakuzi wa kanisa ni nini?

Jibu


Neno “unyakuzi” haliko katika Bibilia. Dhana ya unyakuzi, ingawa yafunzwa wazi katika maandiko. Unyakuzi wa kanisa ni tendo ambalo Mungu anawatoa wakristo wote kutoka ulimwengu ili kutengeza njia ya hukumu yake ya haki ambayo itamwagikia ulimwengu wakati ule wa matezo. Unyakuzi umeelezwa katika 1 Wathesalonike 4: 13-18 na 1 Wakorintho 15:50-54. Mungu atawafufua wakristo wote waliokufa, awape mwili wa utukufu na awachukue kutoka ulimwengu pamoja na wateule walio hai ambao nao pia watapewa mwili wa utukufu wakati huo. “kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo” (1 Wathesalonike 4:16-17).

Unyakuzi ni tukio la ghafla, na tutapokea mwili wa utukufu wakati huo. “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika” (1 Wakorintho 15:51-52). Unyakuzi ni tendo la utukufu ambalo zote tunastahili kulithamani. Hatimaye tutakuwa huru kutoka dhambi. Tutakuwa mbele za Mungu milele. Kuna mjadala juu ya maana ya unyakuzi na vile utakavyo kuwa. Hii sio lengo la Mungu. Bali kuambatana na unyakuzi, Mungu anatutaka “tufarijianeni kwa maneno hayo” (1 Wathesalonike 4:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Unyakuzi wa kanisa ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries