settings icon
share icon
Swali

Je, ukiokolewa mara moja umeokolewa siku zote?

Jibu


Je, mtu akiokolewa, ameokolewa siku zote? Watu wakimtambua Kristo kama mwokozi wanaunganishwa katika ushirika na Mungu unaowahakikishia wokovu wao milele. Aya nyingi za Biblia huyathibitisha haya. (a) warumi 8:30 inasema, “na wale aliowaandalia makao aliwaita; wale aliowaita aliwafanya kuwa wenye haki na wale aliowafanya kuwa wenye hakipia aliwatukuza.” Hii ina maana ya kuwa wakati tunapochaguliwa na Mungu, ni kama tunatukuzwa mbinguni mbele zake. Kwa kuwa ameazimia haya mbinguni tutukuzwe hakuna anayeweza kukataza aliyeamini asitukuzwe. Anapofanywa kuwa mwenye haki wokovu wake ni imara kama aliyetukuzwa tayari mbinguni.

(b) Paulo auliza maswali mawili muhimu katika warumi 8:33-34 “ni nani atakayewashtaki waliochaguliwa na Mungu? Ni Mungu ahalalishaye. Ni nani basi huyo ahukumuye? Kristo Yesu, aliyetufia,akafufuka kutoka kwa wafu na sasa yuko mkono wa kuuma wa Mungu anatuombea.” Ni nani atakaye washtaki wateule wa Mungu? Hakuna, kwa kuwa kristo ndiye mtetezi wetu. Ni nani atakaye tushtaki? Hakuna, kwa kuwa kristo aliyetufia ndiye ahukumuye. Mwokozi wetu ndiye mtetezi wetu na pia ni hakimu.

(c) waumini huzaliwa mara ya pili (hufanywa upya) wanapoamini (Yohana 3:3; Tito 3:5). Kwa mkristo kupoteza ukristo wake ingehitajika aondolewe kufanywa upya kwake. Biblia haitoi ushahidi wa kuwa kuzaliwa mara ya pili kwa mtu kunaweza kuondolewa. (d) Roho mtakatifu anadumu ndani ya kila mwenye kuamini (Yohana 14:17; warumi 8:9) na huwabatiza waumini wote ndani ya mwili wa kristo (wakorintho wa kwanza 12:13). Kwa muumini kuondolewa wokovu wake, ingehitajika atolewe na atenganishwe kutoka ndani ya mwili wa kristo.

(e) Yohana 3:15 inaeleza kuwa yeyote amwaminiye Yesu kristo “ana uzima wa milele.” Unapomwamini kristo leo na kupata uzima wa milele baadaye uupoteze kesho huwa haukuwa wa milele kamwe. Na ukipoteza wokovu wako basi swala la uzima wa milele katika Biblia litakuwa na kasoro. (f) kwa kumalizia, maandiko yanasema vyema, “kwa kuwa nimeshawishika ya kuwa si kifo wala uhai, malaika wala pepo, wakati uliopo wala ujao, wala mamlaka yoyote, urefu wala kina, wala chochote katika viumbe vyote, kitatutenganisha na upendo wa Mungu uliomo ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu” (warumi 8:38-39). Kumbuka Mungu yule aliyekuokoa ndiye atakaye kuhifadhi. Tukishaokolewa tunabaki kila siku tumeokolewa. Kuokolewa kwetu ni kwa milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ukiokolewa mara moja umeokolewa siku zote?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries