settings icon
share icon
Swali

Ulimwengu una umri gani?

Jibu


Katika Mwanzo 1: 1, tunaambiwa kuwa "hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi." Biblia haitoi tarehe ya uumbaji; dukuu pekee ni kwamba ilitokea "mwanzoni." Kwa Kiebrania, neno linalorejelea "mwanzo" ni bereshith, maana yake ni "kichwa".

Wakristo wote wanakubali kwamba Mungu aliumba ulimwengu. Ambapo Wakristo wana maoni tofauti kwa tafsiri ya neno siku (Kiebrania yom) katika Mwanzo sura ya 1. Wale wanaohusika "siku" halisi ya saa ishirini na nne wanaamini katika ulimwengu mdogo; wale ambao wanashikilia kwenye "siku" isiyo ya kweli, ya shairi wanaamini katika dunia zee ya kale.

Wasomi wengi na wanasayansi wa Kikristo wanaamini kuwa neno la siku katika Mwanzo linamaanisha halisi, siku ya ishirini na nne. Hii ingeweza kuelezea marudio katika Mwanzo 1 wa tamko "na kulikuwa na usiku, na kukawa na mchana." Usiku mmoja na mchana moja hufanya siku moja (kwa kuhesabu kwa Wayahudi, siku mpya huanza jua linapotua). Wengine huelezea matumizi yasiyo ya kweli ya neno siku mahali pengine katika Maandiko, kwa mfano, "siku ya Bwana," na kusema kwamba usiku na mchana haifai na ni lazima ieleweke kama mfano kuelezea mwanzo na mwisho wa muda.

Ikiwa nasaba katika Mwanzo sura ya 5 na 11 na historia yote ya Agano la Kale hutafsiriwa kwa usahihi, uumbaji wa Adamu unaweza kuwa na takriban 4000 BC. Lakini hii ingekuwa tu tarehe ya uumbaji wa Adamu, si lazima uumbaji wa dunia, sio hata ulimwengu. Pia kuna uwezekano wa "pengo" la muda katika maelezo ya Mwanzo 1.

Yenye tunayoweza kusema, Biblia hautupi moja kwa moja umri wa ulimwengu. Huduma ya Got Question inachukua kauli ya dunia changa na inaamini halisi kuwa, siku ya saa ishirini na nne katika Mwanzo 1 ni tafsiri bora. Wakati huo huo, hatuwezi kutokubaliana sana na wazo kwamba dunia na ulimwengu inaweza kuwa zee zaidi kuliko miaka 6,000. Ikiwa tofauti zinaelezewa na mapengo au kwa Mungu kuunmba ulimwengu na "kuonekana kwa umri" au kwa sababu nyingine — ulimwengu kuwa zaidi ya miaka 6,000 haisababishi shida kubwa ya kibiblia au ya kitheolojia.

Hatimaye, hata hivyo, umri wa ulimwengu hauwezi kuthibitishwa kutoka kwa Maandiko au sayansi. Ikiwa dunia ina umri wa miaka 6,000 au mabilioni ya umri, maoni ya wote (na kila kitu katikati) hutegemea imani na mawazo. Ni busara daima kuhoji nia za wale wanaosema dunia lazima kuwa mabilioni ya umri wa miaka, hasa tangu Biblia haionekani kuunga mkono azimio hilo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ulimwengu una umri gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries