settings icon
share icon
Swali

Je! Unabii wa kibinafsi ni dhana ya kibiblia?

Jibu


Kuna baadhi ndani ya imani ya Kikristo, hasa katika makanisa ya Uponyaji/Kiroho, ambao wanatazama kipawa cha unabii kama kutoa ushauri wa kibinafsi na maonyesho "ndivyo anasema Bwana". Kwa kusikitisha, wale wanaofanya unabii wa kibinafsi kwa namna hii mara nyingi hawana tofauti na wale wanaojionyesha wenyewe kama bingwa wa maono. Kwa kweli, kuna vituo vya kinabii kama njia badala ya "Kikristo" kwa vituo vya ubingwa wa maono. Wengine katika harakati za unabii wa kibinafsi hutangaza kwa kauli kama vile "kuja upate usomaji wa unabii wako"; hii ni sawa na kutumia neno ubingwa wa maono. Utendaji huu wa kipawa cha unabii sio wa kibiblia kabisa.

Kuongea Kibiblia, kipawa cha unabii ni uwezesho wa Roho kuweza kutangaza ufunuo kutoka kwa Mungu (Warumi 12:6-8; 1 Wakorintho 12:4-11, 28). Unabii wakati mwingine, lakini sio kila wakati, unahusisha kutangaza ufunuo kutoka kwa Mungu kuhusu siku zijazo. Katika Agano la Kale na Jipya, Mungu alitumia manabii na/au kipawa cha unabii kufunua ukweli kwa watu. Unabii unatangaza ukweli wa Mungu; ni ufunuo maalum, ukweli ambao hauwezi kutambuliwa kwa njia nyingine yoyote. Kupitia nabii, Mungu angefunua ukweli ambao watu walihitaji kujua, na wakati mwingine, ukweli huo ungerekodiwa kwa namna ya maandishi. Hili, hatimaye, lilisababishwa katika Biblia, Neno la Mungu, ufunuo maalum wa mwisho kutoka kwa Mungu.

Kukamilika wa Biblia huathiri asili ya kipawa cha unabii. Biblia ina ufunuo wote tunahitaji kwa maisha na uungu (2 Petro 1:3). Neno la Mungu linaishi na ni hai, kali zaidi kuliko upanga wowote unaokata kuwili (Waebrania 4:12). Biblia ni "yafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makossa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema"(2 Timotheo 3: 16-17). Kama matokeo, kipawa cha unabii kilibadilishwa kutoka hasa kuwa ni tamko la ufunuo mpya kutoka kwa Mungu, kwa hasa (au pekee) kuwa tamko la kile ambacho Mungu amekwisha funua, kama ilivyoandikwa katika Neno Lake.

Hii si kusema kwamba Mungu hawezi kumpa mtu mmoja ujumbe wa kutoa kwa mtu mwingine. Mungu anaweza, atafanya, na anatumia watu kwa njia yoyote anayoona inafaa. Lakini, ukweli kwamba Neno la Mungu ni kamilifu na kamili lina maana kwamba tunapaswa kutegemea juu yake kwa uongozi. Hatupaswi kutegemea manabii, vituo vya kiunabii, na masomo ya kiunabii. Neno la Mungu lina ukweli tunahitaji kujua. Neno la Mungu linaonyesha hekima tunayohitaji kujua kutumia vizuri ukweli wake. Zaidi ya hayo, tuna Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu kuongoza, kutufariji, na kutufundisha (Yohana 14:16, 26). Kutumia dhana ya unabii wa kibinafsi ili kupata ushawishi juu ya watu na kuwafanya kutegemea "uongozi wa unabii" ni upotofu wa wazi wa kipawa cha unabii wa kibiblia. Wakati wowote watu wanaamini maneno yenye makosa ya wanadamu badala ya Neno la Mungu lisilo na kosa, ni dhihaki kwa kuiga.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Unabii wa kibinafsi ni dhana ya kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries