settings icon
share icon
Swali

Je, kanisa inaweza aje kufanikisha umoja wa kibiblia ambao ni wa ukweli?

Jibu


Biblia inahimiza umuhimu wa umoja na muungano. Umoja kati ya wengine ni nzuri na ya kufurahisha (Zaburi 133:1). Umoja ni muhimu kwa sababu kanisa ndio mwili wa Kristo (1Wakoritho 12:27), na mwili huezi jitenganisha ama kujikosesha amani. Utengano ukifanyika, basi linakoma kuwa mwili na kuwa kundi la watu waliotengana. Mpango wa Yesu kwa kanisa lake ni watu washiriki kwa imani.

Siri ya umoja inaanza na jinsi tunavyojiona sisi wenyewe kimwili na jinsi tunavyoona wengine. Kifungu ambacho kinaelezea suala ili ni Wafilipi 2:3: "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake." Utengano mara mingi hutokea kanisani wakati tunapokua na tamaa na kujiona wazuri kuliko wengine. Paulo anaendelea kueleza kwa kifungu hiki: "Kila mmoja wenu hafai kuangalia tu manufaa yake mwenyewe bali manufaa ya wengine pia." Cha kuhuzunisha ni kuwa kanisa ambazo zinapitia utengano na migogoro, mara nyingi zimejawa na watu ambao wanaangalia tu mahitaji yao,matarajio yao na tamaa zao tu. Tabia kama hizi hupatikana kwa watu ambao si waumini bali si wale wenye fikra za Kikristo. Kuishi kudunia na si kimungu ndio sifa za kanisa ambayo imetengana, jinsi Paulo aliwakumbusha wakoritho: "Kwa maana ninyi bado mnatawaliwa na mambo ya mwili, je wakati kuna wivu na kugombana kati yenu, ninyi si watu wa mwili wenye tabia kama za watu wa kawaida."(1Wakoritho 3:3)

Lakini Paulo anatuambia kwamba tunafaa kuzingatia mahitaji ya wengine kabla tuzingatie yetu. Kwa adabu,unyenyekevu na fikra za ukarimu, tunafaa kuwa "wanyenyekevu, wapole, wenye subira, mkivumiliana ninyi kwa ninyi katika upendo" (Waefeso 4:2). Kanisa ambalo limejawa na watu kama hawa haliezi kupeana msaada bali kuwa na amani,umoja na maelewano. Mtu ambaye ni mnyenyekevu wa ukweli huwa anaona makosa yake kwa mwangaza kulingana na mapenzi ya Kristo; yeye huwa hashughuliki kuangalia makosa yaw engine, lakini anapofanya, anaongea ukweli kwa upendo na kutamani utakaso wake ili kuiga mfano wa Kristo . Anaona roho yake na uongo zote ambazo zimejificha ndani yake pamoja na nia mbaya na fikra za kidhambi. Lakini hatafuti kuona makosa, kasoro na ujinga wa wengine. Anaona upotovu wa moyo wake mwenyewe na kutarajia hisani kutoka kwa uzuri wa watu na kuamini kwamba mioyo yao imekamilika kuliko wake.

Kama Wakristo tunafaa kuona wezetu kwa mwangaza kama uko msalabani. Wakristo wezetu ni wale ambao Yesu alikufa kifo cha kutisha na uchungu kwa ajili yao ili abadalishe wema wake na dhambi zao( 2Wakorintho 5:21). Tunaeza aje kosa kuwapa upendo, huruma na neema za Baba wetu wa mbinguni? Tunaeza aje dhalilisha, kukosoa, na kukashifu wale ambao wamefunikwa na damu takatifu ya Kristo? Je, hatukua watumwa wa dhambi wakati alituita, kama tumepotea bila matumaini, ka tumekufa kwa makosa yetu wenyewe na dhambi( Waefeso 2:1)? Lakini sasa tumekua watumwa wa Kristo, watumwa wa haki na kama watumwa wa Mkuu, jukumu letu si kugombana na kutarajia mahitaji yetu kutimizwa ila ni kurejelea neema yake na upendo kwa wale ambao ni wake kwa rehema yake. Kanisa ambalo limejawa na watu kama hawa ambao wanafurahia wokovu wao itakua mfano kamili wa kanisa la kikiblia ambayo iko umoja, na kushindana kwa bidii kwa "imani iliyopewa watakatifu" (Judea 1:3).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kanisa inaweza aje kufanikisha umoja wa kibiblia ambao ni wa ukweli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries