Swali
Je! Wazo la uasilia wa ulimwengu ni la Kibiblia?
Jibu
Marejeo ya awali na yakuaminika sana kwa uasilia wa ulimwengu inapatikana katika maandishi ya Kigiriki ya Mycenaean ya mwaka wa 12 au 13 BC. Neno uasilia wa Dunia hutafsiriwa kama "ma-ga" au "Mama Gaia." Nadharia hii ilikuwa na mizizi katika falsafa za kabla ya Sokrasia ambao "walizindua" ulimwengu na pia ilitetewa na Aristotle ambaye alikuwa mwanafalsafa wa Kigiriki. Tamaduni zingine zimekubali wazo la kwamba "ulimwengu" ilikuwa na roho na uwazi wake pekee kutoka kwa Mungu Baba. Tamaduni ya Wahindi wa asili ya Marekani ni moja ambayo inaamini kwamba kuna kitu kinachoitwa "uasilia wa ulimwengu" kinachotupa maji ya uzima ambayo husababisha ukuzaji wa chakula. Kwa kweli, hakuna mtu mwingine ila tu Mungu hutoa mahitaji yetu ya msingi ya chakula, makao, maji, na maisha.
Maneno 'Uasilia wa ulimwengu' wakati mwingine hutumiwa kwa ujumla kuzungumzia mazingira kwa ujumla. Wakati mwingine hutumiwa kwa kushirikiana na itikadi za kisiasa na za kiutamaduni kama vile ongezeko la nyusi, mazingira, na mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa baadhi ya wengine, ripoti za habari za kupanda kwa joto, kuongezeka kwa viwango vya baharini, mavumbi ya ardhi, mitetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, kuongezeka kwa magonjwa mapya na hata ya kale, na kama vile huonyesha kwamba "uasili wa ulimwengu" ni aina ya miungu kigeugeu ambayo huharibu dunia.
Ni Mungu anayedhibiti nguvu za ulimwengu: "Ameiumba dunia kwa uwezo wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu. Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake."(Yeremia 10: 12-13).Yesu alionyesha uwezo wake wa Kimungu juu ya ulimwengu kwa kutuliza bahari kali (Mathayo 8:26). Pia ni kweli kwamba kuna sheria za asili zinazofanya kazi katika mazingira yetu; hii ni mifumo iliyoundwa na Mungu (Mwanzo 8:22). Mungu aliumba ulimwengu wetu; dhambi ya binadamu iliiharibu (Warumi 8: 19-22). Hata hivyo Mungu bado anashikilia ulimwengu wetu pamoja (Wakolosai 1: 16-17). Hakuna miungu inayofanya kazi hiyo.
Jambo lingine la ajabu ni kwamba 'uasilia wa ulimwengu' ni namna ya mke / mshirika wa Mungu na anaongoza mbinguni pamoja naye. Dhana hii ya "mama na mungu baba " inavyoonekana katika mila ya Katoliki inayoashiria kwamba Maria kuwa "malkia wa mbinguni." Hata hivyo, Biblia inasema kwamba Mungu, katika utatu wa Mungu, anatawala mbingu na dunia peke yake (Danieli 4:25). Ulimwengu ni uumbaji Wake na Yeye peke yake anaimarisha na kulinda na, kwa kufanya hivyo, Anathibitisha wema na ukarimu wake. "Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha."(Matendo 14:17).
English
Je! Wazo la uasilia wa ulimwengu ni la Kibiblia?