settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini ufufuo wa Yesu Kristo ni muhimu?

Jibu


Ufufuo wa Yesu ni muhimu kwa sababu kadhaa. Kwanza, unashahudia nguvu kubwa za Mungu Mwenyewe. Kuamini katika ufufuo ni kuamini katika Mungu. Kama Mungu yupo, na kama Aliumba ulimwengu na ana uwezo juu yake, ana uwezo wa kufufua wafu. Kama yeye hana mamlaka hayo, yeye si Mungu anastahili imani yetu na ibada. Ni Yule tu pekee aliyeumba maisha anaweza kuyafufua baada ya kufa, ni yeye anaweza kubadili njia mbaya ambazo ni mauti, na Yeye tu anaweza kuondoa mwiba wa kifo na kwamba ushindi ambao ni kaburi (1 Wakorintho 15:54-55). Katika kufufua Yesu kutoka kaburini, Mungu anatukumbusha mamlaka yake kamili juu ya maisha na kifo.

Pili, ufufuo wa Yesu ni ushahidi wa ufufuo wa binadamu, ambayo ni ni msingi halisi wa imani ya Kikristo. Tofauti na dini zote, Ukristo peke yake ndio unamiliki mwanzilishi ambaye ipita kifo na ambaye anahadi kwamba wafuasi wake watafanya hivyo. Dini zingine zote zilianzishwa na wanadamu na manabii ambao mwisho ulikuwa kaburini. Kama Wakristo, tunafarijika katika kweli kwamba Mungu wetu akawa mtuwanadamu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka siku ya tatu. Kaburi halikuweza kumshikilia. Anaishi, na Ameketi leo hii upande wa kulia wa Mungu Baba aliye mbinguni.

Katika 1 Wakorintho 15, Paulo anaeleza kwa undani umuhimu wa ufufuo wa Kristo. Baadhi ya wengine Korintho hawakuamini katika ufufuo wa wafu, na katika sura hii Paulo anatoa matokeo sita ya maafa kama hakukuwa na ufufuo: 1) kuhubiri Kristo itakuwa na maana (aya ya. 14), 2) Imani katika Kristo itakuwa haina maana (aya ya. 14), 3) Wote mashahidi na wahubiri wa ufufuo watakuwa waongo (aya ya 15), 4) Hakuna mtu atakombolewa kutoka dhambi (aya ya 17), 5) Waumini wote wa zamani wangeangamia (aya ya 18); na 6) Wakristo watakuwa watu wenye mashaka juu ya nchi (aya ya 19). Lakini Kristo kwa kweli amefufuka kutoka wafu na "amekuwa uzao wa kwanza ya wale waliolala" (mstari 20), kutuhakikishia kuwa sisi tutamfuata katika ufufuo.

Neno lilo na pumzi ya Mungu limuhakikishia muumini ufufuo wakati wa kuja kwake Yesu Kristo kwa ajili ya Mwili wake (Kanisa) katika unyakuo. Tumaini kama hili na uhakika matokeo ya ni katika wimbo mkubwa wa ushindi kama jinsi Paulo anavyo andika katika 1 Wakorintho 15:55, "Ku wapi, ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wakio?"

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini ufufuo wa Yesu Kristo ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries