settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inadhibiiti fikra?

Jibu


Watu wengine wanawashutumu Wakristo wa kutumia Biblia kama chombo cha kudhibiti akili. Wanadai kwamba njia pekee ya kujenga kanisa na kudumisha wanachama, ni kutumia mbinu za kuchanganya akili ili kuwashawishi watu katika maisha na mabadiliko ya tabia. Madai haya hayana msingi, lakini wale ambao hawajui uwezo wa Roho Mtakatifu wanahitaji njia ya kuelezea mabadiliko katika maisha ya watu.

Ingawa ni kweli kwamba ibada za uongo ambazo hudai kuwa Wakristo hufanya mazoezi ya udhibiti wa akili, Ukristo wa kweli haulazimishi mtu kwa njia yoyote. Wachungaji wanaompenda Bwana wanataka kulisha, kuimarisha, na kulinda makutaniko yao (Yohana 21: 15-19). Viongozi wa kanisa wanfaa kutumikia wengine bila kujipenda wenyewe na kwa unyenyekevu, bila mawazo ya faida binafsi (1 Petro 5: 2-3). Kwa hiyo, Biblia haidhibiti akili, na haitetei udhibiti wa akili kwa lengo la ubongoji wa akili au programu ya kisaikolojia.

Hata hivyo, Biblia inazungumzia kuhusu kudhibiti mtazamo wa mtu. Toba inahusisha mabadiliko ya akili. Wakristo "hufanywa wapya katika mtazamo wa akili zao" (Waefeso 4:23). Wanapaswa kuwa na mtazamo sawa, ili kuepuka ugomvi (Wafilipi 2: 2). Wamepewa akili ya Kristo (1 Wakorintho 2:16). Matokeo yake ni mtazamo mpya na tabia mpya — kiumbe kipya, kwa kweli (2 Wakorintho 5:17). Mabadiliko hayafanyiki kwa sababu ya udanganyifu au mazingira ya uangalifu; mabadiliko ni ya ndani, ya kiroho, na ya kweli. Ni kutokana na kazi ya Roho Mtakatifu, sio wakala wa kibinadamu (Tito 3: 5).

Binadamu ana asili ya dhambi inayotokana na Adamu (Warumi 5:12). Hali hiyo ya dhambi hushawishi mtu na husababisha dhambi mbalimbali kujionyesha katika maisha ya mtu (Wagalatia 5: 17-21; Waefeso 5: 17-19). Akiongozwa na asili hiyo ya dhambi, mtu hawezi kumjua Mungu na kumpendeza Mungu. Kwa kweli, yeye ni adui wa Mungu (Warumi 5:10; 8: 5-7). Biblia inasema kwamba mwenye dhambi, anayeongozwa na asili yake ya dhambi, anahitaji asili mpya na ukombozi kutoka kwa nguvu za dhambi. Mtu anayekubali Yesu Kristo kama Mwokozi binafsi anapata ile asili mpya (2 Petro 1: 4) na Roho Mtakatifu anapata kuingia ndani yake, ambaye huwapa waumini nguvu ya kuasi dhambi na kukubali uadilifu wa Mungu (Wagalatia 5:16; Warumi 6: 12-23). Muumini katika Kristo amewekwa huru (Yohana 8:32). Yeye hapaswi kutii maagizo ya asili ya dhambi tena, kwa kuwa ana uhuru katika Kristo kufanya kile Mungu anataka na kumtukuza katika Maisha yake.

Biblia haidhibiti akili. Badala yake, Biblia hutoa njia mbadala kwa maisha yanayoongozwa na dhambi. Biblia inatuonyesha jinsi ya kuongozwa na Roho. Ndiyo, mwamini atakuwa na mabadiliko ya akili, anapoasi uongo alioamini hapo awali na kukubali ukweli katika Kristo. Mwaminifu aliyejawa na Roho atakuwa na maisha ya furaha na Mungu. Atakua na uhuru wa maisha kumtumikia Mungu kwa shauku, utimilifu wa milele, na matumaini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inadhibiiti fikra?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries