settings icon
share icon
Swali

Uhakiki wa maandishi — ni nini?

Jibu


Kusema kwa urahasi, uhakiki wa maandishi ni njia inayotumiwa kuamua nini maandishi ya awali ya Biblia yalisema. Maandishi ya awali ya Biblia yamepotea, yamefichwa, au hayapo tena. Yale tunayo ni kumi ya maelfu ya nakala za maandiko ya awali kutoka karne ya 1 hadi ya 15 baada ya Kristo (kwa Agano Jipya) na kutoka karne ya 4 kabla ya Kristo hadi karne ya 15 baada ya Kristo (kwa Agano la Kale). Katika maandiko haya, kuna tofauti ndogo na chache muhimu. Uhakiki wa maandishi ni utafiti wa maandiko haya kwa jaribio la kuamua usomaji wa awali ulikuwa gani kweli.

Kuna mbinu tatu za msingi kwa uhakiki wa maandishi. Ya kwanza ni Receptus Textus. Textus Receptus ilikuwa hati ya Biblia iliyoandaliwa na mtu mmoja aitwaye Erasmus katika miaka ya 1500 baada ya Kristo. Alichukua idadi ndogo ya maandishi ambayo alipata na kuikusanya katika kile kilichojulikana kama Textus Receptus.

Mbinu ya pili inajulikana kama ya Nakala Wingi. Nakala ya Wingi inachukua maandiko yote ambayo yanapatikana leo, kulinganisha tofauti, na kuchagua usomaji sahihi zaidi kulingana na usomaji ambao hutokea zaidi. Kwa mfano, ikiwa maandiko 748 yasoma "alisema" na maandiko 1429 yasoma "walisema," Nakala ya Wingi itachagua "walisema" kama usomaji wa awali zaidi. Hakuna tafsiri kuu za Biblia ambazo zinategemea Nakala ya Wengi.

Mbinu ya tatu inajulikana kama mbinu ya kihakiki au isiofuata mfumo mmoja. Mbinu isiofuata mfumo mmoja inahusisha kuzingatia ushahidi wa nje na wa ndani ili kuamua maandishi ya awali. Ushahidi wa nje unatufanya tuulize maswali haya: ni katika maandiko ngapi usomaji hutokea? ni tarehe gani ya maandishi haya? Ni sehemu gani ya dunia maandishi haya yalipatikana? Ushahidi wa ndani huchochea maswali haya: ni nini kilichosababisha usomaji huu tofauti? ni usomaji gani unaweza kuelezea asili ya usomaji mwingine?

Ni mbinu gani sahihi zaidi? Hapo ndipo mjadala huanzia. Wakati mbinu zinapoelezewa kwa mtu mara ya kwanza, mtu kwa kufanana hasa huchukua Nakala ya Wingi kama mbinu ambayo inapaswa kutumiwa. Kimsingi ni mbinu ya "uamuzi wa wengi" na "kidemokrasia". Hata hivyo, kuna suala la kikanda la kuzingatia hapa. Katika karne za kwanza za kanisa, wengi wa Wakristo walizungumza na kuandika kwa Kigiriki. Kuanzia katika karne ya 4 baada ya Kristo, Kilatini ilianza kuwa lugha iliyojulikana, hasa kanisani. Kuanza na Vulgate ya Kilatini, Agano Jipya lilianza kunakiliwa katika Kilatini badala ya Kigiriki.

Hata hivyo, katika ulimwengu wa Kikristo wa mashariki, Kigiriki iliendelea kuwa lugha kuu ya kanisa kwa zaidi ya miaka 1,000 zaidi. Matokeo yake, idadi kubwa ya maandishi ya Kiyunani yanatoka mkoa wa mashariki/Byzantine. Maandishi haya ya Byzantine yote yanafanana sana. Huenda yote yalitokea katika maandishi machache ya Kigiriki. Hata ingawa yanafanana sana, maandishi ya Byzantine yana tofauti nyingi na maandiko yaliyopatikana katika mikoa ya magharibi na ya kati ya kanisa. Kwa muhtasari: ikiwa ulianza na maandishi tatu, na moja ilinakiliwa mara 100, nyingine ikanakiliwa mara 200, na ya tatu ikanakiliwa mara 5,000, ni kundi gani litakuwa na uamuzi wa wengi? Kundi la tatu, bila shaka. Hata hivyo, kundi la tatu huenda halina usomaji wa awali kuliko kundi la kwanza au la pili. Lina tu nakala nyingi. Mbinu ya kihakiki/isiofuata mfumo mmoja ya uhakiki wa maandishi hutoa "uzito" sawa kwa maandishi kutoka mikoa tofauti, licha ya maandiko kutoka Mashariki kuwa na idadi kubwa.

Je, mbinu ya kihakiki/isiofuata mfumo mmoja hufanya kazi katika mazoezi? Ikiwa unalinganisha Yohana 5:1-9 katika tafsiri mbalimbali, utaona kwamba mstari wa 4 haupo katika tafsiri kulingana na Nakala ya Kihakiki. Katika Textus Receptus, Yohana 5:4 inasoma, "Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibu maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umampata." Kwa nini mstari huu haupo katika tafsiri ya Biblia ambayo inatumia Nakala ya Uhakiki? Mbinu ya isiofuata mfumo mmoja inafanya kazi kama ifuatavyo: (1) Andiko la Yohana 5:4 haitokei katika nyaraka nyingi za kale zaidi. (2) Andiko la Yohana 5:4 hutokea katika maandiko yote ya Byzantine, lakini sio nyingi za maandishi yasiyo ya mashariki. (3) Inawezekana zaidi kuwa mwandishi angeongeza maelezo zaidi kuliko ilivyo kwamba mwandishi angeondoa maelezo. Yohana 5:4 inafanya wazi zaidi kwa nini mtu aliyepooza alitaka kuingia ndani ya bwawa. Kwa nini mwandishi aondoe mstari huu? Hiyo haina maana. Ina maana kwa kuwa utamaduni wa kwa nini mtu aliyepooza alitaka kuingia ndani ya bwawa ingeongezwa. Kama matokeo ya dhana hizi, Nakala ya Uhakiki/Isiofuata mfumo mmoja haijumuishi Yohana 5:4.

Haijalishi mbinu gani ya uhakiki wa maandishi unaoamini ni sahihi, hii ni suala ambalo linapaswa kujadiliwa kwa neema, heshima, na fadhili. Wakristo wanaweza na hawakubaliani juu ya suala hili. Tunaweza kujadili mbinu, lakini hatupaswi kushambulia motisha na tabia ya wale ambao hatukubaliani nao juu ya suala hili. Sisi sote tuna lengo sawa-kuamua maneno ya awali ya Biblia. Baadhi wana mbinu tofauti tu za kufikia lengo hilo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uhakiki wa maandishi — ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries