settings icon
share icon
Swali

Wakristo wanapaswa kushughulikiaje umasikini na njaa duniani?

Jibu


Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, zaidi ya watu milioni 840 ulimwenguni kote ni wamedhoofika kiafya kwa kuwa hawana chakula cha kutosha. Kila siku, watoto wadogo 26,000 wanakufa kutokana na umasikini, njaa, na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa. Wakati idadi kubwa ya watu dunia wakiwa katika hali hiyo ya kusikitisha, Mkristo anapaswa kufanya nini? Kanisa linapaswa kushughulikia suala hili vipi?

Wakristo wanapaswa kukabiliana na umasikini na njaa duniani kwa huruma. Kuwa na huruma ya kweli kwa maskini, kama ilivyoelezwa na Yesu (Marko 8: 2), inamaanisha tunajua haja, tunawajali watu wanaohusika, na tuko tayari kutenda kwa niaba yao. Kuwa na rehema kwa ndugu aliyehitaji ni ushahidi wa upendo wa Mungu ndani yetu (1 Yohana 3:17). Tunamheshimu Mungu tunapokuwa wenye huruma kwa maskini(Mithali 14:31).

Wakristo wanapaswa kukabiliana na umasikini na njaa duniani kwa matendo. Bila shaka, sala kwa wale wanaohitaji ni kitu ambacho kila Mkristo anaweza kufanya. Zaidi ya hayo, Wakristo wanapaswa kufanya yote wanayoweza ili kupunguza mateso yanayosababishwa na umasikini na njaa duniani. Yesu alisema, "Viuzeni mlivyo navyo, mwape maskini. . . . Kwa maana hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo ma mioyo yenu"(Luka 12: 33-34). Kama Tabitha, tunapaswa "daima kuwa tunatenda mema na kuwasaidia maskini" (Matendo 9:36).

Waumini ambao huwapa maskini kwa hiari watabarikiwa na Mungu. "Amhurumiaye masikini humkopesha Bwana, / naye atamlipa kwa tendo lake jema" (Methali 19:17). Baraka hizi za kimungu zinaweza kuwa za kiroho badala ya vifaa, lakini malipo ni ya uhakika-kutoa kwa maskini ni uwekezaji wa milele.

Kuna mashirika kadhaa ya kikristo ya misaada ambayo huwa haipambani na umasikini na njaa duniani tu, bali pia kushiriki injili ya Yesu Kristo. Vikundi kama vile Compassion International hujitahidi kufikia mahitaji ya mtu yote, kimwili na kiroho.

Wakristo wanapaswa kupambana na umasikini na njaa duniani kwa kuwa na tumaini. Waumini wanaweza kutenda kwa niaba ya masikini kwa kujiamini kuwa wanasaidia kazi zaidi ya Mungu ulimwenguni: "Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu/ na wahitaji haki yao" (Zaburi 140: 12). Waumini hufanya kazi kwa matumaini ya kwamba Yesu atarudi, na "atawahukumu maskini , naye atawaoya wanyeyekevu wa dunia kwa adili, (Isaya 11: 4).

Mpaka siku hiyo ya usawa wa mwisho, Yesu alisema, "Kwa maana siku zote mnao maskini " (Mathayo 26:11). Kwa hiyo, tuna fursa zisizo na kikomo-na wajibu wa haraka — kumtumikia Bwana kwa kuwahudumia wengine.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wakristo wanapaswa kushughulikiaje umasikini na njaa duniani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries