settings icon
share icon
Swali

Je, Bibilia inafundisha ubatizo wa muumini/Imani ya ubatizo?

Jibu


Ubatizo umekuwa suala la mjadala ndani ya miduara ya Kikristo kwa miaka mingi. Kwa kweli, tayari ilikuwa suala katika kanisa la kwanza. Paulo aliizungumzia katika 1 Wakorintho 1:13-16. Wakorintho walikuwa wakijisifu juu ya mtume ambaye alikuwa amewabatiza, akibishana juu ya ubatizo wa nani ulikuwa bora zaidi. Paulo aliwakemea kwa ufuasi wao wa madhehebu na kuhitimisha na, "maana Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri injili." Kwa maneno haya ni wazi kwamba kuna tofauti kati ya kupokea Injili na kitendo cha ubatizo. Zinahusina lakini si sawa kwa umuhimu.

Kulingana na wingi wa Maandiko, ubatizo wa maji ni hatua muhimu ya kwanza katika kumfuata Yesu kama Bwana. Yesu alibatizwa (Mathayo 3:16; Luka 3:21) na aliwaambia wale waliokiri jina Lake kufuata mfano Wake kama ushahidi kwamba mioyo yao imebadilika (Matendo 8:16; 19:5). Ubatizo wa muumini ni tendo ambalo muumini katika Yesu Kristo anachagua kubatizwa ili kutoa ushuhuda wa imani yake. Ubatizo wa muumini pia huitwa "Imani ya ubatizo," neno linalotokana na neno la Kilatini kwa "imani," kuonyesha kwamba ubatizo ni ishara ya mtu kuchukua kanuni fulani au imani.

Ubatizo wa muumini unafundishwa wazi katika Matendo 2. Katika sura hii, Petro anahubiri ujumbe wa injili siku ya Pentekoste huko Yerusalemu. Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Petro alitangaza kwa ujasiri kifo na ufufuo wa Yesu na kuwaamuru watu wapate kutubu na kuamini katika Kristo (Matendo 2:36, 38). Jibu la uwasilishaji wa injili ya Petro limenakiliwa katika mstari wa 41: "Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa." Angalia utaratibu wa matukio-walikubali ujumbe (Injili ya Kristo), na kisha wakabatizwa. Ni wale tu walioamini walibatizwa. Tunaona utaratibu sawa katika Matendo ya 16, wakati mlinzi wa gereza wa Filipi na familia yake wanaokolewa. Wanaamini, na kisha wanabatizwa (Mdo. 16:29-34). Kazi ya mitume ilikuwa kubatiza waumini, sio wasioamini.

Ubatizo wa muumini unatofautishwa kutoka kwa ubatizo wa mtoto mchanga kwa kuwa mtoto mchanga, ambaye hana ufahamu wa injili, hawezi kuwa "muumini" katika Kristo. Ubatizo wa Muumini unahusisha mtu anayeisikia injili, kumkubali Kristo kama Mwokozi, na kuchagua kubatizwa. Ni uchaguzi wake. Katika ubatizo wa mtoto mchanga, uchaguzi hufanywa na mtu mwingine, si mtoto anayebatizwa. Wale ambao hubatiza watoto mara nyingi hufundisha kwamba ubatizo wa maji ni njia ambayo Roho Mtakatifu hupewa kwa mtu binafsi. Wanaweka wazo hili hasa juu ya maneno ya Petro katika Matendo 2:38: "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu." Wale wanaoshikilia mafundisho haya wanaamini kuwa kitendo cha kubatiza mtoto mchanga huweka mtoto huru na kupata wokovu. Hakuna mahali katika Maandiko mazoezi ya ubatizo wa watoto wachanga unadokezwa hata. Baadhi wanaelezea marejeleo machache ya mitume kubatiza "kaya" (Mdo. 11:14; 16:15, 33), kwa kudhani kwamba kaya zilijumuisha watoto wachanga, lakini hii inaenda zaidi ya yale maandiko yasema.

Katika Agano Jipya, ubatizo wa maji ulikuwa matokeo ya asili ya imani ya kuokoa na kujitolea kwa Yesu kama Mwokozi na Bwana (Matendo 2:42; 8:35-37). Kwa vile watoto wachanga na watoto wadogo hawawezi kufanya uamuzi sahihi wa kumkiri Yesu kama Bwana, ubatizo wao hauna umuhimu wa kiroho. Ikiwa ubatizo wa mtoto mchanga unamfanya mtoto kuwa haki na Mungu, basi watoto tu ambao wazazi wao walioupenda "wataokolewa." Wale ambao hawakuwa na wazazi waaminifu watahukumiwa kama watoto wachanga, wazo ambalo halina msingi wa kibiblia. Maandiko ni wazi kwamba Mungu anahukumu moyo wa kila mtu na kuhukunu au kuzawadi kila mmoja kulingana na maamuzi yaliyotolewa na mtu huyo, si kwa wazazi wake (Warumi 2:5-6, Yeremia 17:10; Mathayo 16:27; 2 Wakorintho 5:10).

Wengine hufundisha kwamba ubatizo wa maji ni mahitaji ya wokovu, sawa na toba na kukiri ya Yesu kama Bwana (Waruma 10:8-9). Wakati mifano ya kibiblia inaonyesha kwamba ubatizo kwa kawaida ulifuata ubadilishaji, hakuna mahali ambapo Yesu alifundisha kwamba ubatizo ungeweza kumwokoa mtu yeyote. Katika Pasaka, alisema, "kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi" (Mathayo 26:28). Imani katika nguvu ya damu Yake iliyomwagika ni yote ambayo inahitajika kufanya wenye dhambi wenye hatia sawa na Mungu. Warumi 5:8-9 inasema, "Bali Mungu aonyesha pendo lake mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi Zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye."

Ikiwa ubatizo ulihitajika kwa kuingia katika uzima wa milele, basi Yesu alikuwa na makosa kusema kwa mwizi kwenye msalaba, "Leo hivi utakuwa pamoja nami Paradiso" (Luka 23:43). Mwizi hakuwa na nafasi ya kubatizwa kabla ya kukabiliana na Mungu. Alitangazwa kuwa mwenye haki kwa sababu aliweka imani yake katika kile ambacho Mwana wa Mungu alikuwa akifanya kwa niaba yake (Yohana 3:16, Warumi 5:1; Wagalatia 5:4). Wagalatia 2:16 inafafanua ukweli kwamba hakuna chochote tunachoweza kuongeza au kutoa kutoka kwa kazi iliyokamilika ya Kristo kwa niaba yetu, ikiwa ni pamoja na ubatizo: "hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa Imani ya Yesu Kristo; sisi tulimwamini Kristo Yesu hili tuhesabiwe haki kwa Imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki."

Ubatizo wa maji ni hatua ya kwanza muhimu ya utii katika kumfuata Kristo. Waumini wanapaswa kubatizwa. Lakini, ubatizo ni matokeo ya wokovu sio mchangiaji wa wakovu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Bibilia inafundisha ubatizo wa muumini/Imani ya ubatizo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries