settings icon
share icon
Swali

Ufunuo wa sura ya 12 una maana gani?

Jibu


Katika Ufunuo sura ya 12, Yohana anaona maono ya mwanamke "aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kchwa chake" (Ufunuo 12: 1). Angalia ufanano kati ya maelezo haya na maelezo ambayo Yusufu alitoa kwa baba yake Yakobo (Israeli) na mama yake na watoto wao (Mwanzo 37: 9-11). Nyota kumi na mbili zinarejelea kabila kumi na mbili za Israeli. Hivyo mwanamke katika Ufunuo 12 ni Israeli.

Ushahidi wa ziada kwa tafsiri hii ni kwamba Ufunuo 12: 2-5 inazungumzia mwanamke akiwa na mtoto na kujifungua. Cha kweli ni kwamba Maria alijifungua Yesu, ni kweli pia kwamba Yesu, mwana wa Daudi kutoka kabila la Yuda, alikuja kutoka Israeli. Kwa maana, Israeli ilijifungua-au kumleta-Kristo Yesu. Mstari wa 5 unasema kwamba mtoto wa mwanamke alikuwa "mtoto wa kiume, ambaye atatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma, na mtoto wake alinyakuliwa na Mungu na kuketi kiti chake cha enzi." Kwa wazi, hii inaelezea Yesu. Yesu alipaa mbinguni (Mdo. 1: 9-11) na siku moja ataweka ufalme wake duniani (Ufunuo 20: 4-6), na atautawala kwa hukumu kamilifu ("fimbo ya chuma"; ona Zaburi 2: 7-9).

Kutorokea jangwani kwa mwanamke kwa muda wa siku 1,260 kunahusu wakati wa baadaye unaoitwa Dhiki kuu. Siku elfu moja na mia mbili, na sitini ni miezi 42 (ya siku 30 kila moja), ambayo ni sawa na miaka 3 1/2. Nusu ya kipindi cha dhiki, Mnyama (Mpinga Kristo) ataweka sanamu yake mwenyewe katika hekalu ambalo litajengwa huko Yerusalemu. Hii ni chukizo ambalo Yesu alizungumzia katika Mathayo 24:15 na Marko 13:14. Wakati Mnyama anapofanya hivyo, anavunja mkataba wa amani aliyoifanya na Israeli, na taifa hilo linapaswa kukimbilia usalama wao-labda kwa Petra (pia angalia Mathayo 24; Danieli 9:27). Mwepuko huu wa Wayahudi unatizamiwa kuwa kama ule mwanamke anakimbilia jangwani.

Ufunuo 12: 12-17 inazungumzia jinsi shetani atakavyofanya vita dhidi ya Israeli, akijaribu kumwangamiza (Shetani anajua wakati wake ni mfupi, uzungumzi sawia na huo-ona Ufunuo 20: 1-3, 10). Inafunua pia kwamba Mungu atawalinda Israeli jangwani. Ufunuo 12:14 inasema kuwa Israeli atakingwa kutoka kwa shetani "wakati, nyakati, na nusu wakati (" wakati "= 1 mwaka;" nyakati "= miaka 2;" nusu wakati "= nusu ya mwaka; kwa maneno mengine, ni miaka 3 1/2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufunuo wa sura ya 12 una maana gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries