settings icon
share icon
Swali

Torati ni nini?

Jibu


Torati ni neno la Kiebrania linalomaanisha "kuagiza." Torati inahusu vitabi vitano vya Musa katia Biblia ya Kiebrania/ Agano la Kale (Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati). Torati iliandikwa takriban 1400 kabla ya Kristo. Kijadi, Torati imeandikwa kwa mkono kwenye hati ya kuviringisha na "karani"(mwandishi). Haina hii ya hati inaitwa "Sefer Torati." Uchapishaji wa kisasa wa Torati katika mfumo wa kitabu "Chumash" (inayohusiana na neno la Kiebrania inayomaanisha nambari 5).

Haya ni maelezo ya vitabu vitano vya Torati kwa ufupi:

Mwanzo: Kitabu hiki cha kwanza cha Torati kinajumuisha sura 50 na kinashughulikia kipindi cha wakati kutoka uumbaji wa vitu vyote hadi wakati wa kifo na mazishi ya Yusufu. Inajumuisha simulizi ya uumbaji (sura 1-2), mwanzo wa dhambi ya binadamu (sura ya 3), Nuhu na Safina (sura ya 6-9), mnara wa Babeli (sura ya 10-11), maisha yake Ibrahimu, Isaka, na Yakobo na hadithi ndefu ya maisha ya Yusufu.

Kutoka: Kitabu hiki cha pili cha Torati kinajumuisha sura 40 na kinashughulikia kipindi kutoka utumwa wa Kiyahudi huko Misri hadi utukufu wa Bwana uliposhuka juu ya maskani iliyokamilishwa jangwani. Inajumuisha kuzaliwa kwa Musa, tauni sa Misri, Wayahudi kutoka Misri, kuvuka Bahari Nyekundu, na Musa kupewa Sheria juu ya Mlima Sinai.

Mambo ya Walawi: Kitabu cha tatu cha Torati kinajumuisha sura 27 na kina sheria kuhusu dhabihu, matoleo, na sherehe kati ya watu wa Israeli.

Hesabu: Kitabu hiki cha nne cha Torati kinajumuisha sura 36 na kinashughulikia kipind cha miaka 40 wakati Waisraeli walikua wanazunguka jangwani. Katika kitabu cha Hesabu tunaona kuhesabiwa kwa watu wa Israeli na maelezo kadhaa kuhusu yao kuelekea Nchi ya Ahadi.

Kumbukumbu la Torati: Kitabu hiki cha tano cha Torati kinajumuisha sura 34 na kinajukijana kama "Kumbukumbu la Torati" kulingana na neno la Kiyunani linalomaanisha "sheria ya pili." Katika kitabu hiki, Musa anarudia Sheria kwa kizazi kipya ambacho kingeingia katika Nchi ya Ahadi. Kumbukumbu la Torati kinaelezea mabadiliko ya uongozi wa makuhani ( kutoka kwa Haruni kwenda kwa wanawe) na kitaifa( kutoka kwa Musa kwendwa kwa Yoshua).

Vitabu vitano vya Torati vimeunda msingi wa mafundisho ya Kiyahudi tangu wakati wa Musa. Waandishi wa baadaye wa Biblia, Pamoja na Samweli, Daudi, isaya na Danieli, wangerejelea tena kwa mafundisho ya Sheria. Mafundisho ya Torati hufupishwa mara kwa mara kwa kutaja Kumbukumbu la Torati 6:4-5, inayoitwa Shema (au "kusema"): "Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako." Yesu aliita "amri kuu na tena ya kwanza" (Mathayo 22:36-38).

Torati inachukuliwa na Wayahudi na Wakristo kuwa Neno lililo na pumzi ya Mungu. Wakristo hata hivyo wanaona Yesu Kristo kama utimilifu wa unabii wa Masihi na wanaamini kuwa Sheria ilitimizwa katika Kristo. Yesu alifundisha, "Msidhani ya kuwa nimekuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza" (Mathayo 5:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Torati ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries