settings icon
share icon
Swali

Je, Uhuishaji ni nini?

Jibu


Uhuishaji ni imani kwamba kila kitu kina nafsi au roho, anima katika Kilatini, ikiwa ni pamoja na wanyama, mimea, miamba, milima, mito na nyota. Wachawi wanaamini kila anima ni roho yenye nguvu ambayo inaweza kuwasaidia au kuwaumiza na inafaa kuabudiwa au kuogopwa au kwa namna fulani kutambuliwa. Uhuishaji ni dini ya kwanza ambayo wafuasi wake wamekuwepo kwa maelfu ya miaka na wanauhisha wanyama, nyota, na sanamu za aina yoyote na kufanya mazoea ya usingaombwe, uchawi, uganga na urolojia. Wanatumia uchawi, maelekezo, uchawi, ushirikina, uongo, michoro, shanga, au kitu chochote ambacho wanaamini kitasaidia kuwalinda kutoka roho mbaya na kuwapatia roho nzuri.

Mambo ya uhuishaji yapo katika dini nyingi za uwongo ikiwa ni pamoja na Uhindu, Umomoni, na ibada zote za Kizazi Kipya (New Age). Dini ya uwongo daima inafundisha kwa namna fulani kwamba roho ndani ya wanadamu kweli ni Mungu na matendo ya dini yatatusaidia kutambua hili na kuendeleza roho ya mungu ili sisi pia tufanywe kuwa Mungu. Huu ni uongo sawa Shetani amekuwa akieneza tangu bustani mwa Edeni wakati alijaribu Adamu na Hawa kwa kuwaambia, "Mtafanana na Mungu" (Mwanzo 3: 5).

Biblia inasema wazi kwamba kuna Mungu mmoja na kila kitu kingine, kutoka kwa malaika mbinguni mpaka kwenye mchanga wa pwani, uliumbwa na Yeye (Mwanzo 1: 1). Dini yoyote inayofundisha kuna zaidi ya mungu mmoja inafundisha uwongo. "kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine" (Isaya 43:10) na "Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu" (Isaya 45: 5). Kuabudu miungu ya uongo, ambao sio miungu kabisa, ni dhambi amboyo Mungu huchukia hasa kwa sababu inamwibia utukufu ambao ni kwake. Mara nyingi katika Biblia, Mungu anachukia ibada za miungu wa uongo.

Kwa kuongezea, Biblia inakataza kabisa mazoea ya wahuishaji. "Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao" (Mambo ya Walawi 20:27). Mazoea ya uhuishaji ni milango ya wazi ya mapepo kuingia katika maisha ya watu. Biblia inawakemea wale wanaofanya mambo kama hayo kwa nguvu sana (Kumbukumbu la Torati 18; Mambo ya Walawi 20; Isaya 47).

Kama ilivyo kwa dini zote za uongo, uhuishaji ni mpango mwingine tu wa Shetani, ambaye ni baba wa uongo. Lakini wengi duniani kote wanadanganywa na "kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze" (1 Petro 5: 8).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Uhuishaji ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries