settings icon
share icon
Swali

Ufunuo ni nini?

Jibu


Neno "Ufunuo" linatokana na neno la Kigiriki apocalupsis ambalo linamanisha kitabu cha kufunuo, kuweka wazi, au kutoa kifunikacho.” Kitabu cha Ufunuo wakati mwingine hujulikana kama "Ufunuo wa Yohana" kwa sababu Mungu anamfunulia Yohana kuhusu nyakati za mwisho. Zaidi, neno la kiyunani la "ufunuo” ndilo neno la kwanza katika kitabu cha Ufunuo. Kifungu “uandishi wa kimafumbo” limetumika kuelezea utumizi wa ishara, picha na idadi zinazo elezea yatakayo tokea baadaye. Nje ya Ufunuo, mifano ya maandiko ufunuo yako katika Biblia ni Danieli sura 7-12, Isaya sura 24-27, Ezekieli sura 37-4, na Zekaria sura 9-12.

Ni kwa nini maandiko ya Ufunuo yaliandikwa kwa njia ya kimfano na michoro? Vitabu vya ufunuo viliandikwa wakati ilikuwa busara zaidi kwa kuficha ujumbe katika picha na mfano kuliko kutoa ujumbe katika lugha ya wazi. Zaidi ya hayo, mfano uliunda kipengele cha siri juu ya maelezo ya wakati na mahali. Madhumuni ya mfano huo, hata hivyo, hayakuwa yasababishe machafuko, bali kuwafundisha na kuwatia moyo wafuasi wa Mungu katika nyakati ngumu.

Zaidi ya maana hasa ya kibiblia, neno "Ufunuo" mara nyingi hutumiwa kwa kutaja nyakati za mwisho kwa jumla, au matukio ya nyakati za mwisho hasa. Matukio ya nyakati za mwisho kama vile ujio wa pili wa Kristo na vita vya Armagedoni wakati mwingine hujulikana kama Ufunuo. Ufunuo itakuwa kifafanuzi cha mwisho cha Mungu, hasira yake, haki yake, na hatima, upendo wake. Yesu Kristo ndie “Ufunuo” mkuu wa Mungu, vile anavyobaini Mungu kwetu (Yohana 14:9, Waebrania 1:2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufunuo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries