settings icon
share icon
Swali

Je, Utiliteria au (Utiliterianism) ya maanisha nini?

Jibu


Kiini cha Utiliteria au (Utiliterianism) ni dhana yake ya furaha na maumivu. Falsafa ya Utiliteria inaashiria kwamba "kitu kizuri" kama chochote kinachoongeza radhi na kupunguza maumivu. Ni falsafa ya matokeo. Ikiwa matokeo ya kitendo huongeza radhi na kupunguza maumivu, basi hatua hiyo inachukuliwa kuwa nzuri. Kiini cha Utiliteria ni falsafa yake ya Kidedostiki (hedonistic). Historia ya Utiliteria au Utilitarinism iligunduliwa katika enzi zake mwanafalsafa wa kale wa Kigiriki Epicurus lakini Utiliteria haswa kwa mara nyingi huhusishwa mwanafalsafa wa Uingereza Jeremy Bentham, kama mwanzilishi wa fikra hiyo.

Ni matatizo gani yanayoletwa na Utiliteria au Utiliterianism? Kwanza ni mtazamo wake wa kuzingatia matokeo. Kwa kweli, hatua mtu nayochukua si nzuri tu kwa sababu matokeo yake ni mazuri. Biblia inasema kwamba "mwanadamu ana mtazamo wa nje, lakini Bwana Yesu huangalia ndani ya moyo" (Samweli wa kwanza 16: 7). Mungu huwa haangalii sana matokeo kama Yeye anavyozingatia nia za mioyo yetu. Ukitenda mema lakini kwa nia mbaya basi hio haipendezi Mungu. Kwa kuangalia tu, hatuwezi kuona malengo ya wengine. Hatuwezi hata kutambua kabisa makusudi yetu wenyewe. Lakini hiyo sio udhuru; sisi sote tunapaswa kuja mbele ya Mungu na kuchukua jukumu la matendo yetu.

Tatizo la pili na Utiliteria au (Utiliterianism) ni lengo lake la kufurahisha badala ya kuzingatia kile ambacho ni kizuri. Ile haliya kuleta furaha, binadamu anwaez kuitambua kana kwamba ni wema, vile vile inawezakuwa ile hali ya kujipenda yeye mwenyewe. Kinachopendeza au kufurahisha mtu huenda kisifurahishe au kupendeza mwingine . Kulingana na Biblia, Mungu mwenyewe ni ufafanuzi wa mema (Zaburi 86: 5, 119: 68), na kwa kuwa Mungu habadiliki kamwe (Yakobo 1:17), ufafanuzi wa mema haubadiliki basi hakuna ile hali ya kujipenda mwenyewe. Uzuri haubadilika na mwenendo wa tamaa ya kibinadamu au kwa kipindi fulani. Zaidi ya hayo, kwa kulinganisha mema na ridhi, kutakuwepo na hatari ya kufafanua mema kama tu kuridhika kwetu binafsii au tamaa za kimwili. Kama inavyothibitishwa na watu ambao wanajihusisha na maisha ya hedostiki (hedonistic) jinsi mtu anavyofanya kitendo cha kujiridhisha ndivyo anaposhawishika kutenda vitendo zaidi ili kujiridhisha zaidi . Ni sawaa na ile sheria ya kudidimia kwa matokeo. Mfano wa kitendo hiko ni kama vile mtumiaji wa madawa ya kulevya hujaribu madawa ya kulevya yenye nguvu zaidi ili kujiridhisha zaidi.

Tatizo la tatu la Utiliteria au (Utiliterianism) ni kuepuka maumivu. Sio maumivu yote yaliyo mabaya. Sio kwamba maumivu ni mazuri, lakini yanaweza kusababisha mema. Kihistoria, binadamu wamejifunza mengi kupitia kufanya makosa. Wengi wanasema, ile hali ya kushindwa ni mwalimu bora. Hatusemi kwamba tunapaswa kujiingiza kwa mambo yanayoleta maumivu lakini viyo hivo hatuwezifunga macho na tuseme maumivu yote ni mabaya na yanapaswa kuepukwa . Mungu ana hamu zaidi katika utakatifu wetu kuliko furaha yetu. Ushauri wake kwa watu wake ni kuwa watakatifu kama Yeye alivyo Mtakatifu (Mambo ya Walawi 11:44, 1 Petro 1: 15-16). Biblia pia inasema kwamba tunapaswa kuhesabu kama furaha tunapokabiliwa na majaribio ya aina yoyote (Yakobo 1: 2-4), sio kwa sababu majaribio yanafurahisha, lakini kwa sababu husababisha uvumilivu mkubwa na uaminifu.

Falsafa ya Utalitaria au (Utiliterianism) inalenga kufanya maisha kuwa bila maumivu kama iwezekanavyo na kwa watu wengi iwezekanavyo. Bila kuchunguza zaidi , hiyo inaonekana kama lengo la kupendeza. Nani asiyependa kuondokana na mateso ya watu ulimwenguni pote? Hata hivyo Biblia inatuambia kwamba kuna mengi ya kufanya kuliko tu kuishi kwetu humu duniani. Ikiwa tunaishi ile kujiridhisha au kijifurahisha sisi wenyewe basi, tunakosa mtazamo mkubwa wa maisha. Yesu alisema kuwa yeye anayeishi kwa ajili ya uhai huu atakosa furaha halisi (Mathayo 6:19). Mtume Paulo anasema matatizo ya maisha haya hayatalinganishwa na utukufu tutakaopokea milele (Wakorintho wa pili 4:17). Mambo ya maisha haya ni ya muda mfupi tu. (mstari wa 18). Lengo letu linapaswa kuwa la kuongeza utukufu wetu mbinguni, sio maisha yetu humu duniani.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Utiliteria au (Utiliterianism) ya maanisha nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries