settings icon
share icon
Swali

Je, nini ilikuwa utekaji nyara Babeli/uhamisho?

Jibu


Utekaji nyara Babeli au uhamisho unahusu muda wa kipindi cha historia ya Israeli wakati Wayahudi walichukuliwa mateka na Mfalme Nebukadneza wa pili wa Babeli. Ni kipindi muhimu cha historia ya kibiblia kwa sababu yote kuteka nyara/uhamisho na kurudi na kurejeshwa kwa taifa la Wayahudi ulikuwa utimizaji wa unabii wa Agano la Kale.

Mungu alitumia Babeli kama wakala Wake wa hukumu dhidi ya Israeli kwa ajili ya dhambi zao za ibada za sanamu na uasi dhidi Yake. Kwa kweli kulikuwa na nyakati kadhaa tofauti wakati wa kipindi hiki (607-586 KK) wakati Wayahudi walichukuliwa mateka na Babeli. Na kila uasi wa mfululizo dhidi ya utawala wa Babiloni, Nebukadneza angeongoza majeshi yake dhidi ya Yuda mpaka wakazingira Yerusalemu kwa zaidi ya mwaka, akiwaua watu wengi na kuharibu hekalu la Kiyahudi, akiwachukua mateka maelfu ya Wayahudi, na kuacha Yerusalemu kuwa magofu.

Kama ilivyotabiriwa katika Maandiko, watu wa Kiyahudi wangeruhusiwa kurudi Yerusalemu baada ya miaka 70 ya uhamishoni. Unabii huo ulitimizwa mwaka wa 537 KK, na Wayahudi waliruhusiwa na Mfalme Koreshi wa Uajemi kurudi Israeli na kuanza kujenga tena mji na hekalu. Kurudi chini ya mwelekeo wa Ezra uliongoza ufufuaji kati ya watu wa Kiyahudi na kujenga upya hekalu.

Chini ya utawala wa Mfalme Nebukadneza wa II, Ufalme wa Babiloni ulienea kote Mashariki ya Kati, na karibu 607 KK, Mfalme Yehoyakimu wa Yuda alilazimishwa kujisalimisha, akawa mtumishi wa Nebukadneza (2 Wafalme 24:1). Ulikuwa wakati huu ambao Nebukadneza alichukua vijana wengi walio bora sana na wenye akili zaidi kutoka kila mji wa Yuda mateka, ikiwa ni pamoja na Danieli, Hanania (Shadraki), Mishaeli (Meshaki) na Azaria (Abednego). Baada ya kumtumikia Nebukadneza kwa miaka mitatu, Yehoyakimu wa Yuda aliasi dhidi ya utawala wa Babiloni na akageuka tena kwa Misri kwa ungaji mkono. Baada ya kupeleka jeshi lake kukabiliana na uasi wa Yuda, Nebukadneza mwenyewe aliondoka Babeli mwaka wa 598 BC ili kukabiliana na shida hiyo. Alipofika Yerusalemu karibu Mwezi wa tatu wa 597 KK, Nebukadneza alizingira Yerusalemu, akichukua uthibiti wa eneo hilo, akalipora, na kuchukua mateka pamoja naye mwana wa Yehoikimu, Yehoyakini, familia yake, na karibu watu wote wa Yuda, wakiwaacha masikini tu watu wa nchi (2 Wafalme 24:8-16).

Wakati huo Nebukadneza alimteua Mfalme Sedekia kutawala kama mwakilishi wake juu ya Yuda, lakini baada ya miaka tisa na bado hawajajifunza somo lao, Sedekia aliongoza Yuda katika uasi dhidi ya Babiloni mara moja ya mwisho (2 Wafalme 24-25). Akishawishiwa na manabii wa uongo na kupuuza maonyo ya Yeremia, Sedekia aliamua kujiunga na muungano ambao uliumbwa na Edomu, Moabu, Amoni na Foinike katika uasi dhidi ya Nebukadneza (Yeremia 27:1-15). Hii ilisababisha Nebukadneza tena kuzingira Yerusalemu. Yerusalemu ilianguka Julai 587 au 586 KK, na Sedekia akachukuliwa mateka na Babeli baada ya kuona wanawe wakiuliwa mbele yake na kisha macho yake yakang'olewa (2 Wafalme 25). Wakati huu Yerusalemu ilikuwa mahame, hekalu likaharibiwa na nyumba zote zikateketezwa. Wengi wa Wayahudi walichukuliwa mateka, lakini tena, Nebukadneza aliacha mabaki ya watu masikini kuhudumia kama wakulima na watunza wa mizabibu (2 Wafalme 25:12).

Vitabu vya 2 Mambo ya Nyakati na 2 Wafalme vinahusiana na muda mwingi unaoongoza kuanguka kwa Ufalme wa Kaskazini na Yuda. Pia vunahusisha uharibifu wa Yerusalemu na Nebukadneza na mwanzo wa utekaji nyara wa Babeli. Yeremia alikuwa mmoja wa manabii wakati huo wa kuongoza kuanguka kwa Yerusalemu na uhamisho, na Ezekieli na Danieli viliandikwa wakati Wayahudi walipokuwa uhamishoni. Ezra inahusika na kurudi kwa Wayahudi kama ilivyoahidiwa zaidi ya miaka 70 kabla na Mungu kupitia manabii Yeremia na Isaya. Kitabu cha Nehemia pia kinashughulikia kurudi na kujenga upya Yerusalemu baada ya uhamishoni kukamilika.

Utekaji nyara wa Babiloni ulikuwa na athari moja muhimu kwa taifa la Israeli wakati uliporudi katika nchi – kamwe haitapotoshwa tena na ibada ya sanamu na miungu ya uongo ya mataifa yaliyozunguka. Ufufuaji kati ya Wayahudi ulifanyika baada ya Wayahudi kurudi Israeli na kujenga upya kwa hekalu. Tunaona akaunti hizo katika Ezra na Nehemia kama taifa litaweza tena kurudi kwa Mungu ambaye aliyewaokoa kutoka kwa adui zao.

Kama vile Mungu alivyoahidi kupitia nabii Yeremia, Mungu aliwahukumu Wababiloni kwa dhambi zao, na Ufalme wa Babiloni ukaanguka kwa majeshi ya Uajemi mwaka wa 539 KK, mara nyingine tena kuthibitisha ahadi za Mungu kuwa za kweli.

Kipindi cha miaka sabini cha utekaji nyara wa Babiloni ni sehemu muhimu ya historia ya Israeli, na Wakristo wanapaswa kuwa na ufahamu nayo. Kama matukio mengine mengi ya Agano la Kale, akaunti hii ya kihistoria inaonyesha uaminifu wa Mungu kwa watu Wake, hukumu Yake ya dhambi, na uhakikisho wa ahadi Zake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nini ilikuwa utekaji nyara Babeli/uhamisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries