settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu uhamiaji haramu?

Jibu


Warumi 13:1-7 inaweka wazi kabisa kwamba Mungu anatarajia sisi kutii sheria za serikali. Jambo la pekee tu kwa hili ni wakati sheria ya serikali inakulazisha kutotii amri ya Mungu (Matendo 5:29). Uhamiaji haramu ni kuvunja sheria za serikali. Hakuna kitu katika Maandiko ambayo inakinzana na taifa kuwa na sheria za uhamiaji. Kwa hivyo, ni dhambi, uasi dhidi ya Mungu, kuingia nchi nyingine kinyume cha sheria.

Uhamiaji haramu kwa hakika ni suala la utata nchini Marekani (na nchi zingine) leo. Baadhi wanajadili kuwa sheria za uhamiaji sio haki, dhalimu, na hata ni ya ubaguzi — kuwapa watu uthibitisho wa kuhamia kinyume cha sheria. Hata hivyo, Warumi 13:1-7 haitoi idhini yoyote ya kukiuka sheria kwa sababu ni dhalimu. Tena, suala sio haki ya sheria. Sababu tu ya kibiblia ya kukiuka sheria ya serikali ni kama sheria hiyo inakiuka Neno la Mungu. Wakati Paulo aliandika Kitabu cha Warumi, alikuwa chini ya mamlaka ya Falme ya Kirumi, iliyoongozwa na labda mwovu zaidi ya wafalme wote wa Kirumi, Nero. Chini ya utawala huo, kulikuwa na sheria nyingi ambazo zilikuwa si za haki, dhalimu, na/au uovu wa wazi. Hata hivyo, Paulo aliwaagiza Wakristo kujiwasilisha kwa serikali.

Je! Sheria za uhamiaji za Marekani sio za haki au dhalimu? Wengine wanafikiria hivyo, lakini hilo sio suala. Nchi zote zilizoendelea ulimwenguni zina sheria za uhamiaji, zingine kali zaidi kuliko Marekani na zingine si kali kuliko Marekani. Hakuna kitu katika Biblia kunachozuia nchi kutoka kuwa na mipaka ya wazi kabisa au kutoka kuwa na mipaka iliyofungwa kabisa. Warumi 13:1-7 pia inapatia serikali mamlaka ya kuwaadhibu wanaovunja sheria. Ikiwa adhabu ni kifungo gerezani na/au kufukuzwa, au hata kitu kali zaidi, ni ndani ya haki za serikali kuamua.

Wahamiaji haramu wengi mno nchini Marekani wamekuja kwa lengo la kuwa na maisha bora zaidi, kukimu familia zao, na kukimbia kutoka umasikini. Haya ni malengo mazuri na motisha. Hata hivyo, sio kibiblia kukiuka sheria ili kutimiza kitu "nzuri." Kuwajali maskini, mayatima, na wajane ni kitu ambacho Biblia inatuamuru tufanye (Wagalatia 2:10; Yakobo 1:27; 2:2-15). Hata hivyo, ukweli wa kibiblia kwamba tunapaswa kuwashughulikia maskini haimaanishi tunapaswa kukiuka sheria kwa kufanya hivyo. Kusaidia, kuwezesha, na/au kuhamasisha uhamiaji haramu ni, kwa hivyo, pia ni ukiukaji wa Neno la Mungu. Wale wanaotafuta kuhamia nchi nyingine wanapaswa kutii daima sheria za uhamiaji za nchi hiyo. Ingawa hili linaweza kusababisha ucheleweshaji na kuvunja moyo, sababu hizi hazimpi mtu haki ya kukiuka sheria.

Je! Ni suluhisho gani la Kibiblia kwa uhamiaji haramu? Rahisi ... usifanye; tii sheria. Ikiwa kutotii sio chaguo la kibiblia, ni nini kinachoweza kufanywa kuhusiana na sheria dhalimu za uhamiaji? Ni ndani ya haki kabisa ya raia kutafuta mabadiliko kwa sheria za uhamiaji. Ikiwa ni imani yako kuwa sheria ya uhamiaji ni dhalimu, fanya kila kitu ambacho ni kisheria ndani ya uwezo wako ili kupata sheria kubadilishwa: omba, ombi, piga kura, pinga kwa amani, nk. Kama Wakristo, tunapaswa kuwa wa kwanza kutafuta mabadilisha sheria yoyote ambayo ni dhalimu. Wakati huo huo, tunapaswa pia kuonyesha utii wetu kwa Mungu kwa kutii serikali ambayo Yeye ameweka mamlakani juu yetu.

"Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu"(1 Petro 2:13-16).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu uhamiaji haramu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries