settings icon
share icon
Swali

Wazazi Wakristo wanapaswa kushughulikia vipi msichana mdogo anapokuwa mjamzito?

Jibu


Inaonekana kwamba mojawapo ya mambo magumu sana kwa Wakristo kukumbuka ni kwamba sio dhambi kuwa na mimba. Sio dhambi kuwa mjamzito nje ya ndoa. Na sio dhambi ya kuzaliwa kwa wazazi ambao hawajaoana. Ni dhambi kufanya ngono nje ya uhusiano wa ndoa-na ni dhambi tu kwa mwanaume kama ilivyo kwa mwanamke. Lakini uhusiano wa karibu usio na kibiblia ni jambo rahisi sana kujificha kutoka kwa macho ya watu zaidi kuliko mimba na, kwa kusikitisha, hudhuru zaidi sifa ya familia ya kikristo katika jamii.

Ni jambo linarokera kwa mzazi kutambua kwamba msichana wao mdogo kama ni mjamzito, lakini la muhimu kuwa na mtazamo wa ufalme. Dhambi imefanyika tayari. Chochote kilochokuwa kinawashawishi vijana kufanya dhambi hakiwezi kuepukwa sasa. Hali hii mpya sio kuhusu maadili ya ngono ya nje ya ndoa au sifa ya familia. Ni kuhusu ukuaji wa mtoto. Watoto wote ni baraka kutoka kwa Mungu, na ana mpango kwa kila mmoja (Zaburi 139: 13-18). Hata kama hali ambayo mtoto huja inaweza kuwa chini ya bora, mtoto huyo ni wa thamani na anapendwa na Mungu kama nwingine yoyote.

Binti mjamzito pia niwa thamani kwa Mungu. Jukumu la wazazi ni kufundisha na kuongoza watoto wao kuishi maisha ya kimungu katika chochote wanachokabiliana nacho. Hii ni fursa kubwa ya kufanya hivyo tu. Msichana anaweza kuwa na hofu, aibu, na kihisia mbalimbali, na ni wajibu wa wazazi wake kumsaidia kutokwamilia hisia hizo na kumgeukia Baba yake wa Mbinguni.

Wazazi wengine wanaogopa kuwa kumpa binti yao upendo na msaada anaohitaji itasisitiza tabia ambayo imesababisha mimba. Lakini, tena, kuwa na ujauzito na kuzaa mtoto sio dhambi, na kuna faida nyingine nyingi za kusimama kikamilifu na kwa umma na kijana aliyepata mimba. Inalenga mazingira ambayo mtoto anahesabiwa kuwa baraka. Inatia moyo baba kuchukua jukumu bila hofu. Na hufanya wasichana wasichague kuavya mimba.

Ikiwa familia itamwacha kijana wao mjamzito-hata kihisia-atakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya maamuzi yanayoleta madhara. Anaweza kufikiria kuoa baba ya mtoto ni chaguo pekee. Huenda asijue jinsi ya kutunza afya yake na ya mtoto. Vijana wengine wajawazito wanaweza kuona uhusiano huo na kuweka hali yao wenyewe kama siri.

Kinyume chake, msichana ataweza kufanya maamuzi mengi mazuri juu ya maisha ya baadaye ya mtoto wake ikiwa anaweza kupumzika akijua amekubalika kwa wazazi wake na kupata mwongozo wa upendo. Kufanya safari hii ngumu kihisia kwake haitahimiza fikra nzuri. Wazazi wa hekima watasaidia binti yao kufanya uchaguzi kwa baina ya kukaa na mtoto au kumpeana kwa wazazi badala. Inaweza pia kuwa na manufaa kuhusisha baba ya mtoto na familia yake; anahitaji kuchukua umiliki mkubwa kama mama mtotot. Baada ya maombi makini, wazazi wanapaswa kuwa wazi kuhusu kiwango cha msaada wanaoweza kumpa binyi yao katika kumlea mtoto. Tumia vitua vya ujauzito vya uzazi ambavyo ni vya Kikristo.

Mungu wetu ni Mungu mwenye nguvu ambaye anaweza kuleta furaha na baraka hata katika dhambi zetu. Kunaweza kuwa na nyakati nyingi ngumu mbele kwa kijana mjamzito na familia yake, lakini Mungu wetu ni Mungu anayekomboa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wazazi Wakristo wanapaswa kushughulikia vipi msichana mdogo anapokuwa mjamzito?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries