settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya ndoa?

Jibu


Duniani kote, angalau mataifa kumi na saba wamehalalisha ndoa kati ya jinsia moja. Kwa wazi, ufafanuzi wa kijamii wa ndoa unabadilika. Je! ni haki kwaa serikali kutoa ufafanuzi wa ndoa, au ina ufafanuzi wa ndoa tayari umewekwa na mamlaka ya juu?

Katika Mwanzo sura ya 2, Mungu anasema sio vizuri Adamu (mtu wa kwanza) kuishi peke yake. Wanyama wote walikueko, lakini hakuna hata mmoja wao aliweza kuwa mpenzi mzuri kwa Adamu. Kwa hivyo, Mungu, katika tendo maalum la uumbaji, aliumba mwanamke. Vifungu vichache baadaye, mwanamke ameitwa "mkewe" (Mwanzo 2:25). Edeni ilikuwa eneo la ndoa ya kwanza, iliyowekwa na Mungu Mwenyewe. Mwandishi wa Mwanzo ndiye anaandika kiwango ambacho ndoa zote zijazo zimeelezwa: "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" (Mwanzo 2:24).

Kifungu hiki cha Maandiko hutoa hoja kadhaa za kuelewa mpango wa Mungu wa ndoa. Kwanza, ndoa inahusisha mwanamume na mwanamke. Neno la Kiebrania kwa "mke" ni maalum kwa jinsia; haliwezi maanisha kitu chochote isipokuwa "mwanamke." Hakuna kifungu katika Maandiko ambacho kinasema ndoa inahusisha kitu kingine isipokuwa mwanaume na mwanamke. Haitawezekana kwa familia kuunda au uzazi wa binadamu kufanyika mara kwa mara. Kwa vile Mungu alipangia ngono iwe kati ya wanandoa wa ndoa, basi yamaanisha kuwa mpango wa Mungu ni wa kitengo cha familia unapaswa kuundwa wakati mwanamume na mwanamke huja pamoja katika uhusiano wa ngono na kuwa na watoto.

Kanuni ya pili kutoka Mwanzo 2 kuhusu mpango wa Mungu kwa ndoa ni kwamba ndoa inanuiwa kudumu milele yote. Mstari wa 24 unasema hao wawili huwa "mwili mmoja." Hawa alichukuliwa kutoka upafuni mwa Adamu, na hivyo alikuwa halisi mwili mmoja na Adamu. Kila dutu yake ilitolewa kutoka kwa Adamu badala ya udongo. Kwa hivyo kila ndoa inafaa kulenga umoja wa Adamu na Hawa waliokuwa nao. Kwa sababu dhamana yao ilikuwa "katika mwili," walikuwa pamoja milele. Hakuna kifungu cha kutoroka kilichoandikwa katika ndoa ya kwanza ambacho kiliwaruhusu hao wawili kuachana. Hiyo ni kusema kwamba Mungu alinuia ndoa iwe ya milele. Wakati mwanamume na mwanamke wanajitolea kuolewa, "huwa mwili mmoja," wameunganishwa hadi kifo.

Kanuni ya tatu kutoka kifungu hiki kuhusu mpango wa Mungu kwa ndoa ni mke mmoja. Maneno ya Kiebrania kwa "mume" na "mke" ni ya pekee na hairuhusu waume wengi. Ingawa watu wengine katika Maandiko walikuwa na wake wengi, ni wazi kutokana na akaunti ya uumbaji kwamba mpango wa Mungu wa ndoa ulikuwa mume mmoja na mwanamke mmoja. Yesu alisisitiza kanuni hii alipopiga simulizi kwenye akaunti ya Mwanzo ili kukabiliana na wazo la talaka ya urahisi (Mathayo 19: 4-6).

Haipaswi kutushangaza kwamba ulimwengu unataka kutengeneza kile ambacho Mungu ameanzisha. "Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii" (Warumi 8: 7). Ingawa ulimwengu unajaribu kutoa ufafanuzi wao wenyewe kwa kile wanachoita "ndoa," Biblia bado yadumu. Ufafanuzi wa wazi wa ndoa ni muungano wa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja maishani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries