settings icon
share icon
Swali

Kwa nini ubinadamu wa Yesu ni muhimu?

Jibu


Ubinadamu wa Yesu ni wa umuhimu sawia na uungu wa Yesu. Yesu alizaliwa kama mwanadamu huku bado akiwa Mungu. Dhana ya ubinadamu wa Yesu iliyopo na Uungu Wake ni vigumu kwa akili ya mwanadamu iliyo mwisho. Hata hivyo, asili ya Yesu-mwanadamu halisi na Mungu kabisa -ni ukweli wa kibiblia. Kuna wale wanaokataa ukweli huu wa Biblia na kutangaza kwamba Yesu alikuwa mwanadamuw, lakini si Mungu (Ebionism). Docetism ni mtazamo kwamba Yesu alikuwa Mungu, lakini sio binadamu. Mitazamo yote miwili sio ya kibiblia na ni ya uwongo.

Yesu alilazimika kuzaliwa kama mwanadamu kwa sababu kadhaa. Moja ni ilivyoelezwa katika Wagalatia 4: 4-5: "Lakini wakati ule maalumu ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke, akaishi chini ya sharia, apate kuwa kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sharia ili sisi tufanyewe wana wa Mungu." Mwanadamu peke yake ndiye anaweza "kuzaliwa chini ya sheria." Hakuna mnyama au malaika aliye "chini ya sheria." Wanadamu pekee ndio wazaliwa chini ya sheria, na ni mwanadamu peke yake anaweza kuwakomboa wanadamu wengine waliozaliwa chini ya sheria hiyo. Alizaliwa chini ya sheria ya Mungu, wanadamu wote wana hatia ya kupinga sheria hiyo. Mwanadamu mkamilifu-Yesu Kristo-ndiye angeweza pekee kushika sheria kikamilifu na kuitimiza kikamilifu sharia hiyo, na hivyo kutukomboa sisi kutokana na hatia hiyo. Yesu alitimiza ukombozi wetu msalabani, akibadili dhambi zetu kwa haki yake kamilifu (2 Wakorintho 5:21).

Sababu nyingine Yesu alipaswa kuwa binadamu kikamilifu ni kwamba Mungu aliweka umuhimu wa kumwaga damu kwa msamaha wa dhambi (Mambo ya Walawi 17:11; Waebrania 9:22). Damu ya wanyama, ingawa ilikubalika kwa muda mfupi na kama kivuli cha damu ya Mungu-Mwanadamu mkamilifu, haikutosha nay a kudumu kwa ondoleo la dhambi kwa sababu "Maana damu ya fahli na mbuzi hiwezi kamwe kuondoa dhambi" ( Waebrania 10: 4). Yesu Kristo, Mwana-Kondoo mkamilifu wa Mungu, alitoa dhabihu maisha yake ya kibinadamu na kumwaga damu Yake ya kibinadamu ili kufunika dhambi za wote ambao wangeweza kumwamini Yeye. Ikiwa hakuwa mwanadamu, basi hii haingewezekana.

Zaidi ya hayo, ubinadamu wa Yesu humwezesha kuzungumza na sisi kwa njia ambayo malaika au wanyama hawawezi kamwe. "Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi" (Waebrania 4:15). Ni mwanadamu pekee angeweza kuhurumia udhaifu wetu na majaribu. Katika ubinadamu wake, Yesu alikuwa chini kila aina ya majaribio ambayo sisi hupata, na Yeye, kwa hiyo, anaweza kutuhurumia na kutusaidia. Alijaribiwa; Alizunzwa; Alikuwa maskini; Alidharauliwa; Alipata maumivu ya kimwili; na alivumilia huzuni za kifo cha ukali na cha ukatili. Ni mwanadamu pekee anayeweza kuhisi mambo haya, na mwanadamu pekee ndiye anaweza kuyaelewa kikamilifu kupitia uzoefu.

Mwisho, ilikuwa ni lazima kwa Yesu kuja katika mwili kwa sababu kuamini kwamba ukweli ni sharti la wokovu. Kutangaza kwamba Yesu amekuja katika mwili ni alama ya roho kutoka kwa Mungu, wakati Mpinga Kristo na wote wanaomfuata wanakataa (1 Yohana 4: 2-3). Yesu amekuja katika mwili; Anaweza kuhurumia udhaifu wetu wa kibinadamu; Damu yake ya kibinadamu ilimwagika kwa ajili ya dhambi zetu; na alikuwa kikamilifu Mungu na kikamilifu Mwanadamu. Hizi ni kweli za Biblia ambao haziwezi kukataliwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini ubinadamu wa Yesu ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries