settings icon
share icon
Swali

Je, uavyaji mimba na uuaji?

Jibu


Suala la uavyaji mimba ni mojawapo ya masuala yenye huibua hisia kali sana katika siku zetu. Kupata jibu la uaminifu kwa swali hili "uavyaji mimba ni mauaji?" Inahitaji ujasiri kwa wale ambao wamefanya kitendo cha kuavhya au wao wenyewe wameavya mimba. Biblia ii wazi juu ya ukweli kwamba mauaji ni dhambi (Kutoka 20:13). Hata hivyo, wakati mwingine, Biblia haipingi mauaji. Askari wanaowakilisha nchi yao walitarajiwa kuua askari upande wa kupinga (Yoshua 11:20). Hiyo siyo mauaji. Wanyama waliuliwa kwa ajili ya chakula na kwa dhabihu (Kutoka 24: 5; Mwanzo 9: 3-4). Hiyo sio mauaji vile vile.

Mauaji hufafanuliwa kama "mauaji yasiyo ya kisheria, yaliyo pangwa na mtu mmoja ili amue mwingine." Mauaji ni ukiukaji wa sheria — yaani, kuua ambako kwamba kunafanyika kwa hukumu ya mtu mmoja dhidi ya mwingine, kwa sababu binafsi (badala ya kitaifa). Biblia inakataa kuua mara kwa mara kama tabia ya jamii iliyooza (Kumbukumbu la Torati 5:17; Isaya 1:21; Hosea 4: 2; Mathayo 5:21). Kuamua kama utoaji mimba ni uuaji unahusisha mambo mawili: kwanza, ikiwa kichusi katika utumbo ni mwanadamu, na pili, kama kichusi ni mtoto, ikiwa ni mimba au si mimba inaweza kuitwa kwa hakika kuwa ni kisheria katika nchi nyingi. Ikiwa mauaji ni ukiukaji wa sheria, basi itakua kwamba mauaji kwa mjibu wa sharia hayatakuwa mauaji.

Sababu moja ya mauaji yamepigwa marufuku katika maeneo mengi ni kwamba si halali kwa mtu mmoja kuamua moja kwa moja hatima ya mwingine. Chini ya Sheria ya Agano la Kale, mwuaji hakuuawa isipokuwa kuna mashahidi wa wengi: "Mtu awaye yote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu hata akafa" (Hesabu 35:30). Katika vita, askari hawaamui kuua kwa madhumuni yao wenyewe; badala, wao huua kwa maslahi ya kitaifa — kama wanapigana kwa taifa lao wanaoliheshimu, lengo lao ni kwa madhumuni ya kukinga kitaifa na raia wasio na hatia kutokana na tishio fulani. Mimba ni tofauti. Uavyaji mimba ni kuua kwa kuzingatia hukumu ya mama na uamuzi mmoja. Uuaji huo wa kiumbe kisicho weza kujitetea si wa heshima na unapaswa kufafanua uavyaji mimba kama mauaji katika jamii yoyote — isipokuwa kama kichusi sio binadamu. Ikiwa kichusi ni wingi wa tishu zisizo na binafsi au kitu kidogo chini ya binadamu, kutamatisha maisha yake hakuwezi kukabiliana na changamoto sawia ya kimaadili na haipaswi chukuliwa kuwa mauaji.

Hivyo, kichusi ni binadamu? Au ni kitu kingine? Akizungumza kimwili, maisha ya mwanadamu huanza wakati wa ushikaji mimba. Wakati yai la mama na manii ya baba huja pamoja, huchanganya na kujenga chembe mpya ya DNA ambayo ni ya kibinafsi na ya kipekee kabisa. DNA ni lugha fiche, mpango wa ukuaji wa binadamu mpya na maendeleo. Hakuna tena vifaa vya maumbile vinavyohitajika kuongezwa; kichusi ndani ya tumbo ni kama binadamu kama mama ambaye amembeba kwa tumbo lake. Tofauti kati ya kichusi na yeyote kati yetu ni moja, umri, eneo, na kiwango cha utegemezi. Wakati mama anakatiza mchakato wa ukuaji wa kichusi, anaharibu maisha ya kipekee.

Biblia inaelezea wazi kwamba mimba ni mwanzo wa maisha ya mwanadamu. Samsoni akasema, "Mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu" (Waamuzi 16:17). Anaelezea ubinafsi wake kabla hajazaliwa kama tayari kuwa kile ambacho Mungu alimpangia kuwa yeye ni Mnadhiri. Daudi anasema, "Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu" (Zaburi 139: 13). Tena, tunamwona Daudi akijirejelea mwenyewe kama mtu hata akiwa tumboni. Kisha, anasema, "Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado" (Zaburi 139: 16). Daudi anasema kwamba Mungu alikuwa na siku zake zote zilizopangwa kwa ajili yake wakati alikuwa bado tumboni. Tena, ushahidi huu unaonyesha kuwa mtu huanza wakati mimba ishatiwa, badala ya wakati wa kuzaliwa. Tunamwona Mungu alikuwa na mpango sawia wa maisha ya Yeremia aliyezaliwa kabla: "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa" (Yeremia 1: 5).

Biblia inachukulia kichusi mtoto ambaye hajazaliwa, mwanadamu aliyepangiwa ambaye Mungu anamuumba tangu wakati wa kushika. Hii ikiwa hali, haijalishi ni nini sheria ya binadamu inasema au jinsi uavyaji mimba umekubalika kijamii au wa kisiasa. Sheria ya Mungu inazipita zote. Mama ambaye anaamua kuavya mtoto wake anafanya uamuzi wa kumaliza maisha ya mtu mwingine — na hiyo ndiyo imekuwa daima ufafanuzi wa mauaji.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, uavyaji mimba na uuaji?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries