settings icon
share icon
Swali

Je, Agano Jipya la ubatizo linafananishwa na tohara?

Jibu


Tohara ilikua ishara ya kimwili katika agano ambalo Mungu alipea Ibrahimu. Ingawa agano halisi lilikua limepeanwa katika kitabu cha Mwanzo 15, tohara haikua sheria adi kwenye kitabu cha Mwanzo 17- angalau miaka 13 badae, wakati Ishimaili alizaliwa. Wakati huo, Mungu alibadilisha jina la Ibrahimu kutoka 'Abram'(maana yake, "baba aliyeinuliwa"), akawa Ibrahimu ( maana yake, "baba wa umati" ), jina ambalo lilitarajiwa kutimiza agano la Mungu. Agano hilo lilifanywa na Ibrahimu alafu badae kwa Isaka na Yakobo na kwa vizazi zote.

Kwa maana fulani, batizo ni ishara ya Agano Jipya ambalo Mungu anafanya na kanisa yake. Yesu aliamuru batizo katika tume kuu ya wanafunzi wake: " Kwa ivo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" (Mathayo28:19). Batizo ni ishara ya nje ambayo inaashiria mabadiliko ya ndani. Inawakilisha kuzaliwa tena kwa Kristo.

Tamaduni mingi ambazo zimebadilika zinaonyesha ukaribu au kufananisha tohara na batizo kwa kutumia mafunzo ya agano la kale kuhusu tohara ili kuhalalisha batizo kwa watoto wachanga. Mjadala unaendelea kuwa: kwa sababu watoto ambao walizaliwa kwenye agano la kale katika jamii ya wayahudi walipashwa tohara, ina maana kuwa watoto ambao wanazaliwa katika Agano Jipya wanafaa kubatizwa.

Ingawa kuna kufanana kati ya batizo na tohara, izi ni ishara amabazo zinaashiria agano mbili tofauti. Agano la kale lilikua likitendeka kwa njia ya kimwili yani mtu alikua anazaliwa na wazazi ambao ni wayahudi ama kuchukuliwa kama mfanyakazi katika nyumba ya myahudi (Mwanzo 17:10-13). Maisha ya kiroho ya mtu haikua inaambatana na ishara ya tohara. Kila mwanaume alipashwa tohara awe mwaminifu au si mwaminifu kwa Mungu. Hata hivyo katika agano la kale, imetambulika kwamba tohara ya kimwili haijatosha. Musa aliwaamuru waisraeli katika kitabu cha Deuteronomia 10:16 wapashe mioyo zao tohara, na akapeana ahadi kuwa Mungu mwenyewe atafanya iyo tohara( Deuteronomia 30:6). Jeremaya pia alihubiri akiimiza umuhimu wa kupata tohara ya roho (Yeremia 4:4)

Kwa kulinganisha, Agano Jipya liko na maana ya kiroho, yani lazima mtu awe mwaminifu na mwokovu( Matendo ya mitume 16:31). Kwa hivyo, maisha ya kiroho ya mtu imeambatana kwa ukaribu na ishara ya ubatizo. Ikiwa batizo inaashiria kuingia katika Agano Jipya, ina maana kuwa wale tu ambao wanamwabudu Mungu na kumwamini Yesu ndio wanafaa kubatizwa.

Tohara ya ukweli, jinsi Paulo anahubiri katika kitabu cha Warumi 2:29, ni ile ya moyo, na inakamilishwa na roho. Maana yake; siku izi mtu anaingia katika agano na Mungu si kwa matendo ya kimwili bali kwa kazi ya roho ndani ya moyo.

Wakolosai 2:11-12 inarejelea mfumo huu wa tohara: " Katika Kristo mmetahiriwa kwa kuondelewa hali yenu ya asili ya dhambi. Hii si tohara inayofanywa kwa mikono ya binadamu bali inafanywa na Kristo, mlizikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu". Tohara hii haihuzishi kukatwa kwa mwili bali ni kuziacha zile mienendo na tabia zetu za kitambo. Ni tendo la kiroho ambalo linaashiria wokovu ambao unaongozwa na Roho Mtakatifu. Batizo, jinsi imetajwa katika kifungu cha 12,haifananishwi na tohara bali inafuata tohara-na ni wazi kwamba ni tohara ya kiroho inayorejelewa. Kwa hivyo, batizo ni tohara ya ndani ya kiroho.

Fungu hili pia linaashiria kuwa maisha mapya ambayo yanawakilishwa na batizo inakuja kupitia imani yako.Hii ina maana kuwa mwenye anabatizwa ana uwezo wa kuonyesha imani yake. Kwa kuwa watoto hawana uwezo wa kuonyesha imani basi hawafai kua wanafunzi wa ubatizo.

Anayezaliwa (kimwili) katika agano la kale alipokea ishara la agano hilo (tohara); vilevile, anayezaliwa (kiroho) katika Agano Jipya ('kuokoka' Yohana 3:3) analipokea hilo ishara la agano (ubatizo)

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Agano Jipya la ubatizo linafananishwa na tohara?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries