settings icon
share icon
Swali

Je, ufufuo ni nini kulingana na Biblia?

Jibu


Neno jingine la ufufuo ni kuzaliwa upya, linalohusiana na maneno ya kibiblia "kuzaliwa tena." Kuzaliwa upya kwetu unatofautishwa kutoka kuzaliwa kwetu wa kwanza, wakati tulipata mimba kimwili na kurithi asili yetu ya dhambi. Kuzaliwa upya ni wa kiroho, takatifu, na kuzaliwa wa kimbinguni ambao unasababisha kuwa hai kiroho. Mtu katika hali yake ya asili "amekufa katika makosa na dhambi" hadi "atakapofanywa hai" (fufuliwa) na Kristo. Hii hutokea wakati ataweka imani yake katika Kristo (Waefeso 2:1).

Ufufuo ni kiini cha mabadiliko. Kama vile tu kuzaliwa kwetu wa kimwili ulisababisha mtu mpya kuingia katika ufalme wa ulimwengu, kuzaliwa kwetu wa kiroho husababisha mtu mpya kuingia ufalme wa mbinguni (Waefeso 2:6). Baada ya ufufuo, tunaanza kuona na kusikia na kutafuta vitu vya Mungu; tunaanza kuishi maisha ya imani na utakatifu. Sasa Kristo ameumbwa ndani ya mioyo; sasa sisi ni washiriki wa asili ya kimungu, baada ya kufanywa viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17). Mungu, si mwanadamu, ndiye chanzo cha mabadiliko haya (Waefeso 2:1, 8). Upendo mkubwa wa Mungu na zawadi ya bure, neema yake tajiri na huruma nyingi, ni sababu ya kuzaliwa upya. Nguvu kuu ya Mungu-nguvu iliyomfufua Kristo kutoka kwa wafu-inaonyeshwa katika ufufuo na ubadilishaji wa wenye dhambi (Waefeso 1:19-20).

Ufufuo ni muhimu. Mwili wa wanadamu wenye dhambi hauwezi kusimama mbele ya Mungu. Katika mazungumzo yake na Nikodemo, Yesu alisema mara mbili kwamba mtu lazima azaliwe tena ili aone ufalme wa Mungu (Yohana 3:3, 7). Ufufuo sio kwa hiari, kwa maana "kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni riho" (Yohana 3:6). Kuzaliwa kimwili unatufaa sisi kwa dunia; kuzaliwa tena kiroho unatufaa sisi kwa mbinguni. Angalia Waefeso 2:1; 1 Petro 1:23; Yohana 1:13; 1 Yohana 3:9; 4:7; 5:1, 4, 18.

Ufufuo ni sehemu ya kile ambacho Mungu hutufanyia wakati wa wokovu, pamoja na kuziba (Waefeso 1:14), kuasili (Wagalatia 4:5), upatanisho (2 Wakorintho 5:18-20), nk. Ufufuo ni Mungu kufanya mtu kuwa hai kiroho, kama matokeo ya imani katika Yesu Kristo. Kabla ya wokovu hatukuwa watoto wa Mungu (Yohana 1:12-13); bali, tulikuwa watoto wa ghadhabu (Waefeso 2:3; Warumi 5:18-20). Kabla ya wokovu, tulikuwa tumepotoka; baada ya wokovu tumefufuliwa. Matokeo ya kuzaliwa upya ni amani na Mungu (Warumi 5:1), maisha mapya (Tito 3:5, 2 Wakorintho 5:17), na wana wa milele (Yohana 1:12-13; Wagalatia 3:26). Ufufuo huanza mchakato wa utakaso ambapo tunakuwa watu ambao Mungu anatutaka tuwe (Warumi 8:28-30).

Njia pekee ya kuzaliwa upya ni kwa imani katika kazi iliyokamalika ya Kristo msalabani. Hakuna kiwango cha matendo mema au kutunza Sheria inaweza kufufua moyo. "Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele Zake kwa matendo ya sheria" (Warumi 3:20). Kristo peke yake hutoa tiba kwa uharibifu wa moyo wa mwanadamu. Hatuna haja ya ukarabati au marekebisho au urekebishaji; tunahitaji kuzaliwa tena.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ufufuo ni nini kulingana na Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries