settings icon
share icon
Swali

Je! ufafanuzi wa eklesia ni gani?

Jibu


Kuelewa tafsiri ya eklesia ni kiungo muhimu cha kuelewa kanisa. Eklesia ni neno la Kiyunani linalofafanuliwa kama "kusanyiko lililoitwa au mkutano." Eklesia mara nyingi hutafsiriwa kama "kanisa" katika Agano Jipya. Kwa mfano, Matendo 11:26 inasema kwamba "Barnaba na Sauli wakakutana na kanisa [ekklesia]" huko Antiokia. Na katika 1 Wakorintho 15: 9 Paulo anasema kwamba alikuwa amelitesa kanisa [eklesia] la Mungu." "Kusanyiko lililoitwa," basi, ni mkutano wa waumini ambao Mungu amewaita kutoka ulimwenguni na "kuingia katika nuru yake ya ajabu" (1 Petro 2: 9).

Neno hilo katika Agano Jipya pia lilitumiwa kurejelea mkutano wowote wa watu. Katika hotuba yake kwa Baraza la wazee, Stefano anawaita watu wa Israeli "mkutano [eklesia] jangwani" (Mdo. 7:38). Na katika Matendo 19:39, neno eklesia linarejelea mkutano wa raia unaojadili mambo ya kisheria. Walakini, katika muktadha mwingi, neno eklesia hutumiwa kurejelea watu ambao wanaojumuisha kanisa la Agano Jipya.

Ni muhimu kwamba kanisa hii leo lielewa tafsiri ya eklesia. Kanisa linapaswa kujiona kuwa "limeitwa" na Mungu. Ikiwa kanisa linataka kuleta mabadiliko ulimwenguni, lazima liwe tofauti na ulimwengu. Chumvi ni tofauti na chakula inachotia ladha. Mungu ameliita kanisa kujitenga na dhambi (1 Petro 1:16), kukumbatia ushirika na waumini wengine (Matendo 2:42), na kuwa nuru kwa ulimwengu (Mathayo 5:14). Mungu kwa neema ametuita kwake mwenyewe: "'Kwa hiyo tokeni miongoni mwao, mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kitu chochote kilicho najisi, nami nitawakaribisha'" (2 Wakorintho 6:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! ufafanuzi wa eklesia ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries