settings icon
share icon
Swali

Ufalme wa Kirumi uliofufuo ni gani?

Jibu


Neno ufufuo wa ufalme wa Kirumi (ambalo halijatumika katika Biblia) linamaanisha serikali yenye nguvu iliyotabiriwa katika Biblia. Utawala huu utatua mamlakani na kutawala dunia katika nyakati za mwisho. Kulingana na tafsiri mbalimbali za vitabu vya Danieli na Ufunuo, ufufuo wa ufalme wa kirumi ni mfumo wa kisiasa katika ulimwengu wa jumla au taifa maalum chini ya mtawala maalum. Wafasiri mbali mbali wameukita ufalme huu nchini Roma, Uturuki, au Mashariki ya kati.

Ufalme wa kirumi uliofufuliwa kwa kawaida unahusishwa na yule mnyama wa nne katika kitabu cha Danieli mlango wa saba. Mnyama huyu anaelezewa kuwa “mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi” (Danieli 7:7). Mnyama huyu mwenye pembe kumi ni mfano wa kiunabii wa ufalme wa kirumi (Danieli 7:19-24), lakini, Danieli anapotazama, pembe ndogo lijibuka kutoka kwa yule mnyama ikiwa na “Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno” (Danieli 7:8). Pembe hili la mwisho ni mpinga kristo, ambaye kwa namna fulani atahusishwa na ufalme wa kirumi. Tangu karne ya tano ufalme wa kirumi ulikufa na tunatarajia uweze “kufufuliwa” ili utimize unabii wa nyakati za mwisho.

Ufalme wa kirumi uliofufuliwa umehusishwa na ufalme wa tano na wa mwisho ambao umetajwa katika Danieli sura ya pili (Daniel 2:41-43). Maandiko haya yanahusu ndoto ya sanamu ya Nebukadneza iliyotengenezwa na vyuma mbalimbali. Miguu ya chuma inawakilisha ufalme wa kirumi, na nyayo zilizotengenezwa na “chuma nazo sehemu nyingine zilikuwa udongo wa mfinyanzi uliochomwa.” (Danieli 2:33) zinawakilisha ufalme wa mwisho wa kiulimwengu. Kwa vile inashiriki kipengele cha chuma na ufalme wa nne inapendekeza kuwa kuna uhusiano na Rumi, na viganja kumi vinaweza kumaanisha muungano wa mataifa kumi (zinafanana na pembe kumi katika kitabu cha Danieli 7 :20) yakiongozwa kwa pamoja na mtawala mwenye nguvu.

Wafafanuzi wengine huelekeza katika kitabu cha Ufunuo sura ya 13, ambayo inaelezea mnyama anayetoka baharini akiwa na pembe kumi na vichwa saba (Ufunuo 13:1). Taswira hii inaiunganisha na ule mnyama wa nne katika Danieli 7, ambaye pia ako na pembe kumi. Ufunuo unaelezea serikali hii kama ya “kufuru” (Ufunuo 13:1) na ya kudhalimu, ambayo inahitaji utii kamili wa kifedha, kiroho na masuala ya kisiasa (Ufunuo 13:4-8). Nguvu ya kimataifa ambayo taifa hili linamiliki imepeanwa na shetani (Ufunuo 13:2). Kwa muktadha huu, alama hizi utafsiriwa kwa urahisi kama marejeleo ya mtawala maalum na ufalme wa kisiasa maalum ambao bado unakuja, badala ya takwimu Fulani za historia ya hapo awali.

Taswira halisi kuhusu asili ya ufalme wa kirumi uliofufuliwa inaweza kuwa ya kuvutia, lakini tunafaa kukumbuka kuweka mtazamo halisi. Lengo letu la kimsingi kama wakiristo linapaswa kuwa kueneza injili, si kujaribu kutambua wanao mpinga kristo. Hasa, tunafaa kujua kwamba kilichoandikwa kuhusu ufalme wa kirumi uliofufuliwa katika Biblia si pana, na hatuezi enda zaidi ya yaliyoandikwa (1 Wakorintho 4:6). Tunajua mpinga kristo anakuja, na tunajua atakua na uhusiano fulani na ufalme wa kale wa kirumi, haswa kupitia ukoo, jiografia, au mpangilio wa serikali yake. Tunaeza zitambua alama za kale (Mathayo 16:3), lakini hatuezi jua zaidi upana wa mazingira yake.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufalme wa Kirumi uliofufuo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries