settings icon
share icon
Swali

Ufufuo wa kwanza ni nini? Ufufuo wa pili ni nini?

Jibu


Danieli 12: 2 inafupisha mafafanuzi mawili tofauti yanayowakabili wanadamu: "Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele." Kila mtu atafufuliwa kutoka wafu, lakini si kila mtu atashiriki hatima hiyo. Agano Jipya linafunua maelezo zaidi ya kufufuka kwa watakatifu na wasio waadilifu.

Ufunuo 20: 4-6 inataja "ufufuo wa kwanza" na hufafanua wale wanaohusika kama "barakiwa na watakatifu." Kifo cha pili (ziwa la moto, Ufunuo 20:14) hakina mamlaka juu ya watu hawa. Ufufuo wa kwanza, basi, ni kufufua waumini wote. Inafanana na mafundisho ya Yesu kuhusu "ufufuo wa wenye haki" (Luka 14:14) na "ufufuo wa uzima" (Yohana 5:29).

Ufufuo wa kwanza unafanyika katika hatua mbalimbali. Yesu Kristo mwenyewe ("mzaliwa wa kwanza," 1 Wakorintho 15:20), aliweka njia ya ufufuo wa wote wanaomwamini. Kulikuwa na ufufuo wa watakatifu wa Yerusalemu (Mathayo 27: 52-53) ambayo inapaswa kuingizwa katika kuzingatia ufufuo wa kwanza. Ufufuo wa "wafu ndani ya Kristo" wakati wa kurudi kwa Bwana (1 Wathesalonike 4:16) na ufufuo wa walio kufa kwa Imani mwishoni mwa dhiki (Ufunuo 20: 4).

Ufunuo 20: 12-13 hufafanua ule unaoambatana na ufufuo wa pili kama hukumu hafifu ya waliohukumiwa na Mungu katika hukumu kuu ya kiti cha enzi nyeupe kabla ya kutupwa katika ziwa la moto. Ufufuo wa pili, basi, ni kuinuliwa kwa wasioamini wote; Ufufuo wa pili unaunganishwa na kifo cha pili. Inafanana na mafundisho ya Yesu kuhusu "ufufuo wa hukumu" (Yohana 5:29).

Tukio ambalo linagawanya ufufuo wa kwanza na wa pili unaonekana kuwa ufalme wa milenia. Wa mwisho wa waadilifu watafufuliwa kutawala "pamoja na Kristo miaka elfu" (Ufunuo 20: 4), lakini "Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu" (Ufunuo 20 : 5).

Je, ni furaha kubwa iliyoje ambayo tutahudhuria ufufuo wa kwanza! Ni kusaga meno kulioje kwa pili! Ni jukumu gani tulio nalo la kueneza Injili! "na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu" (Yuda 23).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufufuo wa kwanza ni nini? Ufufuo wa pili ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries