settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu uovu?

Jibu


Biblia ina mengi ya kusema kuhusu mada ya udhalimu. Tunajua kwamba Mungu anapenda haki; tunajua kwamba Yeye hapendi udhalimu, hata kidogo. Mwandishi wa Mithali anasema hivi: "Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa Bwana; Tena mizani ya hila si njema." (Methali 20:23). Haki ni msingi kwa kiti cha enzi cha Mungu (Zaburi 89:14), na Mungu hakubali ubaguzi, ikiwa tunazungumzia juu ya mizani ya hila au mfumo wa kisheria ambao una udhalimu. (Mambo ya Walawi 19:15; Yakobo 2: 8-9). Kuna vifungu vingine vingi, katika Agano la Kale na Jipya, ambavyo vinatueleza jinsi Mungu anachukia udhalimu. (2 Mambo ya Nyakati 19: 7, Ayubu 6:29, 11:14, Mithali 16: 8; Ezekieli 18:24; 9:14).

Isaya aliishi wakati ambapo Yuda alikuwa akijitahidi chini ya uzito wa udhalimu: "Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia. Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye Bwana akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki."(Isaya 59: 14-15). Ujumbe wa Mungu kwao ulikuwa rahisi: "Jifunze kufanya haki; kutafuta haki. / Kutetea waliokandamizwa. / mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane."(Isaya 1:17). Baadaye, Mungu anawaambia "Kuzilegeza kamba za nira" (Isaya 58: 6, tazama Zaburi 82: 3), kuonyesha kwamba ukosefu wa haki ni aina ya utumwa na ukandamizaji.

Katika kitabu cha Yakobo, tunaona zaidi ndani ya moyo wa Mungu kuhusu udhalimu. Mungu anaichukulia jamb hili kwa uzito. Hatojali haki tu kwa ajili ya kuwa na utaratibu. Kuna masuala ya kina. Katika Yakobo 2, tunaona majadiliano juu ya ubaguzi. Yakobo anazungumza na kundi la waumini ambao wamewahukumu watu katika mkusanyiko wao kulingana na hali yao ya kijamii. Katika moyo wa mwanadamu, udhalimu ni ishara ya ubaguzi, hukumu, na ukosefu wa upendo. Tunapojitahidi kuwa wenye haki kwa kipimo chetu cha kibinadamu, sisi daima tunasahau kipimo cha Mungu: ukamilifu. Kwa Mungu, Kitu chochote chini ya ukamilifu ni mizani hila.

Kila mwanadamu ni asiye na haki, kwa sababu ya kuanguka. Tunafanya vitu vingi mbaya. Tunafanya makosa, tunafanya na kusema vitu ambazo ni kinyume kabisa. Kama Yakobo anasema, "Sisi sote tunajikwaa kwa njia nyingi" (Yakobo 3: 2). Ukosefu wa haki huingilia maisha yetu, tunapohukumu wengine na kuwapa kiwango tofauti ambacho sisi hatuwezi kukifikia.

Njia pekee ya kuepuka udhalimu ni kukubali kwanza kwamba Mungu ni mwenye haki kabisa na wanadamu ni wadhalimu kwa asili, yaani, sio kamilifu, na kisha kukubali haki ya Mungu (1 Yohana 1: 5-9). Pindi tunapopata kutojali kujifanya tuwe wenye haki tunaweza kumtegemea Yeye anayewahesabia wasiomcha Mungu (Waroma 4: 5). Kisha, kama watoto wa Mungu, tunaweza kuona wazi kupambana na udhalimu karibu nasi kwa mtazamo wa huruma (Mika 6: 8; Yakobo 1:27).

Jesus is totally just; there is no injustice in Him at all. Because of His perfection, Jesus can provide true justice. In fact, "the Father judges no one, but has entrusted all judgment to the Son" (John 5:22). We look forward to the time when righteousness and justice will be the order of the day and injustice will be banished forever: "Of the greatness of his government and peace there will be no end. He will reign on David's throne and over his kingdom, establishing and upholding it with justice and righteousness from that time on and forever. The zeal of the LORD Almighty will accomplish this" (Isaiah 9:7).

Yesu ni mwenye haki kabisa; hakuna udhalimu ndani yake. Kwa sababu ya ukamilifu wake, Yesu anaweza kutoa haki ya kweli. Kwa kweli, "Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote" (Yohana 5:22). Tunatarajia wakati ambapo uadilifu na haki zitakuwa utaratibu wa kila siku na udhalimu utaisha milele: "Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo."(Isaya 9: 7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu uovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries