settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anaenda kutuma udanganyifu mkubwa katika nyakati za mwisho?

Jibu


Biblia inaweka wazi ni kwa nini Mungu anatuma udanganyifu mkubwa katika nyakati za mwisho: “na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.

” (2 Wathesalonike 2:10-12). Iseme kwa urahisi, Mungu anatuma udanganyifu mkubwa kwa wale ambao wanachagua kutoamini injili ya Kristo. Wale wanafurahia katika kumkejeli na kumkataa Yeye, Yeye atawahukumu.

Ni chaguo la mtu binafsi ikiwa atakubali na kuamini ukweli wa Yesu Kristo vile umetolewa katika Maandiko. Kupokea ukweli na upendo Mungu anatoa huko katika kufuata mafudisho yake, “Huku ndiko kumpenda Mungu, yaani, kuzitii amri zake. Nazo amri zake si nzito” (1 Yohana 5:3). Kinyume chake, kujua ukweli na kutotii ni kupata ghadhabu ya Mungu: “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu” (Warumi 1: 18). Kusema ukweli, hakuna hali hatari kubwa zaidi kwa binadamu kujua ukweli na kukataa kuufuata. Kwa kufanya hivyo ni kuufanya moyo kuwa ngumu na kuhakikisha hukumu ya Mungu.

Wakati mtu anajua ukweli na kukataa kuutii, yeye ni somo kwa uongo wowote, udanganyifu wowote, kutokuwa na ukweli wowote ambao mtu anaeza buni. “Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga” (Warumi 1:21-22). Paulo anaendelea kuelezea katika vifungo vichache vivyatavyo kuhusu mawazo na tabia za wale hawaamini (ona Warumi 1:29-31). Kwa sababu ya upumbafu na majivuno ya dharau ya binadamu kwa vitu vya Mungu, “Nao kwa kuwa hawakuona umuhimu wa kudumisha ufahamu wa Mungu, yeye akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa” (Warumi 1:28). Sambamba, “Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda” (Warumi 1:32).

Isaya anaiweka Dhahiri na kwa ufupi: “Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu,na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali, nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa. Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu, niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza. Walifanya maovu machoni pangu na kuchagua lile linalonichukiza” (Isaya 66:3-4).

Wakati watu wanajua ukweli na wanakataa kuupokea, wanapokataa kuutii na kuushikilia kwa njia zisizo aadilifu, “na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.” (2 Wathesalonike 2:12).

“Upendo wa Mungu” (1Yohana 4:16). Yeye sio zimwi katili ambaye kimakusudi na kwa ndani anafurahia katika kutayarisha watu kwa hukumu ya milele. Bali Yeye anatangaza kwa bidii na kwa upendo injili ya Kristo, “maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba” (2 Petro 3:9).

Katika maandiko yote, Mungu anahimiza watu kukubali ukweli. Lakini watu wanapomkataa na kudharau ujumbe Wake, basi—na sio hadi wakati huo—Mungu anawafanya wagumu na kuwageuza kuwa na akili danganyifu ili waanguke katika uovu kwa laana yao ya milele. Hili ndilo Bwana anasema kuhusu wale ambao wanachagua kukataa ukweli: “Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa: “Wanapenda sana kutangatanga, hawaizuii miguu yao. Hivyo Bwana hawakubali;sasa ataukumbuka uovu wao na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao” (Yeremia 14:10).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anaenda kutuma udanganyifu mkubwa katika nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries