settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kuwa na mtazamo upi kuhusu ujamaa?

Jibu


Wanafalsafa wengi kwa karne nyingi wameamini kwamba historia imeundwa na mawazo, kufuata ukweli halisi, au ile fikra ya kibinadamu. Lakini kuna mwanasayansi mmoja maarufu ambaye badala yake alisema kwamba uchumi ndio kitu cha muhumu sana katika historia ya mwanadamu. Karl Marx alizaliwa kwa wazazi wa Kiyahudi wa asili ya Kijerumani mwaka wa 1818 na alipata cheti chake cha masomo ya juu zaidi akiwa na umri wa miaka 23. Kisha akaanzisha ujumbe wa kuthibitisha kwamba utambulisho wa kibinadamu umehusishwa na kazi ya mtu na kwamba mifumo ya kiuchumi inadhibiti binadamu. Alijadili kwamba kujimudi kimaisha inategemea kazi yake mwanadamu. Marx aliamini kwamba jamii za binadamu zinaundwa na mgawanyiko wa kazi.

Marx alisoma historia na alihitimisha kwamba kwa mamia ya miaka, kilimo kimekua msingi wa jamii. Lakini Mapinduzi ya Viwanda yalibadilli yote fikra za Marx, kwa sababu wale ambao walijifanyia kwa kazi walikuwa sasa wamelazimishwa na uchumi kufanya kazi katika viwanda. Marx alihisi kwamab hili, liliondoa heshima yao na utambulisho kwa sababu kazi yao ndio ilikua kitambulisho chao, na sasa walipunguzwa kuwa watumishi tu walioongozwa na msimamizi wa kazi. Mtazamo huu ulimaanisha kwamba uchumi wa ubepari ilikuwa adui wa asili wa Marx.

Marx alibainisha kwamba ubepari unasisitiza mali binafsi na kwa hiyo, kupunguza umiliki kwa wachache walio na fursa. "Jamii" mbili tofauti zlijitokeza katika fikra za Marx: wamiliki wa biashara, au (bourgeoisie); na wale ambao ni wafanya kazi, au (proletariat). Kwa mujibu wa Marx, matumizi ya wajasiriamali huwadhulumu wale wafanyi kazi yaani ( proletariat) na hivyo matokeo yake nukiuwa faida ya mtu Fulani inageuka hasara ya mwingine. Aidha, Marx aliamini kwamba wamiliki wa biashara wanaathiri wabunge ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa dhidi ya kupoteza kwa heshima na haki za wafanyakazi. Mwisho, Marx aliona kuwa dini ni "opiate ya raia" ambayo tajiri hutumia kuwacheza shere wale wafanyikazi; wajadala wanaahidiwa zawadi mbinguni siku moja ikiwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii ambako Mungu amewaweka (wanajishughulisha na wajasiriamali).

Katika utopia ya kidunia Marx alidhani, watu wote wanamiliki kila kitu na wote hufanya kazi kwa manufaa ya wanadamu. Lengo la Marx lilikuwa kukomesha umiliki wa mali binafsi kupitia umiliki wa serikali wa njia zote za uzalishaji wa kiuchumi. Baada ya mali ya kibinafsi kufutwa, Marx alihisi kuwa utambulisho wa mtu utainuliwa na ukuta ambao ni wa ufanyabiashara uliojengwa kuwa kati ya wamiliki na wafanya kazi utaondolewa. Kila mtu atathaminiana na kufanya kazi kwa pamoja kwa kusudi la pamoja.

Kuna makosa angalau nne katika kufikiri kwa Marx. Kwanza, kudai kuwa faida ya mtu mwingine lazima iwe kwa gharama ya mtu mwingine ni si kweli; muundo wa ubepari unaacha nafasi nyingi kwa wote kuongeza kiwango cha maisha yao kupitia uvumbuzi na ushindani. Inawezekana kwa vyama vingi kushindana na kufanya vizuri katika soko la watumiaji ambao wanataka bidhaa na huduma zao.

Pili, Marx alikuwa na makosa katika imani yake kwamba thamani ya bidhaa inategemea kiasi cha kazi kinachojitajika kukiunda. Ubora wa kitu au huduma nzuri haiwezi kuamua kwa kiasi cha jitihada ambazo mfanyakazi hutumia. Kwa mfano, muumbaji mkuu anaweza haraka zaidi na kwa uzuri kufanya samani kuliko wafundi wasio na ujuzi , na kwa hiyo kazi yake ina gharama zaidi (na kwa usahihi hivyo) katika mfumo wa kiuchumi kama vile ukadari.

Tatu, nadharia ya Marx inahitaji serikali ambayo haina ufisadi na inakataa uwezekano wa kuwapanga watu katika njancha za kiuchumi (elitism). Ikiwa historia imeonyesha chochote, ni kwamba nguvu huathiri bidadamu mwenye dhambi, na mamlaka huwaathiri kabisa. Taifa au serikali inaweza kuua wazo la Mungu, lakini mtu atachukua nafasi ya Mungu. Mara nyingi inawezakuwa ni mtu binafsi au kikundi ambacho huanza kutawala idadi ya watu na hutaka kuhifadhi nafasi yao ya kibinafsi kwa gharama zote.

Nne na muhimu zaidi, Marx alikosea kusema kwamba utambulisho wa mtu umefungwa ama ni kupitia katika kazi aliyofanya. Ingawa jamii za kidunia hakika hulazimisha imani hii karibu kwa kila mtu, Biblia inasema kwamba wote wana thamani sawa kwa kuwa wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu wa milele. Hiyo ndio kweli, thamani ya kibinadamu ya kweli .

Je! Marx alikuwa sahihi? Je, uchumi ni kichocheo kinachoongoza historia ya mwanadamu? Hapana, kinachoongoza historia ya kibinadamu ni Muumba wa ulimwengu ambaye anadhibiti kila kitu, pamoja na kupanda na kuanguka kwa kila taifa. Zaidi ya hayo, Mungu pia anadhibiti ambaye anapewa mamlaka juu ya kila kila taifa, kama Maandiko yasema, "Aliye juu sana ndiye mtawala juu ya ulimwengu wa wanadamu, na humpa mamalaka anayemchagua na kuiweka juu yake watu wa chini kabisa" (Danieli 4 : 17). Zaidi ya hayo, ni Mungu ambaye hupa ujuzi wa mtu katika kazi na utajiri kutoka kwa kazi hio, sio serikali: "Hii ndio niliyoona kuwa ni mema na yenye kufaa: kula, kunywa na kujifurahisha katika kazi ya mtu yoyote ambayo anafanya chini ya jua wakati wa miaka michache ya maisha yake ambayo Mungu amempa; kwa maana hii ndiyo malipo yake. Zaidi ya hayo, kwa kila mtu ambaye Mungu amempa utajiri pia amempa uwezo wa kula kutoka kwake na kupokea thawabu yake na kufurahia kazi yake; hii ni zawadi ya Mungu "(Mhubiri 5: 18-19).

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kuwa na mtazamo upi kuhusu ujamaa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries