settings icon
share icon
Swali

Je, imani ya kuleta umoja wa wakristo ni ya kibiblia? Je! Mkristo anapaswa kujihusisha katika harakati ya muungano wa madhehebu?

Jibu


Walter A. Elwell, katika Kamusi ya Teolojia ya Muhtasari wa Kiinjili, anaelezea imani ya kuleta umoja wa wakristo wote kama "jaribio lililopangwa kwa kuleta ushirikiano na umoja kati ya Wakristo." Katika ngazi ya kimataifa, Halmashauri ya Dunia ya Makanisa linawakilisha umoja wa wakristo wakati linasema lengo lake kwa njia hii: "Halmashauri ya Dunia ya Makanisa ni ushirika wa makanisa ambayo yanakiri Bwana Yesu Kristo kama Mungu na Mwokozi kulingana na maandiko, na hivyo kutafuta kutimiza kwa pamoja wito wao wa kawaida kwa utukufu wa Mungu mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni jumuiya ya makanisa kwa njia ya kuonekana umoja katika imani moja na ushirika mmoja wa Karamu ya Bwana, unaoonyeshwa katika ibada na katika maisha ya kawaida katika Kristo. Inatafuta kuendeleza umoja huu, kama Yesu alivyowaombea wafuasi wake, "ili ulimwengu upate kusadiki" (Yohana 17:21)" (www.wcc-coe.org). Hati inayoitwa Kiinjili na Katoliki Pamoja: Ujumbe wa Kikristo katika Milenia ya Tatu, iliyochapishwa mwaka 1994 na kuidhinishwa na wawakilishi wengine walio maarufu wa Ukristo wa Kiinjili na Ukatoliki wa Roma, ni mfano mwingine wa umoja wa wakristo.

Umoja wa wakristo pia unaweza kufafanuliwa kwa kina zaidi: "harakati ambayo inakuza umoja duniani kote miongoni mwa dini zote kwa ushirikiano mkubwa." Kwa mfano, kuhani Mkristo anaweza kumwaalika imamu wa Kiislamu kuzungumza kwenye mimbari yake, au kanisa linaweza kuungana na hekalu la Hindu kushiriki huduma ya maombi ya pamoja. Kufafanuliwa kwa njia hii, umoja wa wakristo ni vibaya kabisa. Hatupaswi "kuunganishwa pamoja na wasioamini" (2 Wakorintho 6:14; tazama pia Wagalatia 1:6-9). Mwanga na giza hawana ushirika na kila mmoja.

Kwa makala haya, tutazuia ufafanuzi wa umoja wa wakristo kwa "mweelekeo wa umoja kati ya makundi ya Kikristo." Swali muhimu ni hili: Je, mafundisho ya muungano wa madhehebu unafaa na wa kibiblia? Je, tunapaswa kushirikiana na "Wakristo" wengine katika mafundisho ya pamoja kimtaa, kitaifa, au kimataifa? Jibu si kamili. Kwa kweli, umoja kati ya Wakristo wa kweli ni muhimu (Zaburi 133:1; Yohana 17:22). Lakini ikiwa baadhi ya wale wanaodai kuwa Wakristo kwa kweli wanakataa msingi fulani wa imani? Mtu lazima azingatie kila hali kibinafsi. Hapa kuna maswali kadhaa ambayo yatatusaidia kufanya maamuzi ya heshima ya Mungu kuhusu umoja wa wakristo:

Kwanza kabisa, je, wale ambao tunajiunga nao na Wakristo wa kweli katika maana ya kibiblia ya neno? Watu wengi na mashirika hurejelea jina la Yesu Kristo na hata kutaja Yeye ni Bwana na Mwokozi lakini bado wanakataa wazi kile Biblia inasema juu yake. Mifano ya wazi ya haya ni Wamormoni na Mashahidi wa Yehova, ambao hunajiita wafuasi wa Yesu Kristo na kudai kuwa "Wakristo" bado wanakataa kile Biblia inasema kuhusu asili na kazi ya Kristo. Mfano usio wa dhahiri ni Ukristo wa ukarimu. Ukristo wa Ukarimu hupatikana karibu kila dhehebu, na, ingawa inaweza kuonekana kuwa Kikristo, kwa kawaida hukataa ukweli kadhaa muhimu. Wafuasi wa ukarimu mara nyingi hukataa au kupunguza msukumo na mamlaka ya Biblia (2 Timotheo 3:16), asili ya pekee ya wokovu katika Kristo (Yohana 14:6, 1 Timotheo 2:5), na utegemeaji kamili juu ya neema ya Mungu, mbali na kazi za kibinadamu, kwa ajili ya wokovu (Warumi 3:24, 28; Wagalatia 2:16; Waefeso 2:8-9).

Kuna msisitizo mkubwa katika siku yetu juu ya umoja wa muungano wa madhehebu kati ya wainjilisti na Wakatoliki wa Roma. Wale wanaokuza umoja wa hali hiyo kuwa makundi yote ni Wakristo na yote ni mifumo ya imani ya heshima ya Mungu. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya vikundi viwili. Ukristo wa Kibiblia na Ukatoliki ya Kirumi ni dini mbili tofauti ambazo hufanya na kuamini mambo tofauti kuhusu jinsi mtu anaokolewa, mamlaka ya Biblia, ukuhani wa waumini, hali ya mwanadamu, kazi ya Kristo msalabani, nk. Orodha ya tofauti ambazo haziwezi kupatanishwa kati ya kile ambacho Biblia inasema na kile Kanisa la Katoliki ya Kirumi inasema inafanya kazi yoyote ya pamoja kati ya hizo mbili haiwezekani. Wale ambao wanakataa hili hawana ukweli kwa kile wanachosema wanaamini, bila kujali ni upande gani wako. Mkatoliki yeyote ambaye ni makini juu ya imani yake atakataa kile Mkristo wa kiinjili makini anaamini, na kinyume chake.

Moja ya mkusanyiko wa umoja wa wakristo ni kwamba mara nyingi makundi ya kiteolojia yaliyotofautiana ni shauku kwa nia sawa kuhusu masuala fulani. Wakristo wa Kibiblia hushikilia msimamo wa nguvu wa maisha, mtazamo wa jadi wa familia, imani ya kutunza wasio na maakazi na wagonjwa, na hamu ya kuona haki duniani. Makundi mengine, ambayo yanaweza kuwa na teolojia isio ya kibiblia, yanaweza kushikilia nafasi sawa kijamii. Hivyo, jaribio la kukusanya rasilimali katika kutafuta sababu sawa wakati mwingine ni muhimu. Hii inasababisha swali linalofuata.

Pili, ni nini lengo kuu la jaribio hili la muungano wa madhehebu? Maandiko hutoa mwongozo wazi kuhusu jinsi Wakristo wanaoamini Biblia watakavyoishi. Wakolosai 3:17 inasema kusudi letu kwa njia hii: "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye." Kuhusu utangamano wetu na waliopotea, Yesu anasema katika Mathayo 5:16, "Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni." Mathayo 28:18-20 na 1 Wakorintho 2:2 inafanya injili kuwa kipaumbele chetu cha juu. Yote tunayofanya ni kuleta utukufu na heshima kwa Mungu, tunapaswa kuishi katika matendo mema mbele ya dunia iliyopotea na kufa, na lazima tulete kwa ulimwengu ujumbe wa kubadilisha maisha ya injili. Kushiriki kifo na ufufuo wa Kristo huleta utukufu kwa Mungu na lazima kuhamasisha ushirikiano wetu na ulimwengu.

Kuhusu jaribio la muungano wa madhehebu, tunahitaji kuuliza ikiwa malengo haya yanatafutwa au la. Mara nyingi, kushiriki injili inakuwa wazo la baadaye, ikiwa itafikiriwa kabisa hata hivyo. Katika nafasi ya injili, umoja wa wakristo huonekana kuzingatia ujumbe wa kisiasa na kijamii. Badala ya kutafuta kubadilisha mioyo, juhudi za muungano wa madhehebu mara nyingi hutafuta kubadilisha mazingira-kisiasa, kijamii, au kifedha. Lengo kuu la vitendo vyetu lazima iwe wokovu wa wenye dhambi waliopotea (Waefeso 2:1-3). Malaika wa mbinguni wanashangilia juu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu (Luka 15:10). Hakuna kitu katika Biblia kinachosema kwamba malaika hufurahi wakati sheria inapitishwa, wakati kisima kinachimbwa, au wakati barabara inatengenezwa. (Sio kwamba kuna kitu chochote kibaya kwa kukamilisha mambo hayo, lakini hayawezi kuruhusiwa kufunika injili.) Tunapofikiria jaribio la muungano wa madhehebu, tunahitaji kuhakikisha kwamba ufalme wa Mungu unenea kupitia uinjilisti.

Kwa kumalizia, tunapaswa kushiriki katika ushirikiano wa muungano wa madhehebu na makanisa mengine ya Kikristo na makundi mengine ya waumini? Ikiwa hakuna maelewano ya mafundisho juu ya msingi wa imani ya Kikristo, ikiwa injili haipunguzwi au kupuuzwa, ikiwa waumini wanaweza kudumisha ushuhuda wazi mbele ya ulimwengu, na ikiwa Mungu anatukuzwa, basi tunaweza kujiunga kwa uhuru na furaha na waumini wengine katika kutafuta ufalme wa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, imani ya kuleta umoja wa wakristo ni ya kibiblia? Je! Mkristo anapaswa kujihusisha katika harakati ya muungano wa madhehebu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries