settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu ukuaji wa kanisa?

Jibu


Ingawa Biblia haitaji hasa ukuaji wa kanisa moja kwa moja, kanuni ya ukuaji wa kanisa ni kuelewa kwamba Yesu alisema, "Nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18). Paulo alithibitisha kuwa kanisa lina msingi wake katika Yesu Kristo (1 Wakorintho 3:11). Yesu Kristo ni kichwa cha kanisa (Waefeso 1:18-23) na uhai wa kanisa (Yohana 10:10). Baada ya kusema hayo, ni lazima ikumbukwe kwamba "ukuaji" linaweza kuwa neon la karibu. Kuna aina tofauti za ukuaji, ambazo baadhi yao hazina uhusiano wowote na ukuaji wa idadi.

Kanisa linaweza kuwa hai na kuongezeka ingawa idadi ya wanachama / wanaohudhuria haibadiliki. Kama wale walio katika kanisa wanakua katika neema na maarifa ya Bwana Yesu, wakinyenyekea kwa mapenzi yake kwa maisha yao, kibinafsi na kwa ushirika, hilo ndilo kanisa linahisi ukuaji wa kweli. Wakati huo huo, kanisa linaweza kuongezeka katitka daftari ya rekodi kila juma, kuwa na idadi kubwa, na bado kuwa palepale kiroho.

Ukuaji wa aina yoyote hufuata mtindo wa kawaida. Kama ilivyo kwa viumbe kinachokua, kanisa la nyumbani lina wale ambao hupanda mbegu (wainjilisti), wale ambao hunyunyizia mbegu maji (mchungaji / walimu ), na wale ambao wanatumia karama zao za kiroho kwa ukuaji wa wale walio katika kanisa la nyumbani. Lakini kumbuka kwamba ni Mungu anayeiwezesha mbegu kuota (1 Wakorintho 3:7). Wale ambao hupanda na wale ambao hunyunyuzia maji kila mmoja hupokea malipo yao kwa mujibu wa kazi yao (1 Wakorintho 3:8).

Lazima kuwe na uwiano kati ya kupanda na kunyunyuzia ndio kanisa la nyumbani likue, ambayo ina maana kwamba katika kanisa lenye afya kila mtu lazima ajue karama yake ili aweze kufanya katika mwili wa Kristo. Kama kupanda na kunyunyizia zinapita nje ya uwiano, kanisa haliwezi endelea vile lengo la Mungu lilikua. Bila shaka, inabidi kuwe na utegemezi kila siku katika utii wa Roho Mtakatifu ili uwezo wake uweze kuachiliwa katika wale ambao kupanda na kunyunyizia maji ili Mungu aifanye iongezeke.

Hatimaye, maelezo ya kanisa lilo hai na kukua yanapatikana katika Matendo 2:42-47 ambapo waumini "wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali." Walikuwa kuhudumiana na kufikia wale waliohitaji kumjua Bwana, kwa ajili ya Bwana "akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa." Wakati mambo hayo yanaendelea, kanisa litahisi ukuaji wa kiroho, hata kama kuna ongezeko la kiidadi au la.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu ukuaji wa kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries